Travelogue_tz
JF-Expert Member
- Sep 28, 2010
- 855
- 1,224
Habari wadau: Ni maoni yangu lakini pia naamini kuwa ndio fikra za wenye akili timamu. Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika moja ya hotuba zake maalumu aliwaahidi Watanzania zawadi ya katiba mpya, Katiba ambayo itatutoa hapa na kutupeleka miaka 50 ijayo. Na katika kusherehesha hotuba yake alisisitiza juu ya upya wa katiba vs kuweka viraka katiba iliyopo, na alisema kuwa Hata nguo inapowekwa viraka huwa haipendezi.
Ni katika nyakati hizo umaarufu wa JK uliongezeka zaidi na kudhaniwa kuwa pengine mchakato huu utafunika udhaifu wake wa muda mrefu wa kiutendaji. Mara kadhaa imekuwa ikitafsiriwa na wadau wa maendeleo kuwa JK ameshindwa kutoa utumishi bora kama ilivyotimainiwa wakati anaingia madarakani 2005.
Mchakato huu wa katiba mpya umekumbana na changamoto nyingi japo Rasimu ya Tume ya Warioba ilirejesha matumaini kwa kujenga mazingira ya utaifa, uzalendo na uwajibikaji. Kibaya na cha kusikitisha ni mjenzi mwenyewe Mhe. Rais Jakaya Kikwete alipovaa vazi la Kijani ndani ya BLK na kuanza kuponda, kulaani,kutisha, na kutoa maelekezo kwa wajumbe wa BLK kana kwamba yupo katika kikao cha NEC.
Akipigiwa vigelegele alitupa koti la Urais na kubaki na T- Shirt ya Kijani huku akisisitiza kuwa ndani ya utawala wake hakuna Serikali 3. Akiendelea kupigiwa meza kwa nguvu alisisitiza kuwa Serikali tatu inaweza kupinduliwa na Jeshi. Baada ya hotuba ile ya CCM ndani ya BLK watu wenye akili timamu wakaanza kuona mkwamo wa katiba mpya. Kutokana na kitendo kile ni wazi sasa JK amepoteza uhalali wa kuwa msuluhishi kwa kuwa chanzo cha tatizo.
Na hatima yake ile NDOTO ya kuwaletea Watanzania katiba mpya imetoweka kama tu NDOTO ya Maisha bora kwa kila Mtanzania ilivyokwama na kuhitimishwa kwa kisingizio cha TIMIZA Wajibu wako.