Jaji Mkuu aagiza nakala za hukumu kutolewa bure

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,698
Reaction score
2,262
JAJI MKUU 2.jpg
​

Jaji Mkuu wa Tanzania Prof Ibrahim Hamis Juma amewaagiza Mahakimu wote nchini kutoa bure nakala za hukumu kwa wananchi ili kurahisisha upatikanaji wa Haki.

Akizungumza wakati wa ziara yake katika Mahakama za wilaya ya Uvinza na Kasulu mkoani Kigoma leo, Jaji Mkuu amewaambia Mahakimu hao kuwa endapo watakutana na kikwazo cha Sheria, au Kanuni katika kutekeleza agizo hilo wasisiste kumpelekea mapendezo yao.

Jaji Mkuu amefikia uamuzi huo kutokana na Maboresho ya Huduma za Mahakama yanayoendelea pamoja na utekelezaji wa Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Mahakama ya Tanzania (2015/16 hadi 2019/20).

Alisema ni haki ya kila Mwananchi aliyekuwa na kesi mahakamani kupatiwa nakala ya hukumu yake ndani ya siku 21 tangu kusomwa kwa hukumu hiyo au mapema iwezekanavyo mara baada ya kesi yake kutolewa hukumu. Nakala ya hukumu imekuwa ikilipiwa kiasi cha shilingi elfu kumi (10,000) kama gharama ya uandaaji wa nakala hiyo.

Akizungumzia maboresho ya huduma za mahakama, Prof. Juma alisema Mahakama inao mpango wa kuanzisha Mahakama zinazotembea (Mobile Courts) ili kutatua changamoto ya upungufu wa Mahakama kwenye baadhi ya Maeneo nchini ikiwemo mikoa ya Tabora na Kigoma. Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, Zaidi ya watanzania milioni 25 wako mbali na huduma za Mahakama.

Chanzo: Nipashe
 
Wakitoa nakala ya hukumu siku hiyo hiyo ya hukumu itakuwa ni vizuri zaidi hata kama tutalipia
 
Jaji Mkuu, we are in dire need of an Independence of the Judiciary, the rest is Rubbish if the independence of the judiciary is not guaranteed!
upload_2018-2-27_15-45-58.png
 
Hakimu/jaji your core duty ni kusikiliza na kutolea maamuzi kesi na unalipwa mshahara kwa kazi hiyo. Yet, wananchi walipie hukumu zitokanazo na majukumu yenu ya msingi! Hii sio consultancy work ndio kazi yenu iliyowaweka huko maofisini/mahakamani. Ni sawa na wanafunzi walipie notes wanazopewa na mwalimu. Sikuwahi kuwaza kama kuna upumbavu wa aina hii aisee!
 
Shida yetu n uhuru wa mahakama mana kuna mhimil ulisema umejchmbia cjui aliyatoa kkt katba ya nchi gan?hlo ulosema kwe2 co ishu
 
Jaji Mkuu wa Tanzania Prof Ibrahim Hamis Juma amewaagiza Mahakimu wote nchini kutoa bure nakala za hukumu kwa wananchi ili kurahisisha upatikanaji wa Haki.

Akizungumza wakati wa ziara yake katika Mahakama za wilaya ya Uvinza na Kasulu mkoani Kigoma leo, Jaji Mkuu amewaambia Mahakimu hao kuwa endapo watakutana na kikwazo cha Sheria, au Kanuni katika kutekeleza agizo hilo wasisiste kumpelekea mapendezo yao.

Jaji Mkuu amefikia uamuzi huo kutokana na Maboresho ya Huduma za Mahakama yanayoendelea pamoja na utekelezaji wa Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Mahakama ya Tanzania (2015/16 hadi 2019/20).

Alisema ni haki ya kila Mwananchi aliyekuwa na kesi mahakamani kupatiwa nakala ya hukumu yake ndani ya siku 21 tangu kusomwa kwa hukumu hiyo au mapema iwezekanavyo mara baada ya kesi yake kutolewa hukumu. Nakala ya hukumu imekuwa ikilipiwa kiasi cha shilingi elfu kumi (10,000) kama gharama ya uandaaji wa nakala hiyo.

Akizungumzia maboresho ya huduma za mahakama, Prof. Juma alisema Mahakama inao mpango wa kuanzisha Mahakama zinazotembea (Mobile Courts) ili kutatua changamoto ya upungufu wa Mahakama kwenye baadhi ya Maeneo nchini ikiwemo mikoa ya Tabora na Kigoma. Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, Zaidi ya watanzania milioni 25 wako mbali na huduma za Mahakama.

Chanzo: Nipashe
Huyu jaji naye kawa mpumbavu...tunataka HUKUMU ZA HAKI siyo hayo manakala yake, nakala ya kazi gani kama hukumu siyo ya HAKI?
 
..kwanini waliohukumiwa wasipewe nakala za hukumu zao mara baada ya kuhukumiwa?

..kuna ugumu gani siku ya hukumu hakimu kuwa na nakala yake ambayo ataisoma, na nakala za watuhumiwa, na nyingine kwa upande wa mwendesha mashtaka?

Petro E. Mselewa
 
Back
Top Bottom