Jaji Ramadhani: Mniombee mapenzi ya Mungu yatimie

Jaji Ramadhani: Mniombee mapenzi ya Mungu yatimie

Fortunatus Buyobe

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2011
Posts
463
Reaction score
1,130
Mgombea urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Jaji mstaafu Augustino Ramadhani amewataka Watanzania kuendelea kumwombea ili mapenzi ya Mungu ya kumfanya kuwa kiongozi wa Taifa yatimie.

Jaji Ramadhani alisema hayo jana wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Dayosisi ya Dar es Salaam. Katika sherehe hizo, mgombea huyo alikuwa mgeni rasmi akiambatana na Dk Mwele Malecela ambaye pia anawania nafasi hiyo.

Jaji Ramadhani, ambaye ni mchungaji wa kanisa hilo alisema haikuwa mapenzi yake kutangaza nia ya kugombea urais, bali alipata msukumo kutoka kwa Mungu mwenyewe.

"Kila siku watu wananipongeza kwa kujitokeza kuwania urais. Ninawaambia safari bado ni ndefu, wazidi kuniombea ili mapenzi ya Mungu yatimie," alisema.

Azungumzia rushwa

Kiongozi huyo alisema rushwa imekuwa tatizo kubwa nchini na kubainisha kuwa yeye anachukia na hata Mungu pia haipendi.

Alisema CCM imekuwa ikipambana na rushwa chini ya msemo wake ‘rushwa ni adui wa haki' na kuwataka wananchi wabadilike na kuepuka rushwa.

Awali akimkaribisha Jaji Ramadhani, Askofu wa Dayosisi ya Dar es Salaam, Dk Valentino Mokiwa alimpongeza kwa kujitokeza kuwania urais, akisema kati ya waliojitokeza, yeye ameonekana kuwa na karama nyingi.

Alisema Jaji Ramadhani amekuwa ni Kasisi wa Kanisa la Anglikana, aliwahi kuwa Brigedia Jenerali, alikuwa Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu na pia ni Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu.

"Tuko nyuma yako, tunakuombea kwa Mungu ushinde nafasi ya urais ili utende haki na kupambana na rushwa," alisema Askofu Mokiwa.

Askofu Mokiwa alisisitiza kuwa wala rushwa wote wafungwe bila huruma ili kuondoa tatizo hilo.

Alipoulizwa kuhusu Jaji Ramadhan kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo licha ya kuwa yeye ni kasisi tu wa kanisa hilo, mjumbe wa kamati ya maandalizi ya sherehe hiyo, Mchungaji John Kamoyo alisema uamuzi huo unatokana na uhusiano kati ya Jaji Ramadhani na Askofu Mokiwa.

"Majibu ya swali hilo ni mengi, lakini nadhani ni uhusiano tu kati ya Askofu Mokiwa na Jaji Ramadhani. Kuna mambo mengi lakini nisingependa kueleza hapa," alisema Mchungaji Kamoyo.

Chanzo:
Mwananchi
 
.
CCM itakuwa chama cha upinzani ikiwa huyu jamaa atateuliwa kukiwakilisha chama.Anakubalika na system na sio wanachi(Nahisi harufu ya Usaliti akipitishwa huyu padre.jaji.mwanajeshi).

Mtu aliyetumwa na System;akiwa Rais ataitetea system iliyomuweka(Mfano wa Bibi KIROBOTO hivi karibuni).
Watanzani wanataka rais aliyetumwa na wao ili awatetee wao.

Acheni kumdhihaki Mungu.Sema Mapenzi ya Mafisa** yatimie na sio Mungu.Waliojitoa kwa Mungu hubakia kanisani hadi vifo vyao.HUYU Ana tamaa ya madaraka;Anaacha upadre na kurudi ktk siasa za kifisadi
 
ili lowassa asipite kila mtia nia anaonekana bora apite kuliko lowasaa
hlfu bado kuna mijitu inajiita migreat thinkers even a simple research and reasoning is hard for them

hata huyu ambae akiwa judge kaonyesha upendeleo kwenye chama kimoja anaonkn bora
 
Ramadhani anajua fika kuwa waombaji hawapeleki jina kwa Mungu bali wanapeleka mahitaji.
1 . Rais mwenye hofu ya Mungu
2. Mpenda amani...
3. Mweledi wa mambo..

n.k

Kama ni mcha mungu kutoka rohoni,asingeacha upadre na kuja ktk siasa za kuwatetea na kuwalinda mafisadi!.Ana tamaa ya madaraka.
 
Kaitwa na Mungu!!? Mnafiki mkubwa. Kashawishiwa na majambazi ya magamba anamsingizia mungu! Akagombee huko kwao
 
Mapenzi ya Mungu ni Kwa Jaji Augustino Ramadhan kushindwa na hapo arejee kanisani kumtumia Mungu.
Tamaa zake za madaraka zimemfanya akimbie madhabahu, na namwomba sana Mwenyezi Mungu ahakikishe huyu Jaji anashindwa vibaya tena kwa aibu kubwa.
 
Nmeamini huyu Mzee apendwi akuna anaye kubaliana na maamzi yake
 
the banker

Huyu naye aache Usanii. Ni mtu wa hovyo sana niliyewahi kumwona tangu alivyoboronga ile hukumu ya Mgombea Binafsi. Akagombee ubunge Zanzibar huko sisi hatumuhitaji
 
Last edited by a moderator:
Nani wa kukuombea kwa unafiki wako......katika nchi mbili hizi hakuna rais wa tanganyika ambaye atatoka zanzibar elewa hili.Rais wa tanganyika atakuwa mtanganyika.

Yaa point na ni kwanini mtanganyika hajawahi tawala zanzibar!?
 
Jaji katika ujaji wake atupe sehemu moja tu aliowahi kufanya maamuzi kwa maslahi ya wananchi
 
Wote mnaombeza huyu jaji ni washenzi, Kamwe Lowassa wenu hawezi kutoboa
 
Mapenzi ya Mungu akaendelee na kazi ya Mungu kanisani na pia kupiga kinanda
 
Back
Top Bottom