Jaji Mkuu aitetea Sheria ya Makosa Mitandao. Adai imetungwa kwa nia njema!

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
JAJI Mkuu wa Tanzania, Mohammed Chande Othman, amesema Sheria ya Mitandao ilitungwa na kupitishwa kwa lengo jema la kumlinda mtumiaji, jamii na usalama wa taifa la Tanzania.

Alitoa kauli hiyo juzi wakati akijibu baadhi ya maswali ya Watanzania waishio Uingereza, kwenye mkutano uliofanyika katika Ubalozi wa Tanzania jijini hapa.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Ofisi ya Waziri Mkuu ilieleza kuwa, Jaji Mkuu alisema katika mkutano huo kuwa sheria hiyo ilitungwa kwa misingi mikuu mitatu, aliyoitaja kuwa ni kumpa mtumiaji uhuru wa kutoa maoni au taarifa, mtu kuwa na faragha na kulinda usalama wa taifa.

Hata hivyo, Jaji Mkuu alisisitiza kuwa uhuru huo unalindwa kikatiba, lakini ni lazima uwe na mipaka kama ilivyoainishwa kwenye ibara ya 30(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Sheria hii inakupa uhuru wa kutumia mtandao kumlinda mwanajamii wenzako”. “Hapa Uingereza nimezungumza na Mwendesha Mashtaka Mkuu ambaye aliniambia kuwa asilimia 60 ya makosa yanafanyika chini ya sheria ya makosa ya kujamiiana yanatokana na mitandao,” alisema Jaji Mkuu wakati akijibu swali kuhusu sheria ya makosa ya mitandao alipoulizwa katika mkutano huo wa Watanzania.

Akifafanua zaidi, Jaji Mkuu alisema, watu watatu kati ya wanne nchini Tanzania wakiwemo watoto, wanamiliki simu za mkononi ambayo ni sawa na watu milioni 35 kati ya milioni 45.

Alisema, hali hiyo inapaswa kuwa na uhuru na udhibiti wa matumizi, hivyo kusisitiza kuwa, sheria hiyo imetungwa kwa nia njema.

Sheria ya Makosa ya Mitandao ya mwaka 2015 imekuwa ikielezwa kuwa na manufaa makubwa ya kudhibiti makosa ya mitandaoni hasa kutokana na matumizi ya mitandao ya kijamii nchini, kumlinda mtumiaji na kuhakikisha usalama wa nchi.

Sheria hiyo imekuwa ikitoa adhabu kwa mtumaji wa taarifa, picha au ujumbe hatarishi pamoja na mtu anayeupokea na kuusambaza.
 
Mheshimiwa Jaji Mkuu, wadau wote wa sheria wa ndani na nje ya nchi wamebaini mapungufu makubwa ya kisheria kuhusu sheria tajwa hapo juu.

Nilitegemea wewe kama Mkuu wa chombo cha kutenda haki uungane nao kuona MAPUNGUFU na sio kusema kuwa ina nia nzuri bila kugusia mapungufu makubwa yaliyomo katika sheria hiyo.

Ni masikitiko kuwa kama wewe unaweza kutozisemea kasoro hizo, nani tena wa kizisemea. Sitegemei umfurahishe Mkuu wa nchi kwa kutosemea mapungufu ya sheria hiyo.

Pamoja na nia nzuri ya sheria hiyo, wajuzi kama wewe wamebaini mapungufu makubwa ya wazi ambayo kwa hakika yako wazi kwa mtaalamu au hata asiyekuwa mtaalamu wa sheria kuyaona.

NASIKITIKA HUKO TUENDAKO NA MUSTAKABALI WA HAKI NCHINI KUPITIA SHERIA KANDAMIZI
 
Yeye atastaafu lini?

Wenzake wote wa umri wake walistaafu miaka mingi, yeye atastaafu lini? Labda anajipendekeza aongezewe muda.

Njaa mbaya sana.
 
lost id

Asante uko sawa astaafu, ilibidi asimfurahishe JPM, asemee mapungufu hayo maana kauli yake inaweza kuleta mabadiliko. Kama ananyamaza anasema mambo ya nia nzuri, NADHANI KUNA WALAKINI!

Lakini nakumbuka alipoteuliwa na rais JK at that time, wadau wa sheria hakuwakuwa COMFORTABLE!

How old is he?
 
Jamani twendeni kifungu kwa kifungu sheria hii inatatizo wapi.huko uk..usa ndo wanasheria kali kuliko hii.hebu tuwe critical thinker tujenge hoja vifungu gani havifai katika sheria hii.maaana hata mabalozi wanaowakilosha nchi zao walipoulizwa which spec provision walikosa kifungu.

Mimi naona kinachokosekana ni strategy ya jinsi ya ku deal na makosa haya na nn kifanyike maana saaa inaonekana ni ya upande mmja while sio kweli. cyber crime ni makosa kama makosa mengine ya jinai kama watu hawashtaki nani wakulaumiwa? Wale wanaoshtaki hatua zinachukuliwa
 
Jamani twendeni kifungu kwa kifungu sheria hii inatatizo wapi.huko uk..usa ndo wanasheria kali kuliko hii.hebu tuwe critical thinker tujenge hoja vifungu gani havifai katika sheria hii.maaana hata mabalozi wanaowakilosha nchi zao walipoulizwa which spec provision walikosa kifungu.
Mimi naona kinachokosekana ni strategy ya jinsi ya ku deal na makosa haya na nn kifanyike maana saaa inaonekana ni ya upande mmja while sio kweli.cyber crime ni makosa kama makosa mengine ya jinai kama watu hawashtaki nani wakulaumiwa? Wale wanaoshtaki hatua zinachukuliwa


USA unamanisha USARIVER au USA hii ninayoijua mimi?

Tumia hata aikili kidogo japo vijana wengi MNA UTAPIAMLO WA UBONGO NA MWILI.

Kifupi UNYAFUZI ni janga nchi hii. hasa hawa vijana wa 90's.
 
Ni Kweli majaji wote wa Tanzania hawakuwa na furaha na uteuzi wa kujuana wa huyu Bwana!

Alitoka alipotoka, walimtegemea nguli wa sheria na majaji waliobobea waongoze na kupewa ujaji mkuu! Anatakiwa apumzike maana mahakama imekuwa kama ime paralyse kwa miaka yote aliokuwepo!

Hakubaliki na hana weledi ulee unaokubalika yeye ni kujipendekeza kwa wakubwa kwa maslahi yake! Sheria iko wazi na mapungufu yake anajitoa akili uzeeni kwa kuweka njaa akilini! Aibu
 
Na yeye atastaafu lini maana wenzake wote wa umri wake washastaafu.

Anajipendekeza apewe mkataba mwingine au aongezewe muda.

Njaa mbaya sana.
Ww na yeye mwenye njaa nani?Wakati mwingine kabla hujaandika jambo yakupasa ujifikrishe japo kidogo ndg.Vinginevyo ni sawa na kujitusi ww mwenyewe.
 
Kwani mapungufu ya hii Sheria ni yapi?

Maana isije ikawa ni mapungufu tu kwa kuwa kuna mafundi wa kulalamika.
 
Back
Top Bottom