Kwa umri wangu huu japo kwa udogo wake nimejifunza kuna watu wana hulka mbaya pengine mapepo machafu kutokana na maisha wanayoyachagua. Wengine kutokana na ushirikina au kushirikiana na mapepo machafu. .
Hapo kaona sawa kunidhalilisha na kunitusi hanijui simjui sijawahi kusemeshana nae wala kufahamiana kwa aina yeyote. Labda anafanya hivyo kutafuta umaarufu au tabia tu au mapepo yakishakuwa ndani ya nafsi ya mtu huwa anafanya mambo ya ovyo ila kwake anaona sawa. Kazi ya shetani si ndogo ni kubomoa tu na kuleta chuki na huitaji sababu yeyote kutaka kukuangamiza. .
This is humanity in this century these desperate times. If someone can hate who he knows nothing of, how about those they know? Sad indeed. .