Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,609
- 218,032
Hii ndio Taarifa mpya iliyosambazwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa Nchini Tanzania .
Kwamba viongozi wa vyama vyote vya Siasa nchini Tanzania wanaombwa kufika Ikulu tarehe 03/01/2023 ili kuonana na kuongea na Rais Dkt Samia Suluhu , kwenye Ukumbi wa Jakaya Kikwete , kuanzia saa 3 asubuhi .
Kila Chama cha siasa kimeombwa kufika na viongozi wanne wa Juu , Mwenyekiti , Makamu Mwenyekiti , Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu .
Nimeona Barua ya mwaliko huo kutoka ofisi ya Msajili kwenda kwa vyama vya siasa , bali Hakuna maelezo yoyote kuhusu ajenda zitakazojadiliwa , Lakini tunadhani kwamba Masuala ya Katiba Mpya , Tume Huru ya Uchaguzi , Mikutano ya hadhara na Maandamano vyaweza kuwa ajenda kuu .
Ngoja tusubiri .