PetCash
JF-Expert Member
- Mar 20, 2012
- 1,995
- 2,017
Kuna jamaa mmoja ni rafiki yangu sana. Sasa kuna mdada mmoja jamaa alimpenda na wakawa na uhusiano.
Dada akamwambia jamaa anatafuta kazi. Jamaa kamfanyia mpango hadi akapata kazi (Na kwenye process hiyo ndo jamaa alikubaliwa). Baada ya miezi mitatu msichana akawa mjamzito. Jamaa anaishi peke yake akaniomba ushauri. Aitoe au aiache na dada ahamie kwake( kwa sababu dada anaishi kwa kaka yake na atarudishwa kwao nje kidogo ya Dar ikitambulika).
Nikamuambia kuitoa ni mbaya sana lakini pia kuishi pamoja ni mipango ambayo wanatakiwa kuongea na si kwasababu ya mimba. Sasa kumbe dada hajampenda jamaa kivile so akakataa kuishi naye na mimba hakutoa lakini. Dada akaacha kazi akarudi kwa wazazi wake. Sasa wazazi wakawa kama wamemtenga fulani hivi akawa anaishi kwenye chumba cha peke yake mbali kidogo na home.
Sasa nadhani wanapishana sana kwenye matumizi jamaa anayotuma. Dada akawa ananicall niongee na mshikaji. Jamaa hayuko na idea hata huwa anamtumia kiasi gani kwa sababu anatuma elfu 20, labda mara nyingine 40, 10, 5,.
Nikamwambia awe anamtengea fungu lake la mwezi ndo poa. Akaniuliza kiasi gani. Hapo ndo nimeshindwa kumjibu kwa sababu mimi hata ukiniuliza nyumbani zinatumika shillingi ngapi naona zinatofautiana sana mwezi kwa mwezi.
Saa nyingine naweza mpa wife hela hata c za mshahara ziwe zimepitia benki ama yeye anaweza tumia hela alizopata nje ya mshahara asahau kuniambia. Nimeuliza kwa rafiki zangu ila wengi ndo kama mimi double income family. Sasa jamani kwa wenye uzoefu jamaa anaweza kutuma shillingi ngapi kwa mwezi?