Jaji Mkuu "awatosa" watuhumiwa wa Escrow

Jaji Mkuu "awatosa" watuhumiwa wa Escrow

EMT

Platinum Member
Joined
Jan 13, 2010
Posts
14,477
Reaction score
15,356
Jaji Mkuu, Mohamed Chande Othman, amevunja ukimya kuhusiana na sakata la uchotwaji wa zaidi ya Sh. bilioni 300 kutoka akaunti ta Tegeta Escrow iliyopo Benki Kuu ya Tanzania (BoT), akisema kuwa watuhumiwa wanamtumia ujumbe kulalamika wamehukumiwa bila kusikilizwa.

Jaji Chande alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam katika mkutano wa pamoja kati ya viongozi waandamizi wa mahakama wakiwamo majaji na wasajili na wahariri wa vyombo vya habari kujadili mahusiano na ushirikiano baina ya mahakama na vyombo vya habari.

Alitoa kauli hiyo kuhusiana na mjadala wa sakata hilo uliofanyika bungeni wiki iliyopita baada ya Mahakama Kuu kuzuia lisijadiliwe bungeni hadi kesi zinazohusu kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) zitakapoamuliwa na Mahakama Desemba 8, mwaka huu.

"Napata meseji nyingi kutoka kwa baadhi ya watu kuwa ule mjadala bungeni umeshawahukumu na kuwa hawana sababu za kwenda mahakamani kujitetea," alisema Jaji Chande wakati wa kufunga mkutano huo.

Akizungumzia majadala huo alisema Mahakama iko nje ya Bunge na kwamba uhuru wa wabunge kuzungumza ndani ya Bunge unalindwa na Katiba ya nchi.

"Uhuru wa Mahakama hauko ndani ya Bunge, kama tutaongea tutakuwa tunaongea na nani. Tukiongea nje tutakuwa tunaongea na vyombo, huwezi kusahihisha hansad (rekodi za Bunge)," alisema Jaji Chande.

Aliongeza kuwa Mahakama haitakiwi kujihusisha na malumbano ya kisiasa kwa sababu huo ni mhimili mwingine na kwamba Katiba ya sasa na inayopendekezwa mahakama na watendaji wake hawatakiwi kujihusisha na siasa.

"Kwa Tanzania Katiba inayopendekezwa mahakimu, majaji wanatakiwa wasiwe wanasiasa na mahakama yenyewe isiingilie wanasiasa. Hilo ni zuio kubwa," alisema.

Kuhusu ukimya wa mahakama wa shutuma zinazotolewa dhidi majaji, alisema ukimya haumaanishi kuwa inajilinda au jaji anajilinda, bali analinda lile lililomuweka ofisini.

Alisema mahakama inapenda mtu apate haki na haina upande wowote wa siasa.

Katika sakata la akaunti ya Escrow, miongoni mwa maazimio ya Bunge ni kuundwa kwa tume ya kimahakama ya kuwachunguza majaji wawili wanaodaiwa kuchotewa pesa na Mkurugenzi wa VIP Engeering & Marketing Limited, James Rugemalira.

Majaji hao ni Profesa John Luhangisa, anayedaiwa kupokea Sh. milioni 400 na Jaji Aloyce Mujulizi, anayedaiwa kupewa Sh. milioni 40.

Akizungumzia kesi mbalimbali zinazoripotiwa mahakamani, alisema kazi ya vyombo vya habari ni kuhakikisha kuwa habari hizo zinakuwa sahihi bila kupotoshwa ili mwananchi aweze kujenga imani na vyombo hivyo.

Alitoa mfano wa nchi ya India ambako alisema mwandishi hawezi kuandika habari za mahakama kama hana uelewa wa mambo ya mahakama.

Alisema pamoja na kwamba watu wanashutumu mahakama kupendelea upande fulani, lakini ikiangaliwa kesi za uchaguzi mahakama zinatoa haki bila kujali upande wowote wa siasa.

Jaji Othuman, pia alisema wanaangalia uwezekano wa waandishi wapiga picha kuruhusiwa kufanya kazi wakati kesi za madai zinaendelea katika kutoa habari za kina kwa umma.

Alisema wataweka taratibu na kanuni za kuwezesha utekelezaji katika kesi za madai zenye mvuto kwa jamii, na kuhusu kesi za jinai alisema itakuwa ngumu kwa kuwa zina mashahidi na wapo wenye kuhitaji usiri.

"Hoja kuu ni kupima uhuru wa taarifa na kupata taarifa moja kwa moja wakati kesi inaendelea, tuangalie haki ya siri kwa mtu, pia lazima kulinda heshima na hadhi ya makahama kusiwe na zogo wakati kesi zinaendelea na waandishi wapiga picha wanaendelea na kazi," alisema.

Aidha, alisema wanaangalia uwezekano wa kuwa na eneo maalum la kukaa waandishi katika kila mahakama, ikiwa ni pamoja na kuweka katika lugha rahisi hukumu inayotolewa ili iwe rahisi kuandika habari.

Alisema lugha ya sheria ni ngumu na wakati mwingine huwalazimu majaji kutumia kamusi, hivyo wataandaa utaratibu wa kuwa na taarifa fupi kwa waandishi mara baada ya hukumu.
"Uhalali wa mahakamani na vyombo vya habari unatokana na haja ya jamii kuwa na utawala bora, demokrasia na uwajibikaji, jukwaa hili limekuja kwa wakati muafaka ili tuwe na mkakati wa pamoja wa kushirikiana kwa kuheshimiana na mahusiano mema kwa pande zote," alibainisha.

"Kusiwe na ‘kiwingu' kila mmoja afanye kazi yake kwa mujibu wa taaluma yake kwa kuheshimiana na kushirikiana," alisema.

Rais wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Jaji Mstaafu, Thomas Mihayo, alisema Mahakama ni kimbilio la wananchi wenye kutafuta haki hivyo waandishi wakipata taarifa kwa muda muafaka wataueleza na kuelimisha umma.

Alisema kwa sasa kuna kutokuaminiana baina ya mahakama na vyombo vya habari, na kwamba baada ya mkutano huo watatoa na maamuzi ya pamoja ya kuwezesha kufanya kazi kwa pamoja kwa chombo ambacho ni muhimili wa tatu wa dola na muhimili usio rasmi.

MCT WAZUNGUMZA
Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga, alisema jukwaa hilo ni endelevu katika kuleta pande zote pamoja ili kuweza kufanya kazi pamoja.

Alisema MCT imeona umuhimu wa kukuza uelewa wa waandishi wa habari kuandika habari za Mahakama kwa kuwapa mafunzo na kutoa kitabu cha muongozo wa jinsi ya kuandika habari za Mahakama, kwa kuwa wanahabari siyo wanasheria ni rahisi kushindwa kutafsiri baadhi ya maneno ya kisheria.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda, alisema ili kila taasisi itekeleze majukumu yake kwa uhuru ni lazima kutakuwa na misuguano na kwamba ni mizuri alimradi isiwe nje ya misingi ya taaluma husika.

Chanzo:
Nipashe.
 
Mkuu EMT hili ni Nipashe la leo ijumaa?

Hapa Makinda na Pinda wameumbuliwa sambamba na wanafki wengine.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu EMT hili ni Nipashe la leo ijumaa?

Hapa Makinda na Pinda wameumbuliwa sambamba na wanafki wengine.
Mimi Makinda kanieleza atakuwa mgeni wa Nani baada ya kuingilia muhimili moja nao ni mahakama , kumbe alikuwa ananidanganya , halafu hili la waandishi wa habari kwa kweli ina bidi tuli upgrade sio reporter naye anajiita mwandishi wa habari n.k
 
Last edited by a moderator:
..
Kuhusu ukimya wa mahakama wa shutuma zinazotolewa dhidi majaji, alisema ukimya haumaanishi kuwa inajilinda au jaji anajilinda, bali analinda lile lililomuweka ofisini. Alisema mahakama inapenda mtu apate haki na haina upande wowote wa siasa.

This is silly; kama kweli mahakama "inapenda mtu apate haki" sasa mtu ambaye anaona Bunge linamkandamiza akimbilie wapi kupata haki? kwa Spika?
 
This is silly; kama kweli mahakama "inapenda mtu apate haki" sasa mtu ambaye anaona Bunge linamkandamiza akimbilie wapi kupata haki? kwa Spika?

Hapo ndio nimetambua aina ya Wasimamia sheria wetu tulionao.
 
Hahahaahahaaha sarakasi zinaendelea kama kawaida, sioni sababu ya kujipambanua kwa ujinga wao.
 
Acha waonewe,mbona sisi huku vijijini tunaonewa kila siku?
Ina maana huo u "silly" wa mahakama ndio mnauona leo kuhusu escrow? Hypocracy at its best!
This is silly; kama kweli mahakama "inapenda mtu apate haki" sasa mtu ambaye anaona Bunge linamkandamiza akimbilie wapi kupata haki? kwa Spika?
 
Jaji ana haki ya kusema alio yasema lkn Wananchi tunataka kujua mwisho wa Hili sakata.

Watoto wetu wanaadhirika Mashuleni Halafu Waziri aliyewekwa Kuangalia Haki zao Analipwa BILIONI 1.6?

Hapa hatoki mtu kimya kimya.
 
Siku ikifika, mnyonge atanyonga mtu.
 
This is silly; kama kweli mahakama "inapenda mtu apate haki" sasa mtu ambaye anaona Bunge linamkandamiza akimbilie wapi kupata haki? kwa Spika?

Katiba ya nchi ndo inayoongoza vyombo vyote. Wee unataka wavunje katiba kwa maslahi ya nani? Ili wawatetee mafisadi? HAIKUBALIKIII..... ACHA WASIMAMIE KATIBA LABDA KAMA ITABADILISHWA..
 
Mahakama ili taka kupeleka mambo kihuni ikaona iachemsha na wananchi wata wachoka...sasa wanatafuta namna ya kujirudisha nyuma kinyemela
 
Wasome Mwanakijiji, Pasco na FF walipendekeza Spika akamatwe.
Nilisema tuna tatizo kubwa katika kitu kinachoitwa "The doctrine of separation of powers and checks and balance" ambayo lento leke ni kila mhimili umepewa powers zake lakini utekelezaji wa powers hizo unakuwa monitored na muhimili mwingine, na ikitokea mhimili mmoja kujiinua kupitiliza mhimili mwingine umepewa powers za kuuzuia.

Bunge kazi yake ni kutunga sheria, mamlaka ya bunge kutunga sheria, hayapaswi kuingiliwa, ila ili sheria inayotungwa na bunge kuwa sheria, lazima ipitishwe na mkuu wa executive, akikataa, sio sheria!. Mahakama kazi yake ni kutafsiri sheria baada ya kutungwa na bunge na kuridhiwa na executive, uhuru wa mahakama katika kutafsiri sheria pia haupaswi kuingiliwa na bunge au na serikali, tumeshuhudia mara kibao, mahakama ikitunga sheria kupitia kitu kinachoitwa "precedence" na mara kibao mahakama inatamka sheria fulani ni "bad law" and should be scraped off from the books of law immediately!.

Mahakama imepewa uwezo wa kutoa amri kwa serikali, (executive order" zinazoitwa "writs" hizi ni "prohibition", "certiorari" na "mandamus" ambapo serikali inazuiliwa au isifanye jambo fulani, au kulazimishwa kufanya jambo fulani, au kutengua uamuzi fulani wa kiserikali, na hazinaga mjadala!.

Kitendo cha bunge kutafsiri vibaya ibara ya 100, hivyo kuidharau mahakama wazi wazi, hakiwezi kukubalika mahali pengine popote duniani!, mahakama halikuizui bunge kufanya kazi yake, limeliamuru lisubiri kwanza hadi baada ya December 8!, naamini baada ya uamuzi ule, spika alikuja kuwa mdogo, na sasa serikali ili kuonyesha heshima kwa mahakama, imeamua kuyakalia kimya tuu mapendekezo ya bunge!.

Kwa waliosoma hoja zangu, za Mwanakijiji, na FF, kila mmoja ametoa hoja zake tofauti na mwingine!.

Mimi nilijibainisha wazi, kuwa wanaoshangilia bunge kuidharau mahakama, wanashangilia ujinga!.

Mzee Mwanakijiji, alitoa hoja ya msingi sana, kwamba kama Bunge litaidharau mahakama, nani ataiheshimu?.

Pasco.
 
Mahakama itaheshimika pale tu itakapoacha kugeuzwa kichaka cha wahalifu (Abuse of juri........)

Unakumbuka pale mbezi Beach kuna mtu alivamia uwanja wa mama mmoja kwa jeuri ya pesa akajenga appartment 4 kesi iliyopo mahakamani ikaamuriwa zile nyumba zivunjwe sasa kichekesho eti siku ya kutekeleza hukumu ya mahakama eti ndio anatokea wakili wa yule tapeli na hati ya mahakama kuzuia ubomoaji ni kwamba hakuna mtu aliyepokea yale makaratasi na nyumba zilibomolewa kama kawa and you know this better.
 
Mtu mwingine yoyote anaweza kuidharau mahakama na kusiwe na impact yoyote!, lakini amini nakuambia, baada ya bunge ambalo ni mhimili, kuidharau mahakama ambayo ni mhimili mwingine, kutakuwa na a very huge impact!, subiria.

Pasco
 
Back
Top Bottom