Jalada kesi ya EPA halijarejeshwa Kisutu

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,322
33,126
JALADA la kesi ya wizi wa Sh6 bilioni za Akaunti ya Madeni ya Nje(EPA), ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), inayowakabili washtakiwa watano bado halijarejeshwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutoka Mahakama Kuu ya Tanzania.

Hakimu Frank Moshi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu alieleza hayo jana alipokuwa akiahirisha kesi hiyo ilipotajwa mahakamani hapo ikiwakabili Bahati Mahenge, Manase Mwakale, Davies Kamungu, Godfrey Mosha na Eddah Mwakale.

Hakimu Moshi aliiahirisha kesi hiyo hadi Aprili 23, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa tena na kuangalia iwapo jalada hilo litakuwa limerudishwa au la ili washtakiwa hao waanze kutoa utetezi wao kwa mashtaka yanayowakabili baada ya mahakama hiyo kuwaona wana kesi ya kujibu.

Kabla ya kuahirishwa kwa kesi hiyo, mshtakiwa Manase aliikumbusha mahakama hiyo imrudishie hati yake moja kati ya mbili alizozitumia kwenye dhamana yake akitoa sababu kuwa, hati moja inatosheleza kukamilisha kiwango cha dhamana walichopewa.

Kuhusu ombi hilo, upande wa mashtaka haukuwa na pingamizi, lakini Hakimu Moshi alimtaka awasilishe ombi hilo mbele ya jopo kwa sababu yeye siyo hakimu husika kwenye kesi hiyo.
Kesi inasikilizwa na jopo la mahakimu watatu, linaloongozwa na Hakimu Sekela Moshi.

Mahenge na wenzake kwa pamoja wanadaiwa kuwa kati ya mwaka 2003 na 2005 walikula njama kuiibia Benki Kuu ya Tanzania, Sh6,041,899,876.45 baada ya kudanganya kuwa kampuni yao ya Changanyikeni ilipewa deni na Kampuni ya Marubeni ya nchini Japan.

Jalada kesi ya EPA halijarejeshwa Kisutu
 
Back
Top Bottom