Jaji Warioba kuna skendo yoyote ya rushwa, matumizi mabaya ya ofisi, unyanyasaji, kujilimbikizia mali nk amewahi kutuhumiwa nayo?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
909
4,215
Tumezoea kusikia mema ya Jaji Warioba kila kukicha. Amesifiwa na CcM , upinzani na wanaharakati.

Mimi nimezaliwa mwaka 1963 na kwa mantiki hiyo nimeshuhudia akiwa kiongozi na akiwa nje ya uongozi. Katika kukua kwangu sijawahi kusikia akituhumiwa may be kwa sababu wakati wa Mwalimu Nyerere Siri zililikuwa Siri kweli.

Naomba kufahamu ili tumfahamishe ni wapi unaamini aliwahi kuvurunda? Tumwambie sasa may be siku akiandika kitabu chake atatueleza kwamba alivurunda kwa utashi wake au alisukumwa kuvurunda.

Tumchambue mzee wetu aweze kufahamu ubaya wake may be kupitia ubaya huo anaweza akatupa mwanga ni nini kilizalisha huo ubaya.

Ninachojua tu mzee anaishi kwa raha kwa sababu anakula kile roho inapenda, hana makuu na anapenda kushirikiana na makundi yote.
 
Akiwa PM Kata yake iliwahi pata Umeme na Mortuary kabla ya Makao Makuu ya Wilaya Bunda..
 
Back
Top Bottom