Jaji Mutungi, sakata la UDA na ESCROW, majaribio kwa spidi ya Rais Magufuli

Mpangawangu

JF-Expert Member
Mar 5, 2014
887
965
Wakuu, kadri siku zinavyokwenda ndivyo dhamira ya uchapaji kazi ya Rais wetu kipenzi Dkt. John Pombe Joseph Magufuli inavyoingizwa Majaribuni.

Kwa namna alivyojisimika kwa umma, Rais JPM hamuangalii mtu usoni anapotaka kufanya maamuzi hasa yenye maslahi kwa umma.(Rejea Kitwanga's Sagga).

Tofauti na ilivyozoeleka na inavyotarajiwa kwake, kwa sasa inaonekana wazi Rais ameanza kuingizwa kwenye majaribio ya kushindwa kusimamia misimamo na njia zake anazozitumiaga kuwawajibisha wabadhirifu, nitafafanua

1. KASHFA YA JAJI MUTUNGI
Msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji Fransis Mutungi ndio kiongozi wa kwanza wa serikali inayoongozwa na JPM kufungua mwaka mpya wa 2017 kwa kashfa ya kutakatisha zaidi ya milioni 360 za Chama cha CUF na kuingizwa kwenye akaunti ya wilaya na baadae kwa mtu binafsi.

Tayari katibu mkuu wa CUF ambaye kisheria ndiye msimamizi na muwajibikaji mkuu wa fedha za Chama hicho ametangaza kutoitambua akaunti iliyoingiziwa fedha hizo wala utaratibu na kwamba ofisini kwake Kuna barua ya msajili inayomuelekeza kuzuia Ruzuku ya Chama hicho kutokana na mgogoro unaoendelea.

Tayari pia bodi ya wadhamini ya Chama hicho imetangaza kutoitambua akaunti hiyo na kupingana na kitendo cha msajili wa vyama vya siasa na kumtaka awajibishwe.

Kwa mtazamo wangu, Msajili wa vyama hakupaswa kuendelea kukalia kiti anachokalia mpaka sasa.

Kitendo hicho kinaashiria kwamba msajili anashirikiana na serikali kumsaidia Lipumba kuihujumu CUF.

Serikali makini kama ya JPM haipaswi kuingizwa mkenge katika mambo ya namna hii yanayofanyika kwa uzembe na tamaa za watu binafsi kama kina Mutungi na wenzake.

2. SAKATA LA UDA
Awali ilisemwa chini chini kwamba Rais JPM hajafurahishwa na namna biashara ya UDA ilivyofanyika.

Ilisemwa kwamba Rais amekataa mara kuzindua mradi wa mabasi ya mwendokasi kwa sababu za uasilia wake wa mauziano ya shirika la UDA ambayo kila mwenye akili timamu anafahamu kuwa ni dili.

Haijulikani Rais Amedanganywa nini na Nani kiasi cha kukubali kwenda kuzindua mradi huo, uzinduzi unaoonyesha na kuthibitisha uhalalishaji wa Ufisadi uliofanywa na wanafamilia ya vigogo fulani hapa nchini.

Jiji la DSM sasa wanaambiwa wapange matumizi ya mgao wao wa bilioni 5.8 kama sehemu ya mauzo ya hisa zao 51%.

UDA wanamtia Majaribuni JPM shirika kama hili Thamani tu ya jina lake 'BRAND' la UDA katika imani ya matumizi ya biashara ya Usafiri jijini Dar na Tanzania kwa Ujumla inavuka hiyo bilioni 5.8 bado Mali zake, viwanja, magodauni nakadharika.

Tumshauri Rais asiyakubali majaribu haya, aendeleze msimamo wake UDA haijauzwa kihalali, UDA imeuzwa kiujanja ujanja na Rais anatumika kuhalalisha biashara hii ya ujanja ujanja.

3. SAKATA LA ESCROW NA IPTL

hili sio jipya, limeshasemwa Sana na likaamuliwa na Bunge kwa kuadhimiwa maazimio 8 ya Bunge.
Itoshe tu kusema serikali inapata hasara ya mabilioni ya shilingi kila siku kugharamia uendeshaji wa kampuni hii ya IPTL.
Gharama za 'capacity charges' ambazo serikali kupitia Tanesco inailipa IPTL kila siku ni zaidi ya milioni 400.

Milioni 400 hizo hulipwa hata kama siku hiyo umeme haujazaliswa, ni dili kubwa Sana hili. Milioni 400 kwa siku? .. Bado tunashangaa kama nchi kwanini umeme unapanda bei kila kukicha really? .

Rais JPM huu ni mtego ama majaribu yake mengine. Wala Rais haitajiki kuwatumbua IPTL. anachotakiwa kufanya ni kusimamia utekelezaji tu maazimio ya Bunge.

Rais wetu mpendwa. Mwaka huu wajanja wamekuanzishia kwa majaribu mawili, la JAJI MUTUNGI na la UDA. hili la ESCROW umelilithi.

Kadri siku zinavyozidi kwenda majaribu haya yataongezeka kutoka matatu ya sasa mpaka matano, kumi na kuendelea.

Wako
Msema Kweli
 
halafu wakishinda kwenye chaguzi za vijijini huko wanafurahi wameugaragaza upinzani wakati kila leo wanawaanzishia makesi na kuwafunga bado viongoz wa ngazi za kimkoa walioteuliwa na mtukufu mbinu chafu zinatumila kutawala taifa hili sio mapenz ya wananchi kwa ccm ila ni vyombo vya dola ndo vinaifanya ccm kuwepo hapo
 
Lumumba wakija utakoma.Maana kwao hawataki kusikia kwamba Mtukufu sana amezidiwa na wajanja wa Mafisi ndani ya Chama chake cha Majangili.

Umesahau yule mtoto wa mbunge aliyetoka kwa fine ndogo kabisa pamoja na kuhujumu uchumi wa Taifa kisa ati ni mwenzao
 
Nimeishia nilipokutana na neno " Raisi wetu kipenzi" huko kungine wengine waendelee kusoma!
 
mutungi hamjaribu bali anatekeleza maelekezo yake hivyo hatamtumbua bali kumpandisha cheo......escrow/iptl ni miradi ya ulaji ya ccm atafumbia macho.............uda itaendelea kupigwa danadana kwani wlaji ni makada wa ccm
 
Kuhusu UDA ckuna mtu ameeleza jinc wtu walivyopew mzigo kasoro Mdee pke yk ss Mkulu anahuska vp tna?
 
0792f4a4ffebd4da554bdc1634499331.jpg
 
Makaburi Yaliyopita na ya sasa... bora angeanza na makaburi ya zamani ili kuweka msingi mzuri kuzuia/kupunguza makaburi mapya.

Hivi Makaburi yakizidi sehemu moja nini hufanyika?
 
Toka mwanzo niliamini hakuna kiongozi atakaetokana na ccm alafu apambane na ufisadi.nilitambua magufuli anafanya maigizo tuu kwan nae ni wale wale.ndio maana anajitahidi kuzuia uwazi,kuzuia vyombo vya habari kufanya kazi zake ili kuficha madhambi yake huku akiendelea kuwadanganya wajinga wajinga wa nchi hii ambao ndio mitaji ya ccm.
 
mutungi hamjaribu bali anatekeleza maelekezo yake hivyo hatamtumbua bali kumpandisha cheo......escrow/iptl ni miradi ya ulaji ya ccm atafumbia macho.............uda itaendelea kupigwa danadana kwani wlaji ni makada wa ccm
CCM oyeeeee.
 
Sijui kuhusu UDA , lakini nina uhakika kwamba iko siku moja miongoni mwa hizi hizi siku alizoumba Mwenyezi Mungu , Francis Mutungi atakuja kufungwa jela .
 
Huyo alipata mgao na inawezekana wapo wengi maana bwana yule anatetewa sana
 
Hivi uda kumbe imeuzwa eeeh?mimi nilidhani kuwa jamaa wamenunua hisa asilimia 51 na serikali wana asilimia 49?uliza basi hata hapo kwa jirani yako hii inamaanisha nini,sio kubwabwaja tu kuwa uda imeuzwa!!!kwa jinsi nilivyomuelewa JPM ni kwamba ameanzisha mahakama ya ufisadi kama ngao ya kujikinga na vitendo vya kifisadi katika kipindi chake cha utawala.na kweli anaelekea kufanikiwa kwani kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa hatujaona skendo kubwa ya kifisadi iliyotokea tangu aingie madarakani mmebaki kuibua zile zile za awamu zilizopita na kumshinikiza azishughulikie.kumbukeni waliongia mikataba hiyo walijua wanachokifanya so ni lazima waliweka na vipengele vya kujilinda likitokea la kutokea na kwa sababu walishirikiana na watawala wa kipindi hicho hili lilifanikiwa ipasavyo.sasa mtu unaangalia gharama ambazo nchi itaingia kwa kuvunja mkataba kama wa iptl na kuacha urun hadi mwisho ipi ni afadhali,unaona kuacha urun ni afadhali basi unaacha tu mambo yanaenda.we angalia tu kwa mfano wapambe ambao ndio tunawaamini wakijumuisha wapinzani waliibana serikali kuhusu dowans ikaingia mkenge jamaa wakaja wakasema tufanye biashara tuwauzie hii mitambo wapambe wakagoma na serikali ikaingia mkenge kilichokuja kutokea imebaki story!!leo hii wapambe hao hao wanakuja na ale yale lakini awamu hii wanailenga iptl,wanailazimisha serikali iingie mkenge kama ilivyokuwa kwa dowans na sie tulivyo wajinga kila siku tunasimama upande wa wapambe hawa!!!hadi kesho nchi hii inalipa deni la dowans ambalo ni zaidi ya mara nne ya bei waliotaka kutuuzia hiyo mitambo(hapo tunalipa na mitambo sio yetu,ni fidia tu) na wapambe hawa wamenyamaza wakati sisi tunaumia!!!so wakati wapambe hawa wanaendelea kuipigia seriakali kelele a kuvunja mkataba wa iptl tuwahoji ni kwa namna gani tunaweza kuepuka ya dowans yasitukute na huku pia!!!
 
Back
Top Bottom