Jakaya Kikwete kuzika Historia yake?

Jakaya Kikwete kuzika Historia yake?

@ Notradamme, Kwanza nimi sio ke ni me, mbili acha matusi ujiheshimu, tatu JK alipokuta uozo alichukua hatua gani???
 
Vladmir Mkuu nakuuliza hata kama hakikuwa kipindi chake alichukua hatua gani??
Kumficha Gavana wa BoT Balali USA, au kuwasamehe wezi hao wa EPA, kina Rostam &CO ??
 
Last edited by a moderator:
Unapo kuwa kiongozi mkubwa ambae unaongoza watu wengi katika nchi unapaswa kuwa na misimamo yako lakini hupaswi kuiweka wazi katika mchakato wowote unaotegemea mawazo ya wale unaowaongoza.

Ni vyema angekaa kimnya na kusikiliza wananchi wanataka nini..
 
Jk anania nzuri na mapenzi makubwa na nchi yake wanaomnyima uwezo wa kufikia malengo yake ni wana CCM wenzie kwa sababu zao mbalimbali.


Habari wadau: Ni maoni yangu lakini pia naamini kuwa ndio fikra za wenye akili timamu. Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika moja ya hotuba zake maalumu aliwaahidi Watanzania zawadi ya katiba mpya, Katiba ambayo itatutoa hapa na kutupeleka miaka 50 ijayo. Na katika kusherehesha hotuba yake alisisitiza juu ya upya wa katiba vs kuweka viraka katiba iliyopo, na alisema kuwa Hata nguo inapowekwa viraka huwa haipendezi.

Ni katika nyakati hizo umaarufu wa JK uliongezeka zaidi na kudhaniwa kuwa pengine mchakato huu utafunika udhaifu wake wa muda mrefu wa kiutendaji. Mara kadhaa imekuwa ikitafsiriwa na wadau wa maendeleo kuwa JK ameshindwa kutoa utumishi bora kama ilivyotimainiwa wakati anaingia madarakani 2005.

Mchakato huu wa katiba mpya umekumbana na changamoto nyingi japo Rasimu ya Tume ya Warioba ilirejesha matumaini kwa kujenga mazingira ya utaifa, uzalendo na uwajibikaji. Kibaya na cha kusikitisha ni mjenzi mwenyewe Mhe. Rais Jakaya Kikwete alipovaa vazi la Kijani ndani ya BLK na kuanza kuponda, kulaani,kutisha, na kutoa maelekezo kwa wajumbe wa BLK kana kwamba yupo katika kikao cha NEC.

Akipigiwa vigelegele alitupa koti la Urais na kubaki na T- Shirt ya Kijani huku akisisitiza kuwa ndani ya utawala wake hakuna Serikali 3. Akiendelea kupigiwa meza kwa nguvu alisisitiza kuwa Serikali tatu inaweza kupinduliwa na Jeshi. Baada ya hotuba ile ya CCM ndani ya BLK watu wenye akili timamu wakaanza kuona mkwamo wa katiba mpya. Kutokana na kitendo kile ni wazi sasa JK amepoteza uhalali wa kuwa msuluhishi kwa kuwa chanzo cha tatizo.

Na hatima yake ile NDOTO ya kuwaletea Watanzania katiba mpya imetoweka kama tu NDOTO ya Maisha bora kwa kila Mtanzania ilivyokwama na kuhitimishwa kwa kisingizio cha TIMIZA Wajibu wako.
 
Wewe!!, ni mwananchi wa wapi ambaye umeongea naye akakuambia anaiunga mkono CCM na rasimu yake yenye serikali 2??, Mbona nyie CCM mnapenda sana kuwalisha maneno wananchi wa Tz.Kitu unachokiwazia wewe unakibadili na kuwa ndiyo mawazo ya wananchi wote wa tz!!!!!!.Huu ni uenda wazimu na ulimbukeni wa siasa.

Achana nae huyo, MaCCM wanajulikana wanatapatapa kuokoa CCM yao sasa kwa kuo ndio wanaoongoza dola wanatumia kila aina ya hila kuokoa ulaji wao!!!!! nani hajui hilo, wamejua wakiruihusu serikali tatu wamekufa kifo cha mende kwa maana hao opponents watajipanga kuchukua nchi. OK, Mi nataka serikali moja ambayo itaniletea mkate wa siku nyumbani kwangu!!!!!!
 
Kwa hiyo Dr.Godbless Jakaya Kikwete hana la kukumbukwa?
Kama ndivyo,basi tumekuwa na miaka kumi ya hasara,tumefanya biashara kichaa?
 
Tanzania ni nchi masikini sana duniani,demokrasia ina gharama zake,kwa hali halisi mhe alimiscalculate kuichagua tume ya jaji Warioba.Wale watu wana akili sana.Unapomchagua mtu mwenye akili sana pengine hata kukuzidi wewe tegemea changamoto nyingi Tume ya jaji Warioba imejaa wasomi wenye akili sana na wakweli na wenye kumuogopa Mungu,namfahamu msomi Paramagamba Kabudi mtoto wa mchungaji jaji Agostino Ramadhani baba yake alikuwa askofu mkuu,marehemu dr Mvungi asiye na woga wa kile anachokiamini mzee Butiku na Salim A Salim na wengine kadha ni watu wasiokurupuka.Uzalendo wao ni kusema ukweli. Mheshimiwa raisi watu hawa ni makini.Kwa sababu ya umasikini wa nchi yetu hii ya Tanzania baada ya rasmi ya kwanza bunge la katiba lingetumia muda muchache kujadili hatimaye iletwe kwa wananchi waipigie kura.Nashangaa nguvu nyingi zinatumika kubishana serikali 3 au 2 kana kwamba wao ndio watu wa mwisho kuamua.Maana waamuzi wa mwisho ni sisi wapiga kura,iweje leo wajumbe wa BMLK ndio waendesha mashtaka wao mawakili wao mahakimu ni wao.Kuna siku nilisema hawa jamaa wanatumia delay tactick ili waendelee kutanua pale mjengoni.Mwisho wa siku watupe kitu kibovu na sisi wananchi tutaikataa. Watanzania ni watu wavumilivu lakini hizi kelele zinavyoongezeka zinaanza kufungua masikio ya wengi mh rais ni bora ukavunjilia mbali hili BMLK itafutwe njia nyingine ya watu kutoa maoni yao bila gharama kubwa isijefika mambo yakashindwa kwenda kwa serikali kuishiwa fedha.Mbona hata humu jf kuna maoni mazuri tu bila gharama
 
I appreciate every good things Kikwete has done for this beautiful country, the desire for change I see in him including the New Katiba movement. But kulinda maslahi ya chama ndio kunakomuangusha most of the times
 
Wezi wamemkaba koo labda kitakacho muokoa aseme kama noma na iwe nouma mambo yatakwenda sawa na atawekwa kwenye kumbukumbu nzuri daima apitishe maoni ya wana nchi na siyo ya wezi
 
Kwani mtu akikwambia ujiandae kisaikolojia anamaanisha serikali tatu? Unatumia tafsili gani ya lugha.
Hivi mtu akikwambia ujiandae kisaikolojia kuna msiba unkuja anamaanisha nini..?
 
Unashangaa nini kwani wewe ulimchagua Kikwete, wewe rais wako Slaa.

Unalalamika nini sijui wakati haukumchagua.
Ivi watu wengine huwa mnajua mnachoandoka kweli..?!
 
Back
Top Bottom