Jaji Mkuu anza na Tanzania Law Report (TLR)

MdogoWenu

JF-Expert Member
Dec 23, 2009
555
915
Wasio wanasheria mjue kwamba Tanzania Law Report (TLR) ni kitabu chenye case zilizoropotiwa ili zitumike kwa reference. Kitabu hiki huwa kina kesi za kila mwaka.

Sasa, imepita karibu miaka 12 Tanzania haijatoa kesi za miaka ya 2006 hadi leo!

Huu ni uzembe wa ajabu. Wadau wanasumbuka jinsi kupata report za kesi na hii inaishia kuleta mabishano mahakamani


Gharama za kesi kutokuwepo kwenye TLR ni kubwa kote kwa mwenye kesi na Mahakama vilevile.

Kwanza kama kesi haipo kwenye TLR huuwezi kuitaja kama reference kwenye kesi yako hadi uandike neno "unreported" hala uiambatanishe.

Huu ni mzigo mkubwa maana kesi kama ya juzi ya THE ATTORNEY GENERAL versus JEREMIA MTOBESYA. ina kurasa 90! Sasa ukiitaja hii basi maana yake ufanye printing ya page 90x3=270.

Kama gharama ya printing ni shs. 500 kwa page basi maana yake kesi moja utagharimikia shs. 135,000/=. Hii ni kama umetaja kesi hiyo tu, bado hujataja zingine.

Vilevile ni rundo la mzigo kwa mahakama. Matkeo yake Registry ya Mahakama zinajaa ma-file bure kwa kitu ambacho kingerahisishwa kwa kutoa TLS kila mwaka.

Hivyo Jaji Mkuu,

Jipe changamoto yako nyingine iwe ya kutengeneza TLR ya miaka yote kuanzia mwaka 2007 hadi leo, ili kuondoa matatizo haya.
 
Hapo kama unampigia mbuzi gitaa. Kazi kubwa aliyonayo ni kuanza kufukuza wafanyakazi ili aonekane kafanya kazi na kusigina haki za wafanyakazi wa chombo hiki cha kutafsiri sheria.
 
Mahakama imeoza! Kwanza hadi majaji na mahakimu wenyewe wananyimana kesi (case law), yaa ni kama wanafunzi wa sekondari vile. Halafu wanaohusika kusambaza kesi zilizoamuliwa hawafanyi kazi kwa moyo mmoja, ukitoa rushwa wanakupa, usipotoa chochote wanakuambia hawana.

Kabla mzigo haujamuangukia jaji mkuu tuwatupie lawama wasajili wa mahakama. Kwanza Ni msajili mkuu wa mahakama (huyu mama anajijua mwenyewe, nafasi hii si yake). Halafu wengine ni manaibu wasajili wote -wa rufaa, main registry, kanda zote na divisheni zote.
 
Back
Top Bottom