VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,007
Jaji Damian Lubuva,Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,tunakuamini. Unafanya kazi ya kutukuka. Tafadhali wapuuze wapinzani.Usiruhusu Tume yako ifanye marekebisho Daftari la Kudumu la Wapigakura. Daftari hilo ndilo tunalolitegemea kama chama tawala.Ndilo uwanja wetu wa nyumbani. Libaki kama lilivyo. Usijali kelele zao.
Sisi tumenunua baadhi ya kadi za kupigia kura toka kwa wananchi watiifu kwetu.Ukifanya marekebisho watatudai kadi zao au kupewa mpya.Halafu,watatuacha mkono. Watapigia kura upinzani au sisi lakini hadi tuwabembeleze tena. Ukifanya marekebisho Daftarini, vijana wengi waliofikisha umri wa kupiga kura watajiandikisha. Halafu, wataleta 'vurugu' za kikura.
Ukirekebisha sasa Daftari la Kudumu la Wapigakura,wale ambao hawakujiandikisha 2010 watajiandikisha. Halafu, watasimama katikati kutaka kuvutiwa na upande fulani wa kisiasa. Kama chama tawala,hatuko tayari kurekebishwa kwa daftari hilo. Jaji Lubuva,zipuuze chopa za CHADEMA na wapinzani wengineo. Muda si huu.
Daftari likirekebishwa, majina ya marehemu yataondolewa.Halafu itakuwaje unadhani? Tunataka Daftari libaki.Kama lilivyo.Lisibadilishwe.Labda baada ya 2015.
Daftari la Kudumu na lidumu!!!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam