Jakaya Kikwete na msafara mkubwa

Bususwa

JF-Expert Member
Sep 30, 2021
429
1,011
Toka mwaka mpya umeanza nipo kusini mikoa ya Lindi na Mtwara napambana na maisha yangu yakujiandaa na uzee wangu, maana kula na tafuna kabisa mfupa ukiwa bado na meno mdomoni, hapa maana yangu nikufanya kazi kwa nguvu zote nakujiandaa kwa ajiri ya uzee!

Basi bwana, jana nikiwa pale Lindi hospitali ya Mkoa, Sokoine! Nikaona msururu wa magari yakipanda kwenda kule juu Mtanda! Polisi wa usalama barabarani wakizuia magari ili ule msafara uweze kupita! Basi bwana kuna jamaa akaniambia huyo ni Kikwete yupo hapa ana siku zaidi ya 3!

Leo asubuhi mida ya saa tano hivi,nikaanza safari yakurudi zangu Dodoma! Nikiwa njiani dereva aliona gari ya polisi inakuja kwa kasi mno,ikiashiria tupishe njia, bila hiyana dereva alipisha! Ukapita msururu wa magari yakiwa yanatembea kwa mwendo kasi sana!

Basi tukafika pale SOMANGA! Tukayaona yale magari yakiwa yamesimama kwa pembeni kuna watu wengi, nami nikatupa jicho nikamuona Mzee Kikwete akinunua samaki pale, sababu pale ni sehemu ya kula chakula,tukasimama pale,tukala na Mzee Kikwete aliingia hadi ndani ndani kabisa kununua samaki!

Basi sisi tukaanza safari tukawaacha wao pale, kabla hatujamaliza mpaka wa Lindi na Pwani, tulimkuta pale RPC wa Pwani akisubiri msafara ule aupokee na RPC wa Lindi arudi zake Lindi!

Sasa swali langu, kwa nini Mzee Kikwete ana msururu wa magari mengi vile?? Yaani zilikua gari zaidi ya 10! Na zote ni V8 VX na gari yake Nissan VX zile walizopewa marais wastaafu!
 
Rais mstaafu hua ana gari tatu tu! Moja ya kwake, Moja spare na moja walinzi!
Ndio mnavyodanganywa hivyo mtaani?

Hivi unajua kuwa rais aliyopo madarakani au msataafu akipata tatizo lolote awapo safarini nje ya mkoa anaoishi lazima RPC wa mkoa husika awe responsible?

Na je RPC huyo anatakiwa kuwa na gari ngapi za ku escort msafara wa raisi?

Na je RPC anaweza kuusindikiza na kuusubiria msafara wa rais alafu RTO awe kalala tu na mkewe nyumbani?

Hopital ya mkoa watajibu nini endapo raisi atapata ugonjwa wa ghafla na kukosa huduma kwa kutokutoa ambulance?

Nimekufungua macho kidogo tu but ukiona anatumia gari 10 jua hana mambo mengi la sivyo kwa uchache ni gari 15+ zinahitajika kuwepo kwenye msafara
 
sasa wewe mwenyewe ulishamwita rais mstafu alafu unauliza tena kwanini ana msururu mrefu wa magari na magari yenyewe hayazid 20
Paul Kagame alishwahi kumwambia hivi , “ I will wait for you at the right place and time, then i will hit you!” , nadhani bado anakumbuka hii kauli, wacha ajilinde, yasije kumkuta ya Mtikila.
 
Kila nikiwa pale kwangu Kawe Beach na yeye akiwa anatoka kwake,huwa naona gari tatu na pikikipi moja tu.
bro nmeongelea kikwete akiwa kwenye safari nje ya mkoa anaokaa.

na hata hapo kawe unaposema unaonaga akiwa kwenye gari tatu tu huenda ikawa ni macho yako lakini kiuhalisia katika kila mataa au makutano huwa kuna gari iko hapo mda mrefu kabla ya yeye kupita
 
Back
Top Bottom