Jaji Ramadhani: Mniombee mapenzi ya Mungu yatimie

Jaji Ramadhani: Mniombee mapenzi ya Mungu yatimie

Jaji Ramadhani hizi ni zama za NURU kuongoza, utawala wa giza hauna nafasi tena. Sisi tunamwomba Mungu jambo hili lipate kibali chake nawe ukawe mteule wake utakayeliongoza taifa hili la maziwa na asali yaani Tanzania. Penye nuru giza hutoweka lenyewe, WEWE NI NURU!!
 
Sidhani kama ni mapenzi ya Mungu, zaidi ya mapenzi ya wale wote waliomshawishi kugombea.
 
Atuambie kadi ya ccm alikuwa anailipia?...
Ana uadilifu gan ktk kutenda haki wakat alipokuwa jaji huku ni mwanaccm?
 
Mheshimiwa alikuwa kwenye taasisi iliyotopea kwa rushwa japo hiyo taasisi inatakiwa iwe mbele katika kupambana na rushwa. Sasa sijui ata shughulika vip na ufisadi akiwa rais.

Mbona miaka yote hakuwa maarufuku kwa hilo na rungu na nafasi alikuwa nayo tena Pana tu?
 
kwanza atujibu swali kabla ya kuombewa, Pesa za Escrow ni za umma au sio za umma?
 
rais wa tanzania -mzanzibar
rais wa zanzibar- mzanzibar

hiyo hatutaki,awe makamu rais wa MAGUFULI
vinginevyo ccm hawana wabunge mwaka huu,
 
hivi watu vijijini wanamjua hadi sasa amefanya nini katika taifa hili tunachoweza kukiona na akaomba kura tukampa?cv ya kutumika mahakama ambazo ndo zinatunyanyasa na kutunyima haki na kuwapa wenye pesa,anapoteza muda ccm watashinda kwa shida .
 
anachukia rushwa wakati alikuwa anatumikia mahakama na mahakama ndo zinaongoza kwa kura rushwa,ajipange upywa,nafasi yake makamu wa rais basi,rais mtanganyika mwenzetu,
 
Kama akitaka tumuombee naomba kwanza apokee masharti yetu mawili:

1.Kama akiingia madarakani avunje Tume ya Uchaguzi na asaidie kupelekwa Bungeni sheria ya kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi.

2.Baada ya hili kufanyika avunje Bunge na kuanza uandikishwaji upya kwa kutumia tume huru ya uchaguzi ili watanzania tuwachague viongozi kwa uhuru bila mazingizra hatarishi na kutishana.

Kama upo tayari kwa haya mawili,tukubaliane kwa maandishi na kiapo,basi tutakuombea upite huko kwa Chama Cha Majasusi
 
agh huyu katumwa na ccm ili kupunguz kura za FISADI edward lowassa
 
Atuambie kadi ya ccm alikuwa anailipia?...
Ana uadilifu gan ktk kutenda haki wakat alipokuwa jaji huku ni mwanaccm?


Afadhali angegombea kama mgombea binafsi, kwa CCM, hapana, tutakuwa na shaka..
 
CCM wamepofuka ..hivi ni nani kawadanganya watanganyika wanamtaka huyu mzee amabaye hajawahi hata kutwambia msimamo wake juu ya rasmu ya Warioba, ile rasmu iliharibiwa wazee wenzie wakaingia front wakatwambia ukweli wala yeye hakuwahi kuwa nao tukajua alikuwa na msimamo gani sasa leo anajigeuza ana mahaba na mustakabari wa nchi yetu, wallah hatukubali, taasisi yake ilinuka rushwa ikamshinda na akawalinda wanunua haki alafu leo anaitaka Ikulu yetu? wallah huyu tena ndo sitaki hata kumsikia ..hatuwezi kuichezea Ikulu yetu kiasi hiki, Hatufai katu.
 
hivi watu vijijini wanamjua hadi sasa amefanya nini katika taifa hili tunachoweza kukiona na akaomba kura tukampa?cv ya kutumika mahakama ambazo ndo zinatunyanyasa na kutunyima haki na kuwapa wenye pesa,anapoteza muda ccm watashinda kwa shida .

Mkapa mlikuwa mnamjua?!
 
Mkapa mlikuwa mnamjua?!

Mkapa kama si mwl Nyerere Ikulu angeishia kuisikia na unatakiwa uelewe watu walimchagua Mkapa kwasababu walimwamini Mwalimu kama Baba Wa Taifa na wakaamini baba yao hawezi kuwatakia mabaya. Sasa hayo ndugu zangu yamekwenda, hayapo tena, CCM ya leo hayupo mwenye kuwwza kumuuza Ramadhani na akaeleweka kwasababu Mwl. ndo alikuwa mtu wa mwisho msafi kati ya viongozi wa kitaifa na aliyeaminika kwasababu ya staili ya maisha yake aliyokuwa anayaishi, aliamua kuishi matendo yake ...Ukawa tunaichukua nchi asubuhi.
 
Back
Top Bottom