Jaji Werema: Ambaye hataki muungano ni mwendawazimu

BASI KUMBE JAJI WEREMA NDIYE MWENDAWAZIMU WETU NAMBA MOJA KATIKA HILI!!!

Kama hivyo ndivyo mambokweli yalivyo basi kumbe Mwendawazimu wetu namba moja ni Jaji Werema kwa maana kwamba kwa vitendo vyake sibaki na shaka yoyote kichwani mwangu kwamba huyu baba hapendi kabisaaa Muungano wetu niipendayo ikiboreshwa na sisi wenye wananchi wa Bara na Visiwani kwenye Katiba Mpya.

Hoja yangu ya kunifanya niamini hivyo ni kule katika kuhoji kwangu kwamba ileje yeye kama mshauri mkuu wa serikali katika masuala ya kisheria awe anairuhusu serikali ya Muungano kupanga, kuketi na kujadili na hata kuyatolea maamuzi masuala ya ki-Muungango bila ya mmbia muhimu Zanzibar kukamilisha picha nzima???

Iweje kila leo awe anazunguka kwenye vyombo vya habari bila kuonekana akiandamana na hata mtu mmoja kutoka katika kambi ya wabiya wetu katika Muungano???

Kumbe adui wa kweli wa Muungano si mwingine bali ni huyu huyu Jaji Werema and by extension, kwa maneno yake mwenyewe, ni mwendawazimu!!!
 
Mbona kuna wendawazimu wanaoupenda muungano, bila kujali kasoro zake. Mbona kuna wenye akili timamu wanouchukia muungana na wana sababu zao. Perception do differ, kwani wanasheria hawasomi saikilojia.:help:
 
Mheshimiwa Jaji Werema Hakuna asiyeutaka muungano bali wanachi wanataka matatizo ya muungano yatatuliwe kwa haraka jombo gani hilo lisilokwisha kama kweli lina mslahi ya jamii kwa nini hamtatui matatizo tatueni matatizo na si kuwatukana wananchi eti ni wendawazimu, maana hao wakiamua kuuvunja muungano wanaweza ila wantumia busara na wewe usiwaite wananchi wendawazimu maana je wakikwita na wewe mwendawazimu utajisikiaje ? tatueni matatizo ya wanachi na sio kuwaita wendawazimu
 
Alishaonesha uendawazimu wake tokea mswada wa katiba alivyoutetea halafu Waliomteua wakakubali kasoro zake na kuutoa kwa aibu, anaendeleza uendawazimu wake katika suala la Muungano. Haja jipya, kazi kujikomba kwa Baba yake anayempa ugali JK.
 
Back
Top Bottom