Jaji Mkuu "awatosa" watuhumiwa wa Escrow

Jaji Mkuu "awatosa" watuhumiwa wa Escrow

Wezi wamejipanga kulipa visasi. Naona mratibu wa wezi Singasinga anataka kumfunga jela kamishna wa TRA kwa "kosa" la kudai kodi iliyokwepwa miaka mingi.
 
Acha waonewe,mbona sisi huku vijijini tunaonewa kila siku?
Ina maana huo u "silly" wa mahakama ndio mnauona leo kuhusu escrow? Hypocracy at its best!

Yaap! ndo unaona jinsi nchi hii ilivyo. Hata wale wanaojiita au kuitwa wasomi, ignorance hawaikubali kwamba kiasi fulani wanayo.

Pesa kweli sabuni ya roho. hata akina Mwanakijiji sasa wanajidai hawaoni ukweli! Au ni yale yale kwamba kuna ndugu kafaidika sasa basi!

Mahakama huwa haifuati ukweli. Mahakama inafuata sheria na siyo lazima kwamba sheria inasimamia ukweli na haki. Sisi tunafahamu Mahakama zinaachia wezi wakubawa tena ambao ukweli tunao. Hiyo inaitwa haki kwa upande wa mahakama ni ile haki ya kisheria. Sawa na unyongaji wa Hitler, ilikuwa haki kwa mujibu wa sheria za Nazi!

Majaji wameonyesha upuuzi lazima umma tuwahukumu. Bunge lilikuwa sahihi.
 
Jaji ana haki ya kusema alio yasema lkn Wananchi tunataka kujua mwisho wa Hili sakata.

Watoto wetu wanaadhirika Mashuleni Halafu Waziri aliyewekwa Kuangalia Haki zao Analipwa BILIONI 1.6?

Hapa hatoki mtu kimya kimya.

Mkuu nakukubali kwa jambo moja tu....

Ukiacha yote Una akili kubwa Sana.
 
Mtu mwingine yoyote anaweza kuidharau mahakama na kusiwe na impact yoyote!, lakini amini nakuambia, baada ya bunge ambalo ni mhimili, kuidharau mahakama ambayo ni mhimili mwingine, kutakuwa na a very huge impact!, subiria.

Pasco

Sidhani kama Bunge limedharau Mahakama,bali mahakama imejidharaulisha mbele ya jamii kwa watendaji wake wakuu( majaji) kujihusisha na rushwa ya dhahiri hivyo kujiondoa katika uaminifu.
Nakumbuka Lembeni alisema Bungeni kuwa taasisi pekee zinazoaminika kwa wananchi ni Bunge na JWTZ tuu. Lakini kwa matukio yaliyojitokeza ya wabunge nao kutuhumiwa kupokea rushwa kutetea ufisadi basi na Bunge nalo limeingia katika orodha ya wasioaminika.
Kwa usemi wa Lembeni maana yake ni kuwa Taasisi pekee iliyobaki kuaminiwa na kutodharauliwa nchi hii ni JWTZ. Ni kusema kuwa zingine zote yaani Ikulu,Polisi, mawizara, taasisi za dini nk nk haziaminiki tena. Hii sijui inaleta muono gani kwa nchi. Jee tuwape uongozi hao tunaowaamini?
 
hizi za ruge sikuziotea nami ningezilamba kwani naona Rais anakuwa rahisi kuwaonea huruma
 
Potelea mbali. Kwa nini wao tu wapate haki? Wafungwe tu. Kuna maelfu ya Watanzania wako jela bila haki tena hawakuiba hata senti moja, sembuse hawa wana kiwingu cha kuiba mamilioni? Nani maskini atafikiria hata kuiba milioni 10? Ni hawa hawa tu hakuna wengine. Tia kamba tu wao na wakubwa wao ambao bado hawaja...
 
Hatoki Muhongo,werema wala tibaijuka...ama zitto, mbowe nao watoke😛😡
 
ninachokiona mimi ni matumizi mabaya ya mahakama katika kunyima mijadala huru ndani ya bunge. Mahakama zisitumike kama vyombo vya kuwanyima wananchi haki ya kusikia maswala nyeti yanayowahusu. Kama bunge lingeridhia maamuzi ya mahakama, kila anayeona mambo yake yataguswa basi hatasita ukimbilia mahakamani kuweka zuio ili jambo hilo lisizungumzwe.

Tukifanya reference kwa Article 30 ya katiba utaona kwamba si sasihihi kwa maslahi ya wachache kunyima haki ya wengi kwa kuzingatia kwamba haki hiyo inasimama katika maslahi ya kitaifa, nanukuu hapa:

30.-(1) The human rights and freedoms, the principles of which are set
out in this Constitution, shall not be exercised by a person in a manner that causes
interference with or curtailment of the rights and freedoms of other persons or of
the public interest.

Hivyo basi Bunge lilifanya tafsiri sahihi ya ibara hii ya 100, ninainukuu :

100.-(1) There shall be freedom of opinion, debate and in the National
Assembly, and that freedom shall not be breached or questioned by any organ in
the United Republic or in any court or elsewhere outside the National Assembly.

Kwa kuzingatia kwamba, Wananchi wanayo haki ya msingi ya kikatiba ya kuhabarishwamambo muhimu yanayogusa maisha yao moja kwa moja:
18. Every person -
(a) has a freedom of opinion and expression of his ideas;
(b) has out right to seek, receive and, or disseminate information
regardless of national boundaries;
(c) has the freedom to communicate and a freedom with protection
from interference from his communication;
(d) has a right to be informed at all times of various important events
of life and activities of the people and also of issues of importance
to the society.

Jambo hili la escrow, lilikua lina gusia haki za msingi za watanzania, hivyo ilikua sahihi kwa wabunge kulijadili bila kuingiliwa na mhimili mwingine.

Si sahihi kwa mahakama kulinda haki za wachache kwa kutumia mamlaka yake na kunyima haki za wengine kwa kisingizio cha kuingiliwa uhuru wake. Swali ni je mahakma ipo tayari kuvunja katiba kwa kigezo cha kulinda uhuru wake??

Je mahakama haioni faida ya uwepo wa ibara ya 18, 30 na 100 ya katiba katika swala hili?? sidhani kama ni sahihi.

Tuache mijadala huru iendelee kwa ustawi wa taifa letu.

Mijadala ndio mwanzo wa suluhisho la matatizo mengi hata yale makubwa yaliyoshindikana hufanyika kwa njia ya mijadala.
 
This is silly; kama kweli mahakama "inapenda mtu apate haki" sasa mtu ambaye anaona Bunge linamkandamiza akimbilie wapi kupata haki? kwa Spika?

Yes anapaswa kurudi kwa Spika, Rejea ugomvi waMalima na Mengi, Wabunge wana Immunity ya kutoshtakiwakwa watachosemaBungeni
 
Tokea usiku ule niliona Mama Makinda anavyoposha jamii eti anaingilia uhuru wa mahakama. Kimsingi alikuwa anawalinda watuhumiwa akina pinda and Co.

Eti bunge letu haliwezi kumuangiza rais sasa hapo tumewatuma wakafanye nini kule kama rais atafanya anavyotaka ikiwa na wao wapo pale.
Jaji Mkuu, Mohamed Chande Othman, amevunja ukimya kuhusiana na sakata la uchotwaji wa zaidi ya Sh. bilioni 300 kutoka akaunti ta Tegeta Escrow iliyopo Benki Kuu ya Tanzania (BoT), akisema kuwa watuhumiwa wanamtumia ujumbe kulalamika wamehukumiwa bila kusikilizwa.

Jaji Chande alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam katika mkutano wa pamoja kati ya viongozi waandamizi wa mahakama wakiwamo majaji na wasajili na wahariri wa vyombo vya habari kujadili mahusiano na ushirikiano baina ya mahakama na vyombo vya habari.

Alitoa kauli hiyo kuhusiana na mjadala wa sakata hilo uliofanyika bungeni wiki iliyopita baada ya Mahakama Kuu kuzuia lisijadiliwe bungeni hadi kesi zinazohusu kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) zitakapoamuliwa na Mahakama Desemba 8, mwaka huu.

“Napata meseji nyingi kutoka kwa baadhi ya watu kuwa ule mjadala bungeni umeshawahukumu na kuwa hawana sababu za kwenda mahakamani kujitetea,” alisema Jaji Chande wakati wa kufunga mkutano huo.

Akizungumzia majadala huo alisema Mahakama iko nje ya Bunge na kwamba uhuru wa wabunge kuzungumza ndani ya Bunge unalindwa na Katiba ya nchi.

“Uhuru wa Mahakama hauko ndani ya Bunge, kama tutaongea tutakuwa tunaongea na nani. Tukiongea nje tutakuwa tunaongea na vyombo, huwezi kusahihisha hansad (rekodi za Bunge),” alisema Jaji Chande.

Aliongeza kuwa Mahakama haitakiwi kujihusisha na malumbano ya kisiasa kwa sababu huo ni mhimili mwingine na kwamba Katiba ya sasa na inayopendekezwa mahakama na watendaji wake hawatakiwi kujihusisha na siasa.

“Kwa Tanzania Katiba inayopendekezwa mahakimu, majaji wanatakiwa wasiwe wanasiasa na mahakama yenyewe isiingilie wanasiasa. Hilo ni zuio kubwa,” alisema.

Kuhusu ukimya wa mahakama wa shutuma zinazotolewa dhidi majaji, alisema ukimya haumaanishi kuwa inajilinda au jaji anajilinda, bali analinda lile lililomuweka ofisini.

Alisema mahakama inapenda mtu apate haki na haina upande wowote wa siasa.

Katika sakata la akaunti ya Escrow, miongoni mwa maazimio ya Bunge ni kuundwa kwa tume ya kimahakama ya kuwachunguza majaji wawili wanaodaiwa kuchotewa pesa na Mkurugenzi wa VIP Engeering & Marketing Limited, James Rugemalira.

Majaji hao ni Profesa John Luhangisa, anayedaiwa kupokea Sh. milioni 400 na Jaji Aloyce Mujulizi, anayedaiwa kupewa Sh. milioni 40.

Akizungumzia kesi mbalimbali zinazoripotiwa mahakamani, alisema kazi ya vyombo vya habari ni kuhakikisha kuwa habari hizo zinakuwa sahihi bila kupotoshwa ili mwananchi aweze kujenga imani na vyombo hivyo.

Alitoa mfano wa nchi ya India ambako alisema mwandishi hawezi kuandika habari za mahakama kama hana uelewa wa mambo ya mahakama.

Alisema pamoja na kwamba watu wanashutumu mahakama kupendelea upande fulani, lakini ikiangaliwa kesi za uchaguzi mahakama zinatoa haki bila kujali upande wowote wa siasa.

Jaji Othuman, pia alisema wanaangalia uwezekano wa waandishi wapiga picha kuruhusiwa kufanya kazi wakati kesi za madai zinaendelea katika kutoa habari za kina kwa umma.

Alisema wataweka taratibu na kanuni za kuwezesha utekelezaji katika kesi za madai zenye mvuto kwa jamii, na kuhusu kesi za jinai alisema itakuwa ngumu kwa kuwa zina mashahidi na wapo wenye kuhitaji usiri.

“Hoja kuu ni kupima uhuru wa taarifa na kupata taarifa moja kwa moja wakati kesi inaendelea, tuangalie haki ya siri kwa mtu, pia lazima kulinda heshima na hadhi ya makahama kusiwe na zogo wakati kesi zinaendelea na waandishi wapiga picha wanaendelea na kazi,” alisema.

Aidha, alisema wanaangalia uwezekano wa kuwa na eneo maalum la kukaa waandishi katika kila mahakama, ikiwa ni pamoja na kuweka katika lugha rahisi hukumu inayotolewa ili iwe rahisi kuandika habari.

Alisema lugha ya sheria ni ngumu na wakati mwingine huwalazimu majaji kutumia kamusi, hivyo wataandaa utaratibu wa kuwa na taarifa fupi kwa waandishi mara baada ya hukumu.
“Uhalali wa mahakamani na vyombo vya habari unatokana na haja ya jamii kuwa na utawala bora, demokrasia na uwajibikaji, jukwaa hili limekuja kwa wakati muafaka ili tuwe na mkakati wa pamoja wa kushirikiana kwa kuheshimiana na mahusiano mema kwa pande zote,” alibainisha.

“Kusiwe na ‘kiwingu’ kila mmoja afanye kazi yake kwa mujibu wa taaluma yake kwa kuheshimiana na kushirikiana,” alisema.

Rais wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Jaji Mstaafu, Thomas Mihayo, alisema Mahakama ni kimbilio la wananchi wenye kutafuta haki hivyo waandishi wakipata taarifa kwa muda muafaka wataueleza na kuelimisha umma.

Alisema kwa sasa kuna kutokuaminiana baina ya mahakama na vyombo vya habari, na kwamba baada ya mkutano huo watatoa na maamuzi ya pamoja ya kuwezesha kufanya kazi kwa pamoja kwa chombo ambacho ni muhimili wa tatu wa dola na muhimili usio rasmi.

MCT WAZUNGUMZA
Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga, alisema jukwaa hilo ni endelevu katika kuleta pande zote pamoja ili kuweza kufanya kazi pamoja.

Alisema MCT imeona umuhimu wa kukuza uelewa wa waandishi wa habari kuandika habari za Mahakama kwa kuwapa mafunzo na kutoa kitabu cha muongozo wa jinsi ya kuandika habari za Mahakama, kwa kuwa wanahabari siyo wanasheria ni rahisi kushindwa kutafsiri baadhi ya maneno ya kisheria.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda, alisema ili kila taasisi itekeleze majukumu yake kwa uhuru ni lazima kutakuwa na misuguano na kwamba ni mizuri alimradi isiwe nje ya misingi ya taaluma husika.

Chanzo:
Nipashe.
 
Sidhani kama Bunge limedharau Mahakama,bali mahakama imejidharaulisha mbele ya jamii kwa watendaji wake wakuu( majaji) kujihusisha na rushwa ya dhahiri hivyo kujiondoa katika uaminifu.
Nakumbuka Lembeni alisema Bungeni kuwa taasisi pekee zinazoaminika kwa wananchi ni Bunge na JWTZ tuu. Lakini kwa matukio yaliyojitokeza ya wabunge nao kutuhumiwa kupokea rushwa kutetea ufisadi basi na Bunge nalo limeingia katika orodha ya wasioaminika.
Kwa usemi wa Lembeni maana yake ni kuwa Taasisi pekee iliyobaki kuaminiwa na kutodharauliwa nchi hii ni JWTZ. Ni kusema kuwa zingine zote yaani Ikulu,Polisi, mawizara, taasisi za dini nk nk haziaminiki tena. Hii sijui inaleta muono gani kwa nchi. Jee tuwape uongozi hao tunaowaamini?
Kwa hiyo kwa maneno mengine, unataka kusema Davis akitoa marching orders kwa vijana wake, kwenda kumtimua yule mpangaji fisadi pale kwenye ile nyumba tuliompangisha, majirani watashangilia?!.

Pasco
 
Nilisema tuna tatizo kubwa katika kitu kinachoitwa "The doctrine of separation of powers and checks and balance" ambayo lento leke ni kila mhimili umepewa powers zake lakini utekelezaji wa powers hizo unakuwa monitored na muhimili mwingine, na ikitokea mhimili mmoja kujiinua kupitiliza mhimili mwingine umepewa powers za kuuzuia.

Bunge kazi yake ni kutunga sheria, mamlaka ya bunge kutunga sheria, hayapaswi kuingiliwa, ila ili sheria inayotungwa na bunge kuwa sheria, lazima ipitishwe na mkuu wa executive, akikataa, sio sheria!. Mahakama kazi yake ni kutafsiri sheria baada ya kutungwa na bunge na kuridhiwa na executive, uhuru wa mahakama katika kutafsiri sheria pia haupaswi kuingiliwa na bunge au na serikali, tumeshuhudia mara kibao, mahakama ikitunga sheria kupitia kitu kinachoitwa "precedence" na mara kibao mahakama inatamka sheria fulani ni "bad law" and should be scraped off from the books of law immediately!.

Mahakama imepewa uwezo wa kutoa amri kwa serikali, (executive order" zinazoitwa "writs" hizi ni "prohibition", "certiorari" na "mandamus" ambapo serikali inazuiliwa au isifanye jambo fulani, au kulazimishwa kufanya jambo fulani, au kutengua uamuzi fulani wa kiserikali, na hazinaga mjadala!.

Kitendo cha bunge kutafsiri vibaya ibara ya 100, hivyo kuidharau mahakama wazi wazi, hakiwezi kukubalika mahali pengine popote duniani!, mahakama halikuizui bunge kufanya kazi yake, limeliamuru lisubiri kwanza hadi baada ya December 8!, naamini baada ya uamuzi ule, spika alikuja kuwa mdogo, na sasa serikali ili kuonyesha heshima kwa mahakama, imeamua kuyakalia kimya tuu mapendekezo ya bunge!.

Kwa waliosoma hoja zangu, za Mwanakijiji, na FF, kila mmoja ametoa hoja zake tofauti na mwingine!.

Mimi nilijibainisha wazi, kuwa wanaoshangilia bunge kuidharau mahakama, wanashangilia ujinga!.

Mzee Mwanakijiji, alitoa hoja ya msingi sana, kwamba kama Bunge litaidharau mahakama, nani ataiheshimu?.

Pasco.

Utumbo huu,mahakama ni mahakama na bunge ni bunge vitu viwili fotauti,na kama mahakama inaona ina nguvu juu ya bunge ifanye inavyoweza ili kuliwajibisha bunge
 
This is silly; kama kweli mahakama "inapenda mtu apate haki" sasa mtu ambaye anaona Bunge linamkandamiza akimbilie wapi kupata haki? kwa Spika?
Haaa Mwanakijiji inajulikana kabisa mto haki ni Mahakama HUO ukandamizaji unao uzungumzia ni upi NI MJADALA unao ibuka na maazimio ambayo mtekelezaji ni Serikali ambayo ina vyombo vyake vya uchunguzi...umechange!!
 
Nilisema tuna tatizo kubwa katika kitu kinachoitwa "The doctrine of separation of powers and checks and balance"
Pasco the doctrine of separation of powers and checks and balance ndiyo nini?

Niliona umeandika hivyo kwenye uzi mwingine.

Nadhani hizo ni concepts mbili tofauti japokuwa zina-address the same thing.
 
Last edited by a moderator:
Pasco the doctrine of separation of powers and checks and balance ndiyo nini?

Niliona umeandika hivyo kwenye uzi mwingine.

Nadhani hizo ni concepts mbili tofauti japokuwa zina-address the same thing.

Hahahahaaa umeniwahi maani nami nilitaka kumwuliza hivyo hivyo.

Halafu tena kawekea na alama za kunukuu kabisa.

Kaka msomi huyo!
 
Nilisema tuna tatizo kubwa katika kitu kinachoitwa "The doctrine of separation of powers and checks and balance" ambayo lento leke ni kila mhimili umepewa powers zake lakini utekelezaji wa powers hizo unakuwa monitored na muhimili mwingine, na ikitokea mhimili mmoja kujiinua kupitiliza mhimili mwingine umepewa powers za kuuzuia.

Bunge kazi yake ni kutunga sheria, mamlaka ya bunge kutunga sheria, hayapaswi kuingiliwa, ila ili sheria inayotungwa na bunge kuwa sheria, lazima ipitishwe na mkuu wa executive, akikataa, sio sheria!. Mahakama kazi yake ni kutafsiri sheria baada ya kutungwa na bunge na kuridhiwa na executive, uhuru wa mahakama katika kutafsiri sheria pia haupaswi kuingiliwa na bunge au na serikali, tumeshuhudia mara kibao, mahakama ikitunga sheria kupitia kitu kinachoitwa "precedence" na mara kibao mahakama inatamka sheria fulani ni "bad law" and should be scraped off from the books of law immediately!.

Mahakama imepewa uwezo wa kutoa amri kwa serikali, (executive order" zinazoitwa "writs" hizi ni "prohibition", "certiorari" na "mandamus" ambapo serikali inazuiliwa au isifanye jambo fulani, au kulazimishwa kufanya jambo fulani, au kutengua uamuzi fulani wa kiserikali, na hazinaga mjadala!.

Kitendo cha bunge kutafsiri vibaya ibara ya 100, hivyo kuidharau mahakama wazi wazi, hakiwezi kukubalika mahali pengine popote duniani!, mahakama halikuizui bunge kufanya kazi yake, limeliamuru lisubiri kwanza hadi baada ya December 8!, naamini baada ya uamuzi ule, spika alikuja kuwa mdogo, na sasa serikali ili kuonyesha heshima kwa mahakama, imeamua kuyakalia kimya tuu mapendekezo ya bunge!.

Kwa waliosoma hoja zangu, za Mwanakijiji, na FF, kila mmoja ametoa hoja zake tofauti na mwingine!.

Mimi nilijibainisha wazi, kuwa wanaoshangilia bunge kuidharau mahakama, wanashangilia ujinga!.

Mzee Mwanakijiji, alitoa hoja ya msingi sana, kwamba kama Bunge litaidharau mahakama, nani ataiheshimu?.

Pasco.

Bunge linatimiza wajibu wake kama Msimamizi na Mtunga Sheria na ndio maana imeandikwa kwenye katiba MJDALA WOWOTE NDANI YA BUNGE HAUWEZI KUHOJIWA NA MTU YOYOTE YULE AU MUHIMILI WOWOTE MBONA IKO WAZI...HIVYO MJADALA WA ESCROW HAUNA WA KUHOJI ILA BUSARA ZINAONGOZA NA KUTOA MWONGOZO KAMA ILIPO WAHUSU MAJAJI BASI BUSARA NI kuwaagiza MUHIMILI WA MAHAKAMA KUUNDA TUME NA KUONA WANATENDEWA HAKI KUPITIA TUME ITAKAYOUNDWA NA MUHIMILI HUO WA UTOAJI WA HAKI.

Sasa hii habari yenu ya kutwambia kuwa Mahakama ina leta Barua ya ZUIO kuwa BUNGE isiendeshe Vikao vyake kujadili hoja za Wananchi eti kunapingamiza Mahakamani.

Ni nani asiye jua kuwa BUNGE ni wawakilishi wa Wananchi Milioni 45 ambao kutokana na kutokuwa na uwezo wa kukusanyika kwa UMOJA wao kukaa kikao cha kuamua MAMBO YAO KWA UJUMLA WAO basi kunakuwapeo na uwakilishi kwa kutumia wawakilishi wao kwa jina la WABUNGE.

IVI LETS BE FRANK Pasco na Mwanakijiji imagine tuchukue ujima enzi hizo vitu FRANCE Revolution [UMMA-BUNGE] ungeweza kuzuia Wasiongee kwa agizo la Mahakama....This is to say Misri na kwingineko kuliko fanyika mapinduzi kwa nguvu ya Umma.Sasa tendo la sie kuwa na wawakilishi ni sura hiyo hiyo ya kusanyiko la umma katika njia ya DEMOKRASIA ya kiungwana ya uwakilishi ambayo asili yake UMOJA katika KUWAKILISHWA.

To me naamini BUNGE lapaswa kuwa ni zaidi ya SERIKALI na MAHAKAMA.Kwa kuwa BUNGE ndio jumuhiko la Umma.Sasa hii habari ya mtoto kutaka kumzaa Mama Siwaelewi eti....
 
Upo sahihi mkuu kwa kuzingatia kwamba Wananchi ndio wenye dhamana ya mwisho katika taifa lolote, wao ndio mabosi wa mihimili yote ya nchi, nikimaanisha BUNGE, SERIKALI na MAHAKAMA, hivyo kama kuna jambo linalowahusu moja kwa moja wanayo haki ya kujulishwa na sidhani kama kuna mhimili wenye mamlaka zaidi ya KATIBA ambayo ndio muongozo wa taifa kama ulivyohakikiwa na kukubaliwa na mabosi "wenye nchi". Sioni kama ni sahihi kwa mahakama kujiona kama ina mamlaka zaidi na kusahau haki ya wananchi?? kufanya hivyo ni kuwa na ubinafsi wa kimamlaka, kwa heshima mahakama ijivue taswira hiyo inayotaka kujivika, na Bunge kama chombo pekee cha uwakilishi wa wananchi moja kwa moja, lisiache kupiga kelele palel haki za msingi za wananchi zinapofinywa.
 
Back
Top Bottom