Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Akizungumza kuhusu suala hilo, Warioba amesema tathmini ya matumizi ya nguvu inapaswa kuangaliwa kwa uhalisia, hususan kwa kuzingatia idadi ya vifo vilivyotokea. Ameeleza kuwa maandamano yamesababisha vifo vingi, jambo linalozua maswali kuhusu aina ya maandalizi yaliyofanywa na vyombo vya ulinzi na usalama.
Soma: Jaji Warioba: Waliouawa Oktoba 29, 2025 ni wengi kuliko waliouawa kwenye Vita ya Kagera
Kwa mujibu wa Warioba, kwa takribani miaka miwili vyombo hivyo vilikuwa vimeelekezwa kujiandaa kusimamia mchakato wa uchaguzi ili uwe huru, wa haki na wa amani. Hali hiyo ilisababisha wananchi kudhani maandalizi hayo yalikuwa kwa ajili ya kudhibiti hali endapo kungetokea vurugu.
“Hivyo basi, tunajiuliza: walijiandaa vipi? Je, walijiandaa kwa bunduki na risasi? Kwa sababu hizo ndizo zimeonekana kutumika zaidi,” amesema Warioba.
Ameongeza kuwa kinachopaswa kujadiliwa ni aina ya maandalizi yaliyofanyika na kama nguvu iliyotumika ililingana na mazingira halisi ya tukio. Kwa maoni yake, matumizi ya silaha za moto dhidi ya waandamanaji wasio na silaha za kisasa yanahitaji kuwekewa wazi ili jamii iweze kufanya tathmini ya haki.
“Hapa unashughulika na vijana ambao hawana silaha za kisasa, lakini wewe una bunduki na risasi, unatumia nguvu na kuua. Basi matukio haya yawekwe wazi ili tuweze kuamua kama kweli nguvu iliyotumika ilistahili. Kwa maoni yangu, hali ilikuwa tofauti."
Video: Jamhuri TV