Jaji mkuu aomba kipimo cha (DNA) kitumike kusaidia kurahisisha ushahidi kesi za ubakaji

mbahachu

Member
Jul 26, 2019
19
10
Jaji Mkuu wa Tanzania Prof.Ibrahim Juma amesema ufanyike mkakati wa kuangalia matumizi ya kuchukua sampuli kwa ajili ya kipimo cha vina saba (DNA) ili visaidie kurahisisha upatikanaji wa ushahidi kwa watuhumiwa wanaofanya vitendo vya ubakaji na kulawiti watoto hapa nchini.

Jaji Mkuu wa Tanzania Prof.Ibrahim Juma akiwa katika ziara ya kutembelea mahakama na kukagua miradi mipya ya ujenzi ya majengo ya mahakama mkoani Njombe amesema bado hajaona matumizi ipasavyo ya kipimo cha vina saba (DNA) na kwamba anazani ipo haja matumizi ya kuchukua sampuli ya vinasaba ikatumika kupata ushahidi wa kesi za ubakaji na kulawiti.

Aidha Jaji Mkuu wa Tanzania akizungumzia lengo la ziara katika mkoa wa Njombe amesema kuna jopo la majaji wanne waliofika kufanya kikao cha kesi za rufani akiwemo yeye mwenyewe ili kuzitolea majibu.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendaka amemweleza Jaji Mkuu Prof.Ibrahim Juma alipokuwa katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa huyo kuwa hadi sasa jumla ya washitakiwa wa matukio ya mauaji mkoani hapa wapo zaidi ya 156 na kwamba upo umuhimu wa kuwa na Mahakama Kuu mkoani Njombe.
 
Tuanze kuangalia na sababu za ubakaji kuongezeka pamoja na kuwepo kwa sheria kali
 
Back
Top Bottom