BUSH BIN LADEN
JF-Expert Member
- Mar 16, 2019
- 8,628
- 19,810
Kwema wana jukwaa?
Kuna jamaa yangu kakumbwa na mkasa amenisumulia nimebaki kinywa wazi.
Ni hivi jamaa anaishi na mke wake na ndoa haina muda mrefu akiwa anajishughulisha na kazi za miradi ambayo huwa inamfanya awe mtu wa kusafiri sana.
Sasa jamaa huwa ana utaratibu wa kuja na gunia la mkaa anaporejea nyumbani kama kawaida ya wanaume tulio wengi tunapotoka safarini kuja tumebeba chochote kwa ajili ya familia zetu.
So siku hiyo amefika toka safari akaja na mkaa kama kawaida akapokelewa, mkewe kamtengea maji bafuni. Jamaa kaoga amemaliza kakaribishwa mezani kwa ajili ya chakula. Mkewe kaongoza sara na mwisho jamaa kafungua hotpot ili apakuwe. La haula si kafungua hotpot kakutana na mkaa.
Jamaa akiwa kapigwa na mshangao si akauliza hiki ni kitu gani, mke akamjibu ni mkaa. Jamaa anauliza ndo nini sasa kunitengea mkaa, mke anajibu nimekutengea mkaa liwe funzo maana unaona mahitaji ya humu ndani ni mkaa tu kwamba kila ukirudi kutoka safari unachoona cha muhimu sana ni gunia la mkaa.
Jamaa kauliza sasa kwani shida iko wapi, mke anajibu shida ipo kwa sababu mkaa hua unahitaji vitu vipikwe ili kupata chakula kwahiyo nilitegemea wakati unakuja mara zingine uwe unabeba mchele, ndizi, maharagwe, kuku nk.
Jamaa akabaki mdomo wazi si ndo kunisimulia nikamuuliza kwani hivyo vitu kama mchele, maharagwe nk havipo nyumbani jamaa kadai vipo na hata kama havipo hua anaacha hela ya mahemezi anaposafiri.
Kiukweli mpaka hapa hapa sijaona kwanini jamaa katengewa msosi wa mkaa kwenye hotpot.