The Phylosopher
JF-Expert Member
- Mar 11, 2015
- 1,906
- 2,885
Licha ya mikwara ya kutumbua majipu bado wapo mawaziri hawajajaza fomu ya maadili inayowataka kujaza fomu za mali zao.
Ikiwa kweli Rais JPM amedhamiria kukomesha uzembe na kufanya kazi kwa mazoea nashauri aanze na hao.
Ikiwa kweli Rais JPM amedhamiria kukomesha uzembe na kufanya kazi kwa mazoea nashauri aanze na hao.
Wakati akitoa mada katika semina elekezi ya mawaziri na manaibu mawaziri leo, Kamishna wa Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Salome S. Kaganda kwa masikitiko alimweleza Waziri Mkuu kwamba kuna baadhi ya Mawaziri na Manaibu Waziri, ambao hawajajaza fomu za maadili mpaka leo, wakati Mheshimiwa Waziri Mkuu, Rais Mstaafu Kikwete na Mhe. Rais John Pombe Joseph Magufuli, ameshajaza fomu hizo. Jaji Salome Kaganda, alikabidhi majina ya Mawaziri husika. Sijui wana utetezi gani.
MAONI: Mheshimiwa Rais ni maajabu hawa mawaziri wanashinda kutumbua majipu, wakati kumbe wao pia ni majibu. Ili kuleta somo, mawaziri na manaibu waziri husika wanyang'anywe wadhifa wao.