Jaji Warioba kukutana na wahariri kesho Jumanne Karimjee saa 3:00 asubuhi - 7:00 mchana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jaji Warioba kukutana na wahariri kesho Jumanne Karimjee saa 3:00 asubuhi - 7:00 mchana

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwalwimle, Jun 18, 2012.

 1. M

  Mwalwimle Member

  #1
  Jun 18, 2012
  Joined: Oct 19, 2011
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Wakuu,


  Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mstaafu Joseph Warioba kesho, Jumanne, Juni 19, 2012 atakutana na Wahariri wa Vyombo mbalimbali vya Habari katika Ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar es Salaam kuanzia saa 3:00 asubuhi - 7:00 mchana kwa lengo la kuzungumza naokuhusu kazi ya ukusanyaji wa maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya.


  Mkutano wa aina hiyo pia utafanyika mjini Zanzibar katika Ukumbi wa Hoteli ya Bwawani keshokutwa Jumatano, Juni 20, 2012, kuanzia saa 3:00 asubuhi kwa Wahariri waliopo Zanzibar. Pamoja na Mwenyekiti wa Tume, katika mikutano hiyo ya wazi kwa Waandishi wa Habari pia watakuwepoWajumbe wengine wa Tume.

  Katika mikutano hiyo, Mwenyekiti wa Tume atafafanua kazi za Tume, kama zilivyoainishwa katika Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 nanamna Tume inavyozitekeleza.

  Tume ya Mabadiliko ya Katiba imeanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83, na Wajumbe wake waliteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 6 Aprili na aliwaapisha tarehe 13 Aprili mwaka huu. Tume ilianza kazi rasmi tarehe 1 Mei, 2012.

  ----------------------

  Omega S. Ngole,
  Principal Information Officer,
  Constitutional Review Commission (Tanzania),
  Ohio Street,
  PO Box 1681,
  Dar es Salaam,
  Tel: +255 (0) 22 2133425,
  Fax: +255 (0) 22 2133442,
  Mobile: +255 (00 757 500800

   
 2. s

  slufay JF-Expert Member

  #2
  Jun 18, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,372
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  znz walindwe na ffu maana wako tofauti na agenda yenu wao wanataka znz huru
   
Loading...