Jaji Mkuu aitetea Sheria ya Makosa Mitandao. Adai imetungwa kwa nia njema!

Ni Kweli majaji wote wa Tanzania hawakuwa na furaha na uteuzi wa kujuana wa huyu Bwana! Alitoka alipotoka, walimtegemea nguli wa sheria na majaji waliobobea waongoze na kupewa ujaji mkuu! Anatakiwa apumzike maana mahakama imekuwa kama ime paralyse kwa miaka yote aliokuwepo! Hakubaliki na hana weledi ulee unaokubalika yeye ni kujipendekeza kwa wakubwa kwa maslahi yake! Sheria iko wazi na mapungufu yake anajitoa akili uzeeni kwa kuweka njaa akilini! Aibu
Eti njaa akilini;hivi ww na yeye mwenye njaa nani?Mwenzio hata akistaafu leo uhakika wa kushiba hadi mwisho wa maisha yake anao.

Hoja hapo ingekuwa vinginevyo na sikumtuhumu JM eti ananjaa.Vingenevyo,ni kinyume chake.
 
Ww na yeye mwenye njaa nani?Wakati mwingine kabla hujaandika jambo yakupasa ujifikrishe japo kidogo ndg.Vinginevyo ni sawa na kujitusi ww mwenyewe.
Anaweza akawa na njaa lakini akawa na ujasiri wa kutetea anachokiamini pamoja na njaa yake.

Unadhani Jaji mkuu haoni mapungufu ya sheria hii, anaona sana (unless awe sio mtaalamu wa sheria), lakini kuna kitu kinamsukuma "kujifanya" haoni mapungufu.

It may be Njaa, kuogopa kusema ukweli, kumfurahisha aliyemchagua and the like!
 
Kwani mapungufu ya hii Sheria ni yapi?

Maana isije ikawa ni mapungufu tu kwa kuwa kuna mafundi wa kulalamika.
well, first of all the law criminalizes free expression of opinion. Section 16, for example, imetumika kum arrest mtoto wa Chacha Wangwe ambae ameandika kwenye facebook yake kwamba Zanzibar ni koloni la Tanganyika.

Kosa hapa ni kwamba kachapisha habari ya uongo, japo hayo ni mawazo yake yeye, kama ambavyo mwalimu wa siasa darasa la saba alikuwa anatufundisha kwamba Tanzania na nchi masikini duniani zinapigana na ukoloni mamboleo wa matajiri wa Magharibi kama Marekani. Na walimu mashuleni washtakiwe kwa kushindwa ku prove kwamba Tanzania ni koloni la Marekani?

Second example, ofisi za CHADEMA zilikuwa raided na polis wakati wa uchaguzi na computer kuporwa kwa kosa la kuwa na false information ndani ya computer zao japo zilikuwa hazijachapishwa popote. Ni kosa hata kuwa na taarifa hizo kwenye computer!

Mfano mwingine of the worst kind, section 33 mpaka 39, zinamruhusu Waziri wa Habari kuwalazimisha internet service provider kuwapa taarifa za mteja anaetumia internet, which is the most abhorrent invasion of privacy by government.
 
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Ofisi ya Waziri Mkuu ilieleza kuwa, Jaji Mkuu alisema katika mkutano huo kuwa sheria hiyo ilitungwa kwa misingi mikuu mitatu, aliyoitaja kuwa ni kumpa mtumiaji uhuru wa kutoa maoni au taarifa, mtu kuwa na faragha na kulinda usalama wa taifa.
.
RE: WANAOIKOSOA SHERIA YA MTANDAO BADO HAWAJAPAMBANUA HOJA YAO IPASAVYO

Mimi naona kwamba, maoni ya Jaji Mkuu yanao umantiki ambao baadhi ya wachangiaji hapa wanaupiga kisogo kwa makusudi kutokana na sababu ambazo hawajaziweka wazi. Nijuavyo mimi, huu ni mjadala ambao unapaswa kuongozwa na kanuni za jurisprudence. Kwa hiyo wanazuoni, na hasa wanasheria, wangeweza kutoa michango yao hapa wakawa na msaada mkubwa--lakini kama wakitaka kusema ukweli. Mimi sio mwanahsriea. Lakini ni bush Philosopher niliyebahatika kuyafahamu mambo haya kwa kina.

Kwa kutumia uzoefu huo, hebu niwakumbushe wanajukwaa kanuni muhimu za "jurisprudence of human rights" kulingana na mwanasheria mmoja maarufu duniani anavyozitaja. Huyo ni Profesa John Finnis wa Uingereza anayeandika hivi:

"The fundamental postulates of Hohfeld’s system [of human rights] are:

(i) that all assertions or ascriptions of rights can be reduced without remainder to ascriptions of one or some combination of the following four ‘Hohfeldian rights’: (a) ‘claim-rights’, (b) ‘liberty rights’, (c) ‘power rights’, and (d) ‘immunity rights’; and

(ii) that to assert a Hohfeldian right is to assert a three-term relation between one person, one act-description, and one other person.

"(Concerning claim-rights and liberty-rights,) if A and B signify persons and F stands for an act description signifying some act, then, the following logical relations among A, B, and f will obtain:

(1) A has a claim-right that B should f, if and only if B has a duty to A to F.

(2) B has a liberty (relative to A) to F, if and only if A has no-claim-right (‘a no-right) that B should not F.

(2’) B has a liberty (relative to A) not to F, if an only if A has no-claim-right (‘a no right’) that B should F.

"From the above, one can easily see, in light of these three-term relations that, the most important of the aids to clear thinking provided by Hohfeld’s schema is the distinction between A’s claim-right (which has as its correlative B’s duty) and A’s liberty , which is A’s freedom from duty and thus has as its correlative the absence or negation of the claim-right that B would otherwise have.

"A claim-right is always either, positively a right to be given something (or assisted in a certain way) by someone else, or, negatively, a right not to be interfered with or dealt with or treated in a certain way, by someone else. When the subject-matter of one’s claim of right is one’s own act(s), forbearance(s), or omission(s), that claim cannot be to a claim-right, but can only be to a liberty

(Source: John Finnis, Natural Law and Natural Rights. New York/Oxford: Clarendon Press, 1980, p. 199-200.)."

Kwa kuzingatia mwongozo huu wa kisomi kabisa, mimi naona kwamba, haki zinazohusiana na uhuru wa habari zitajadilika vizuri zaidi ikiwa tunao ufahamu mmoja juu ya kategoria gani za haki zinajadiliwa katika hoja iliyo mbele yetu. Kwa mfano, kwa kuzingatia mwongozo wa profesa John Finnis hapo juu maelezo yafuatayo ni kweli:

(a) Haki ya raia A kupokea habari kutoka kwa raia B kupitia mitandao ya kijamii ni POSITIVE CLAIM RIGHT--Hii tuiite haki W
(b) Haki ya raia A kuwa huru dhidi ya habari za uwongo au habari zenye maudhi kutoka kwa raia B kupitia mitandao ya kijamii ni NEGATIVE CLAIM RIGHT--Hii tuiite haki X
(c) Haki ya raia A kusambaza habari kwenda kwa raia B kupitia mitandao ya kijamii ni POSITIVE LIBERTY RIGHT--Hii tuiite haki Y
(d) Haki ya raia A kujizuia kusambaza habari kwenda kwa raia B kupitia mitandao ya kijamii ni NEGATIVE LIBERTY RIGHT--Hii tuiite haki Z

Kwa kuzingatia mchanganuo huo hapo juu, ni wazi kwamba, utekelezaji wa "HAKI Y" unayo mipaka inayotokana na uwepo wa "HAKI X."

Kwa lugha ya walei wa mitaani tunasema kuwa uhuru wa kunyoosha mikono yako hewani na kujizungusha unaishia pale pua ya jirani yako inapoanzia.

Hii ndiyo sababu haki ya mvuta sigara inaminywa na jukumu lake la kuheshimu haki za majirani zake (kwa mfano wagonjwa waliolazwa wodini). Vivyo hivyo, haki ya mwimbaji inaminywa na jukumu lake la kuheshimu haki za majirani zake (kwa mfani wanafunzi walio darasani wanajisomea).

Ni katika mazingira haya, Jaji Mkuu anasema kwamba: "sheria hiyo ilitungwa kwa misingi mikuu mitatu... kumpa mtumiaji uhuru wa kutoa maoni au taarifa, mtu kuwa na faragha na kulinda usalama wa taifa."

Na ni kwa sababu ya umantiki huu wanazuoni wengi tulilikosoa tamko la Bodi ya MCC lililodai kwamba hawa waheshimiwa walitaka serikali ya Tanzania iwape uthibitisho kwamba sheria ya mtandao haitatumika kuweka "limits" katika uhuru wa habari za mtandaoni. Hatukuamini kwamba hata huko Marekani kuna viongozi wa kitaifa ambao ni MAIMUNA wa sheria za kimataifa kuhusu mipaka ya haki za binadamu kwa kiwango hiki. (Waziri wa Mambo ya Nje ya Marekani ni mjumbe wa Bodii hii).

Hivyo basi, baada ya utangulizi huu ulioweka mfumo wa dhana zinazopaswa kuongoza mjadala huu (conceptual framework) sasa nawakaribisha wachangiaji wenye hoja nzuri zaidi kuboresha uzi huu.....
 
.
RE: WANAOIKOSOA SHERIA YA MTANDAO BADO HAWAJAPAMBANUA HOJA YAO IPASAVYO

Mimi naona kwamba, maoni ya Jaji Mkuu yanayo umantiki ambao baadhi ya wachangiaji hapa--wakiwemo maPhD holders ninaofahamu ID zao--wanaupiga kisogo kwa makusudi kutokana na sababu ambazo hawajaziweka wazi. Nijuavyo mimi, huu ni mjadala ambao unapaswa kuongozwa na kanuni za jurisprudence. Kwa hiyo wanazuoni, na hasa wanasheria, wangeweza kutoa michango yao hapa wakawa na msaada mkubwa--lakini kama wakitaka kusema ukweli. Mimi sio mwanahsriea. Lakini ni bush Philosopher niliyebahatika kuyafahamu mambo haya kwa kina.

Kwa kutumia uzoefu huo, hebu niwakumbushe wanajukwaa kanuni muhimu za "jurisprudence of human rights" kulingana na mwanasheria mmoja maarufu duniani anavyozitaja. Huyo ni Profesa John Finnis wa Uingereza anayeandika hivi:

"The fundamental postulates of Hohfeld’s system [of human rights] are:

(i) that all assertions or ascriptions of rights can be reduced without remainder to ascriptions of one or some combination of the following four ‘Hohfeldian rights’: (a) ‘claim-rights’, (b) ‘liberty rights’, (c) ‘power rights’, and (d) ‘immunity rights’; and

(ii) that to assert a Hohfeldian right is to assert a three-term relation between one person, one act-description, and one other person.

"(Concerning claim-rights and liberty-rights,) if A and B signify persons and F stands for an act description signifying some act, then, the following logical relations among A, B, and f will obtain:

(1) A has a claim-right that B should f, if and only if B has a duty to A to F.

(2) B has a liberty (relative to A) to F, if and only if A has no-claim-right (‘a no-right) that B should not F.

(2’) B has a liberty (relative to A) not to F, if an only if A has no-claim-right (‘a no right’) that B should F.

"From the above, one can easily see, in light of these three-term relations that, the most important of the aids to clear thinking provided by Hohfeld’s schema is the distinction between A’s claim-right (which has as its correlative B’s duty) and A’s liberty , which is A’s freedom from duty and thus has as its correlative the absence or negation of the claim-right that B would otherwise have.

"A claim-right is always either, positively a right to be given something (or assisted in a certain way) by someone else, or, negatively, a right not to be interfered with or dealt with or treated in a certain way, by someone else. When the subject-matter of one’s claim of right is one’s own act(s), forbearance(s), or omission(s), that claim cannot be to a claim-right, but can only be to a liberty

(Source: John Finnis, Natural Law and Natural Rights. New York/Oxford: Clarendon Press, 1980, p. 199-200.)."

Kwa kuzingatia mwongozo huu wa kisomi kabisa, mimi naona kwamba, haki zinazohusiana na uhuru wa habari zitajadilika vizuri zaidi ikiwa tunao ufahamu mmoja juu ya kategoria gani za haki zinajadiliwa katika hija iliyo mbele yetu. Kwa mfano, kwa kuzingatia mwongozo wa profesa John Finnis hapo juu maelezo yafuatayo ni kweli:

(a) Haki ya raia A kupokea habari kutoka kwa raia B kupitia mitandao ya kijamii ni POSITIVE CLAIM RIGHT--Hii tuiite haki W
(b) Haki ya raia A kuwa huru dhidi ya habari za uwongo au habari zenye maudhi kutoka kwa raia B kupitia mitandao ya kijamii ni NEGATIVE CLAIM RIGHT--Hii tuiite haki X
(c) Haki ya raia A kusambaza habari kwenda kwa raia B kupitia mitandao ya kijamii ni POSITIVE LIBERTY RIGHT--Hii tuiite haki Y
(d) Haki ya raia A kujizuia kusambaza habari kwenda kwa raia B kupitia mitandao ya kijamii ni POSITIVE LIBERTY RIGHT--Hii tuiite haki Z

Kwa kuzingatia mchanganuo huo hapo juu, ni wazi kwamba, utekelezaji wa "HAKI Y" unayo mipaka inayotokana na uwepo wa "HAKI X."

Kwa lugha ya walei wa mitaani tunasema kuwa uhuru wa kunyoosha mikono yako hewani na kujizungusha unaishia pale pua ya jirani yako inapoanzia.

Hii ndiyo sababu haki ya mvuta sigara inaminywa na jukumu lake la kuheshimu haki za majirani zake (kwa mfano wagonjwa waliolazwa wodini). Vivyo hivyo, haki ya mwimbaji inaminywa na jukumu lake la kuheshimu haki za majirani zake (kwa mfani wanafunzi walio darasani wanajisomea).

Ni katika mazingira haya, Jaji Mkuu anasema kwamba: "sheria hiyo ilitungwa kwa misingi mikuu mitatu, aliyoitaja kuwa ni kumpa mtumiaji uhuru wa kutoa maoni au taarifa, mtu kuwa na faragha na kulinda usalama wa taifa."

Na ni kwa sababu ya umantiki huu wanazuoni wengi tulilikosoa tamko la Bodi ya MCC lililodai kwamba hawa waheshimiwa walitaka serikali ya Tanzania iwape assuarance kwamba sheria ya mtandao haitatumika kuweka "limits" katika uhuru wa habari za mtandaoni. Hatukuamini kwamba hata huko Marekani kuna viongozi wa kitaifa ambao ni MAIMUNA wa sheria za kimataifa kuhusu mipaka ya haki za binadamu kwa kiwango hiki. (Waziri wa Mambo ya Nje ya Marekani ni mjumbe wa Bodii hii).

Hivyo basi, baada ya utangulizi huu ulioweka mfumo wa dhana zinazopaswa kuongoza mjadala huu (conceptual framework) sasa nawakaribisha wachangiaji wenye hoja zisizo na ulemavu kuboresha uzi huu. Kama huna competence katika jambo hili sio vibaya ukabaki mtazamaji (spectator).

Umeandika, vizuri tu. Kumbe nawewe huelewi hoja yetu. Kuna specific provision/sections ambazo hazifai.

Do your homework, ipitie sheria yote utavigundua kama kweli wewe ni "bush Philosopher uliyebahatika kuyafahamu mambo haya kwa kina".Sina haja ya ku-site hizo provisions/sections.

Unaelekea uko knowledgeable and not informed! Good.
BY THE WAY JIEPUSHE NA LUGHA YA KEJELI NA KUONYESHA KUWA UNAJUA SANA, MANENO KAMA HOJA ZA ULEMAVU, KUBAKI MTAZAMAJI ETC SIYO STAHA
 
Yeye atastaafu lini?

Wenzake wote wa umri wake walistaafu miaka mingi, yeye atastaafu lini? Labda anajipendekeza aongezewe muda.

Njaa mbaya sana.
Hivi wewe na jaji mkuu wa tanzania nani ana njaa...?
 
Umeandika, vizuri tu. Kumbe nawewe huelewi hoja yetu. Kuna specific provision/sections ambazo hazifai. Do your homework, ipitie sheria yote utavigundua kama kweli wewe ni "bush Philosopher uliyebahatika kuyafahamu mambo haya kwa kina".Sina haja ya ku-site hizo provisions/sections. Unaelekea uko knowledgeable and not informed! Good.
BY THE WAY JIEPUSHE NA LUGHA YA KEJELI NA KUONYESHA KUWA UNAJUA SANA, MANENO KAMA HOJA ZA ULEMAVU, KUBAKI MTAZAMAJI ETC SIYO STAHA
.
Nimekuelewa na nitazingatia ushauri.
 
Mtoto wa chacha anajua whts ina face hilo kosa lililoandikwa no dogo na ame confirce sasa wewe unamtetea hujui the inner part.tusishabikie tusiyoyajua
 
Watu jaman tuwe na uhakika kifungu cha 16 cha cyber kinazingumzua kuchapisha taarifa za uongo kwa makusudi na kwa nia ya kuudhi..kudhuru..nk sasa wapi inanyima freedom of expression. ..kabla ya kupitishwa na bunge serikali na wabunge walikifanyia marekebisho kifungu hichi kwani kilikuwa kina miss the word with intent...sasa rudi tena soma sheria ilopitishwa na sio bill
 
“Hapa Uingereza nimezungumza na Mwendesha Mashtaka Mkuu ambaye aliniambia kuwa asilimia 60 ya makosa yanafanyika chini ya sheria ya makosa ya kujamiiana yanatokana na mitandao,”

Dah¡¡¡¡¡
 
Amenisikitisha sana, sijajua UK alienda kufanya nini, nimemuona wakati PM akiongoea na wtz walioko kwa bibi mkubwa nae kakaa pembeni nilistaajabu sana.

Lakini angalizo asijeangusha muhimili wa mahakama, chonde chonde. Mh Chande, hata kabla Mungu hajaumba dunia, na baada ya kuumba dunia ilikuwa wa kwanza kuzaliwa ndio anakuwa wa kwanza kufa, lakini zambi zilivyozidi ndio ikawa hata mtoto wa siku moja anakufa, ili usitumie kama karata kwako, amini nyuma yako kuna vizazi vingi vinategemea maamuzi yako ya leo.
 
hivi huchaguliwa na nani?
anaemchagua ni wa chama gani?
ye anasimamia sera za chama gani?

tusipate shida,haiwez kutetea wananchi na kuangusha sera zqa chama,.never happen
sheria zimewekwa na ccm.,so waache waseme waonavyo.ni mawazo yao
 
Back
Top Bottom