Jaji Lubuva ajibu mapigo ya UKAWA kuhusu BVR

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,496
3,461
Jaji LubuvaMauli Muyenjwa na Maneno Selanyika, Dar es Salaam
MWENYEKITI wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva, amewataka wanasiasa waache kutumia changamoto za mfumo wa kielektroniki wa uandikishaji wapigakura (Biometric Voter Registration-BVR) ili kujipatia umaarufu wa kisiasa.

Kauli hiyo ya Jaji Lubuva imekuja siku chache baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, kumuonya na kudai kamwe chama chake hakitakubaliana na vitendo vya hujuma ambavyo tayari tume hiyo imeanza dhidi ya upinzani.

Mbowe, alimtaka Jaji Lubuva asiwe adui wa demokrasia kwa kutoa uamuzi kama suala hilo ni la nyumbani kwake wakati nchi nzima iko kwenye ‘tension’ kuhusu daftari la wapigakura na mfumo wa BVR.

Akizungumza jana mjini Makambako wakati wa uzinduzi wa uandikishaji wa daftari la kudumu la wapigakura kwa kutumia mfumo wa BVR, Jaji Lubuva, alisema hoja za wanasiasa ambao wanapinga mchakato huo hazina uzito.

Alisema hata kama wangekata rufaa mahakamani, hoja zao zingetupwa kwa kukosa uzito.
“Pamoja na changamoto tulizokutana nazo katika mchakato huo, lakini tumefanya vizuri kwa kuwa zoezi hili ni zito na hakuna yeyote ambaye atafika kujiandikisha na akaachwa, wote watakaofika wataandikishwa.

“Ni vema wanasiasa waache kutumia changamoto za BVR kwa lengo la kujitafutia umaarufu, hili jambo si sawa hata kidogo,” alisema Jaji Lubuva.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, alipongeza kazi hiyo na kusema kuwa ilitegemewa siku ya kwanza ya uandikishaji wangeandikishwa watu 1,850 lakini NEC imefanikisha na kuandikisha watu 3,014 jambo ambalo ni la kupongezwa.

Kutokana na mafanikio hayo, aliwataka wanasiasa kuacha kauli za kuikatisha tamaa NEC, huku akiwataka kutoa ushirikiano kwani mfumo wa BVR umekuwa na mafanikio na umeshatumika katika nchi nyingi.

“Aprili 30, mwaka huu Kura ya Maoni ya Katiba Inayopendekezwa itapigwa kwa kutumia daftari linaloboreshwa sasa kwa mfumo huu wa BRV, na mabadiliko haya yamefanyika ili kuboresha ufanisi na kutoa haki sawa katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwaka huu na sio vinginevyo,” alisema Pinda.

Alisema NEC na Serikali wamejipanga vizuri katika mchakato huo, ambapo aliwaomba viongozi wa dini kutumia muda wao kutoa elimu kwa wananchi ili waweze kujitokeza kwa wingi katika maeneo yote litakapopita daftari la wapigakura.

Aliongeza kuwa vituo vya kupigia kura vimeongezeka na kufikia 40,150 ikilinganishwa na kipindi kilichopita ambapo vilikuwa 24,919.
“Kuongezeka kwa vituo hivyo kutachangia kuboresha upigaji kura katika sahemu mbalimbali, kwani kuanzia ngazi ya vitongoji, kata na vijiji vitakuwa na mashine hizi ili kupunguza msongamano na kutembea umbali mrefu ili kupiga kura,” alisema Pinda.

Chanzo:Mtanzania
 
Yaani hapo NEC inatapatap hiyo tarehe 30 hakuna kura hata ukimuangalia lubuva wakati anaongea ni km anawasiwasi na hana uhakika na kz yake
 
Mh. Jaji bado siku 53 toka leo hadi siku ya uchaguzi 2Oth April. Hapo nimeunganisha na Jumapili na Jmosi. Je tutakuwa tayari watanzania wote wenye sifa za kupiga kura tumo ndani ya daftari?
 
Hivi hilo daftari utaratibu wake ukoje? Yaani tarehe ipi litakuwa wapi na tarehe ipi tena litakuwa wapi ili wdau tujiandikishe maana mpaka sasa sijajua ni wapi pa kujiandikisha
 
UKAWA si wanatapatapa tu.

Nasikia ulizimia siku tatu mfululizo baada ya kuukosa udc na badala yake akaukwaa shoga yako huyu
 
Attachments

  • 1424859787365.jpg
    1424859787365.jpg
    26 KB · Views: 472
upumbavu wa lubuva na chama cha majangiri kitaligarimu taifa

Mh!Tupo Watanzania zaidi ya Millioni ishirini tunaotegemea kujiandikisha,mpaka leo ni machine 250 tu zilizokwisha kuwasili.Na hizo nyingine hazijulikani lini zitafika............

Mpaka April 30,na changamoto za mashine, sina uhakika hata robo ya watanzania itafikiwa.............Sina uhakika kama Judge Lubuva anatuona watanzania hatuna AKILI za kujua UWONGO na UKWELI ,basi hata kuuona ukweli pia!!!!!!!!!!!
 
Dawa ya Ma-ccm ni kuyaondosha kwa AK 47 tuu, njia nyingine zote ni kupoza muda tuu!
 
Lubuva ndiye anatakiwa ajione kufanya siasa pasipohitajika siasa. Si kila jambo likiongewa na wanasiasa linakuwa na mrengo wa kisiasa. Hawa pamoja na kufanya siasa, ni watanzania wenye taaluma, uelewa, nia na uzalendo wao unaoweka Tanzania mbele kabla ya itikadi za vyama.

Ningemwona Lubuva kajibu mapigo kama angeacha siasa, aka address challenges zilizotolewa na ambazo ni za msingi kuliko umaaarufu wa msemaji au aibu ya Lubuva na nia yake ya kujihami.

LUBUVA TUNATAKA UJIBU HOJA, NAMNA GANI TUME IMETATUA CHANGAMOTO ZINAZOAINISHWA KUHUSIANA NA BVR. Acheni kuwafanya watanzania wajinga kwa kutoa majibu yaliyo nje yahoja. Kama udhaifu wako ama failure yako inampa nafasi mkosoaji wako kuwa imara kisiasa, hilo ni jukumu lako kuhakikisha hutoi nafasi ya watu kutumia uovu wako kujiimarisha. Tunahitaji mfumo sahihi, ulio wazi, shirikishi na unaoeleweka kwa maslahi ya nchi yetu.

Kwendeni mbali nasi wenye fake motives mnaoota ndoto kuchakachua kila kitu. You are out of time guys!.

Jaji LubuvaMauli Muyenjwa na Maneno Selanyika, Dar es Salaam
MWENYEKITI wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva, amewataka wanasiasa waache kutumia changamoto za mfumo wa kielektroniki wa uandikishaji wapigakura (Biometric Voter Registration-BVR) ili kujipatia umaarufu wa kisiasa.

Kauli hiyo ya Jaji Lubuva imekuja siku chache baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, kumuonya na kudai kamwe chama chake hakitakubaliana na vitendo vya hujuma ambavyo tayari tume hiyo imeanza dhidi ya upinzani.

Mbowe, alimtaka Jaji Lubuva asiwe adui wa demokrasia kwa kutoa uamuzi kama suala hilo ni la nyumbani kwake wakati nchi nzima iko kwenye ‘tension' kuhusu daftari la wapigakura na mfumo wa BVR.

Akizungumza jana mjini Makambako wakati wa uzinduzi wa uandikishaji wa daftari la kudumu la wapigakura kwa kutumia mfumo wa BVR, Jaji Lubuva, alisema hoja za wanasiasa ambao wanapinga mchakato huo hazina uzito.

Alisema hata kama wangekata rufaa mahakamani, hoja zao zingetupwa kwa kukosa uzito.
"Pamoja na changamoto tulizokutana nazo katika mchakato huo, lakini tumefanya vizuri kwa kuwa zoezi hili ni zito na hakuna yeyote ambaye atafika kujiandikisha na akaachwa, wote watakaofika wataandikishwa.

"Ni vema wanasiasa waache kutumia changamoto za BVR kwa lengo la kujitafutia umaarufu, hili jambo si sawa hata kidogo," alisema Jaji Lubuva.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, alipongeza kazi hiyo na kusema kuwa ilitegemewa siku ya kwanza ya uandikishaji wangeandikishwa watu 1,850 lakini NEC imefanikisha na kuandikisha watu 3,014 jambo ambalo ni la kupongezwa.

Kutokana na mafanikio hayo, aliwataka wanasiasa kuacha kauli za kuikatisha tamaa NEC, huku akiwataka kutoa ushirikiano kwani mfumo wa BVR umekuwa na mafanikio na umeshatumika katika nchi nyingi.

"Aprili 30, mwaka huu Kura ya Maoni ya Katiba Inayopendekezwa itapigwa kwa kutumia daftari linaloboreshwa sasa kwa mfumo huu wa BRV, na mabadiliko haya yamefanyika ili kuboresha ufanisi na kutoa haki sawa katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwaka huu na sio vinginevyo," alisema Pinda.

Alisema NEC na Serikali wamejipanga vizuri katika mchakato huo, ambapo aliwaomba viongozi wa dini kutumia muda wao kutoa elimu kwa wananchi ili waweze kujitokeza kwa wingi katika maeneo yote litakapopita daftari la wapigakura.

Aliongeza kuwa vituo vya kupigia kura vimeongezeka na kufikia 40,150 ikilinganishwa na kipindi kilichopita ambapo vilikuwa 24,919.
"Kuongezeka kwa vituo hivyo kutachangia kuboresha upigaji kura katika sahemu mbalimbali, kwani kuanzia ngazi ya vitongoji, kata na vijiji vitakuwa na mashine hizi ili kupunguza msongamano na kutembea umbali mrefu ili kupiga kura," alisema Pinda.

Chanzo:Mtanzania
 
J
MWENYEKITI wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva, amewataka wanasiasa waache kutumia changamoto za mfumo wa kielektroniki wa uandikishaji wapigakura (Biometric Voter Registration-BVR) ili kujipatia umaarufu wa kisiasa.

Ninachukia sana jinsi watanzania wanavyotumia huu msamiati wa CHANGAMOTO ie. challanges

Utamsikia Mwalimu, wanafunzi wake hawajui kusoma wala kuandikia akisema kwamba Shule yangu ina changamoto ya wanafunzi kutojua kusoma na kuandika!

Shule haina madawati. Mwalimu mkuu utamsikia anasema kwamba Shule yangu ina changamoto ya kutokuwa na madawati!

Mtanzania hana fedha mfukoni. Utamsikia anasema nina changamoto ya kutokuwa na fedha naomba unikopeshe.

Mtanzania amefiwa na baba/mama yake, Utasikia anasema nina changamoto ya kufiwa na baba/mama yangu!

Sasa sikia huyu ni Judge, NEC haina vifaa vya kutosha vya kuandikisha wapiga kura. Vifaa vilivyopo kwasasa ni 250 badala ya 5,000 vinavyotakiwa kuandikisha Watanzania wote wenye sifa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura.

Yeye tatizo hilo la ukosefu wa vifaa vya kukidhi mahitaji anaita chagamoto!

Kukosa vifaa vya kutosha inakuwa CHANGAMOTO kweli?!

Msamiati wa matatizo umegeuzwa kuwa changamoto!
 
Mbona sielewi kwani Dares salaam wameshamaliza uandikishaji?
 
mtoto wa lubuva ni mwenyekit serikali ya mtaa oysterbay hapo mnategemea nini?
 
Back
Top Bottom