Jaji Prof. Ibrahim Hamis Juma katika Utendaji

Mkuu Frei, asante kwa hili. Umenikumbusha zile lori mbili za semi trella zilizobeba 40ft contena mbili zenye karatasi za kura ziliziopigia CCM zikitokea Malawi!. Au zile meli mbili kubwa zilizojazwa shehena ya majambia!.

Kuna watu humu ni watumwa wa upofu wa mapenzi yao upande wao!. Their vision is unidirectioinal, wanauwezo wa kuona upande mmoja tuu!. Na their sight ni myopic, mwisho wao wa uoni ni humo humo ndani ya box walimo!.

Paskali.
 
...Vuta Nkuvute...you may have a point...lakini ulitakiwa uje humu na trend nzima ya maamuzi ya huyu jaji....kwa kuangalia kesi ..at least 10 alizofanyia ruling....toka akiwa mahakama kuu...hadi alipohamia mahakama ya rufaa....Inawezekana kabisa ukawa na point kumhusu huyu jaji...

Issue hapa si quality (by profession)ya jaji...bali bias katika maamuzi(ruling).....hili linawezekana kabisa....Nadhani kwa vile umeamua kufunguka kuhusu huyu jaji...ni vizuri ukajaribu kwenda deeper...kuchimba ruling zake zilizopita...haswa zile zilizohusisha kesi kati ya wana ccm...serikali...na upinzani(member wa upinzani)....

Kuna uwezekano pia yale mambo ya danganya toto kwenye ruling za mwanzo mahakama kuu yakawa yanafanyika.....kwa kuja ku balance baadaye kwenye appeal court....Labda watu wamesahau kwamba kuna list of shame ya Mh.Lissu inayohusu majaji wenye controversies kwenye high court.......haswa linapokuja swala la teuzi zao....ni angalizo tu...

anything can happen in TZ.....
 
Kwa ninavomjua prof Juma, kiukweli we mleta mada unamuonea, ni mtu makini, hapendelei mtu, ni mchapa kazi asiye na mfano...yaani yuko fit kila idara...kwanza hata judgment zake zimeanyiwa research na judge ambaye sio mvivu........

Kuna majaji wengine watakaa na kesi miaka nenda rudi lkn yeye yuko kazini akiwaambia ni hukumu ni hukumu kweli, hana cha kuahirisha wala nini.....

Nahisi ndio mana akapanda haraka kwenda court of appeal...ni jembe anachapa mzigo baba wa watu hebu mwacheni au mwamuonea wivu nini?

Tz km tungekuwa na majaji wote km huyu basi mahakamani kusingekaa kesi miaka 10.....
 
Jk ni bingwa wa kulipa fadhila huyu naye na uprof wake atachafuliwa tu,,,,,,,Jk anachafua wenzake af anakaa pembeni! Big up JF imekuwa sorce ya kuaminika Tanzania!
 

JK hapashwi kusamehewa katu, amefanya maovu mengi
 
Haya matoto ya Bavicha sijui nani kayaroga porojo tu kwahiyo jaji mzuri ni yule anayesimamia kesi halafu chadema wakashinda huyo ndo mzuri matoto majinga hatari.
 
Hivi kwanini wengi mliosoma hapo UDSM hamko vizuri katika fikra kabisa...I doubt the credibility of UDSM
 
Kwa sababu tumepoliticise kila kitu, uamuzi wowote in favour of Chadema then huo ndio uamuzi wa haki!. Uamuzi wowote in favour of CCM ni upendeleo!.Pasco.
Tatizo tutatibu dalili za maradhi badala ya maradhi yenyewe.

Kutoaminiana hadi kufikia vyombo vya sheria kutiliwa shaka ni hatua ya kusikitisha.

Hata hivyo kuna sehemu mbili za kujadili

1. Vyombo vya sheria:
Kumekuwepo na mtazamo usiopendeza juu yake

Hili linachangiwa kwa sehemu na vyombo vya sheria ''kupoteza'' nguvu kama mhimili

Matukio yanayoendelea hasa ya siasa yanatia shaka hata pasipohitaji shaka

Kwa maneno mengine, trust na vyombo vya kutoa sheria ipo tofauti na matarajio

2. Hatuwezi kupata suluhu ya jambo hili hadi tutakapobadili mfumo

Jaji mkuu anapaswa kupitia katika 'vetting' nyingine

Nchi za wenzetu mtu akiwa Jaji, kwanza hawezi kuondolewa, pili anawajibika maeneo mengine si kwa eneo moja

Kwa mtazamo huo hakuna mhimili 'uliozama' zaidi chini, na yote inakuwa huru

Tuangalie hili la Jaji wa sasa. Wadhifa wake anakaimu Ujaji mkuu hadi uteuzi kamili

Hii si nafasi ya kukaimu, si kuwa inamkwaza mhusika, inajenga mashaka bila ulazima.

Jaji kwa kukaimu anakuwa na conflict of interest.
Kulinda masilahi ya taasisi lakini kama binadamu naye ana matarajio binafsi

Likitokea jambo maamuzi ya Jaji yataweza kuunganishwa na 'ukaimu'

Kwavile mfumo wetu ni mbovu, unatoa fursa tu ya mteuzi kuamua lini afanye hivyo

Hivi Jaji Othman aliamka tu na kutoa taarifa au kulikuwa na taarifa siku nyingi?

Kwanini nafasi ya Ujaji mtu akaimu?

Kwa umuhimu wake katika nchi na utawala hili linatokeaje?
 
Mzee tupatupa haya mambo adimu unayajuaje .. hongera sana ..ongezea kabia mwendokasi nakuja kulipa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…