Jakaya Kikwete: Mkapa hakupenda sifa (populism)

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
7,197
2,000
Kwa mujibu wa hii speech (eulology) aliyoitoa JK kwenye msiba wa BWM, imetusaidia kujua Mkapa alikuwa ni mtu wa namna gani. Licha ya kufanya mambo makubwa katika nchi lakini hakutumia kabisa vyombo vya habari vya Taifa kujipigia mapromo kama tunavyoona kwenye utawala wa sasa.

Ifahamike Mkapa ndiye rais wa kwanza aliyekataa title ya "Mtukufu"

Na ni rais wa kwanza wa nchi yetu aliyekataa picha yake kukaa kwenye fedha

Huyo ndiye rais aliyekuwa hapigi mayowe, bali aliacha watu waone wenyewe.

Na kweli mwanaume yule alipiga kazi ya maana kwa nchi.

Namkumbusha rais wa sasa na wapambe wao, chema chajiuza kibaya chajitembeza, acheni kupiga mayowe, tuacheni tuone wenyewe.

"Na hiyo ndo tatizo la kustukizwa"

Video hapa chini:

The Elephant

JF-Expert Member
Dec 18, 2014
4,164
2,000
Hii speech ndo iliyoharimu mood ya jamaa- jamaa kasahau kuwa wote wamechaguliwa na Watanzania na ni haki yao kuchagua wanachotaka

Chintu

JF-Expert Member
Feb 4, 2011
5,178
2,000
Vyote vipo. Vya kuona na vya kusikiliza mayowe.
Kama huoni basi kereka na Mayowe, na kama unaona Unaona basi achana na Mayowe.
Uhuru ni wako.
 
mngony

JF-Expert Member
Jul 27, 2012
3,629
2,000
Populism maana yake siyo sifa, acha kujiokotea maneno ambayo wala hauelewi maana yake, ungeacha tu neno sifa peke yake, kwa maana,,populism“ ina maana nyingine kabisa na wala haifit kwenye ujumbe wako, ...
Tuelimisha Kada
 
Shehullohi

JF-Expert Member
Jul 21, 2020
557
500
Kweli hakupenda sifa ndio maana katika kitabu chake maadhui ni kutaka sifa ziwaendee Wataalamu wa shauri wake. Akimanisha hasa sifa zile zinazohusisha mapuñgufu ya utawala wake.

Kama hili halitoshi akaomba atafutiwe picha ya rafiki yake Waziri mkuu wa zamani wa Sweden ili iwe sehemu ya yaliyo jumuishwa katika kitabu chake. Maana hakutaka makuu na sifa za kujikweza kuweka picha za malofa na wapumbavu.
 
Ndinani

JF-Expert Member
Aug 29, 2010
6,023
2,000
Populism maana yake siyo sifa, acha kujiokotea maneno ambayo wala hauelewi maana yake, ungeacha tu neno sifa peke yake, kwa maana,,populism“ ina maana nyingine kabisa na wala haifit kwenye ujumbe wako, ...
Nielewavyo mimi “ populism” maana yake shauku ya kutaka kusifiwa. Itapendeza kama utatueleza maana tofauti na hii.
 
Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
21,550
2,000
Nielewavyo mimi “ populism” maana yake shauku ya kutaka kusifiwa. Itapendeza kama utatueleza maana tofauti na hii.

Hiyo siyo maana ya populism, populism maana yake siyo sifa, unaweza usipende Sofa na bado ukawa populist na kinyume chake, ...
 
Bome-e

JF-Expert Member
Jan 3, 2014
12,929
2,000
Populism maana yake siyo sifa, acha kujiokotea maneno ambayo wala hauelewi maana yake, ungeacha tu neno sifa peke yake, kwa maana,,populism“ ina maana nyingine kabisa na wala haifit kwenye ujumbe wako, ...
Aliyomaanisha JK ndiyo hiyo ya sifa,maana ametafsiri kabisa na kwa kiswahili! So alichokusudia kusema kimefika barabara!
 
Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
21,550
2,000
Aliyomaanisha JK ndiyo hiyo ya sifa,maana ametafsiri kabisa na kwa kiswahili! So alichokusudia kusema kimefika barabara!

Lakini populism tafsiri yake siyo ,,kupenda sifa“ angeweza kutumia tu neno sifa bila ya populism, ...
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom