Jaji Mtungi inabidi tukae kikao! Yamemshinda

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,862
106,788
Jaji Mtungi na mlezi wa vyama vya siasa yameanza kumshinda!

Amenukuliwa na magazeti akisema kuwa suala la mkanganyiko wa kufanya mikutano ya kisiasa ni suala la sekretariat na sio la kwake peke yake.

Ameyasema hayo baada ya kutaitiwa na waandishi wa habari kuhusu kauli za Magufuli na mikutano ya Ole Sendeka huko Arusha.

Wakati huo huo Ole Sendeka amejibu kuwa anatekeleza ilani ya CCM inayotaka viongozi wafanye ufuatiliaji wa utekelezaji wa ilani
 
nchi haiongozwi kwa ghadhabu,hasira na visasi! ukitaka kuua upinzani fanyeni kazi vizuri simamieni vizuri watu watarudisha imani kwenu,then acheni watu wawakosoe mnapokosea!lkn mkipenda kushangiliwa majukwaani kwa kauli zenu za ubabe basi kumbukeni kuna sheria na katiba ya nchi!
 
Bila katiba bora tutaendelea kuwa na viongozi wa ajabu ajabu kama huyu jaji. Anashindwa kusema ukweli kuwa anachofanya Rais Magufuli ni ubakaji wa demokrasia, matokeo yake Msajili anajiuma uma tu ili kulinda ugali wake.
 
Ukiua upinzani ni wakina nani watatoa mawazo mbadala na fursa ya vyama mbadala?

Hapa sioni sababu ya kufikiria kuua upinzani bali wafikirie jinsi ya kufanya shughuli pamoja ili kuendeleza Tanzania yetu
 
Huyu Jaji ni kichwa sana, lakini kwa bahati mbaya Mungu aliweka hisia za njaa kutokea tumboni..........kuna wakati kwa sababu hiyo watu tunalazimika kuhamishia akili yetu kwenye tumbo ili TULE.............njaa ile ndugu zangu.
Nawahimiza watoto wangu wasomee kazi wanazoweza kujiajiri..........kwa circus hizi za JPM, ningetegemea kuona baadhi ya wateule wake wakijiuzuru. hivi wote wanakubaliana na vitimbwi hivi?
 
Hata wakifanya kazi nzuri kupita hata malaika,Upinzani lazma uwepo,Hebu niambieni ni nchi gani duniani haina chama cha upinzani ukiacha Korea Kaskazini ambayo ni kidikteta?
China, Cuba, Vietnam,Saudi Arabia, morocco.
 
Nachukua nafasi hii kutangaza kumdharau moja kwa moja Francis Mutungi kwa kipindi chote alichobakiwa nacho hapa duniani .
 
Huyu Jaji ni kichwa sana, lakini kwa bahati mbaya Mungu aliweka hisia za njaa kutokea tumboni..........kuna wakati kwa sababu hiyo watu tunalazimika kuhamishia akili yetu kwenye tumbo ili TULE.............njaa ile ndugu zangu.
Nawahimiza watoto wangu wasomee kazi wanazoweza kujiajiri..........kwa circus hizi za JPM, ningetegemea kuona baadhi ya wateule wake wakijiuzuru. hivi wote wanakubaliana na vitimbwi hivi?
Swali zuri sana !
 
Back
Top Bottom