Mkuu ulipotea sana , hebu nijalie matokeo ya marudio ya uchaguzi wa Serikali za mitaa huko Sumbawanga.
mkuu acha uchokozi,...timu nzima ya LB bk7 haikuonekana jana, sasa unataka wakimbie tena?
BTW: nasikia magamba wameyapinga matokeo hayo.
Mkuu ulipotea sana , hebu nijalie matokeo ya marudio ya uchaguzi wa Serikali za mitaa huko Sumbawanga.
Haaaahaaahaaaaaaaaaa! Umenikuna! Basi tu nina changamoto sio demu vinginevyo ningehakikisha 'nakupa'Ninachukia sana jinsi watanzania wanavyotumia huu msamiati wa CHANGAMOTO ie. challanges
Utamsikia Mwalimu, wanafunzi wake hawajui kusoma wala kuandikia akisema kwamba Shule yangu ina changamoto ya wanafunzi kutojua kusoma na kuandika!
Shule haina madawati. Mwalimu mkuu utamsikia anasema kwamba Shule yangu ina changamoto ya kutokuwa na madawati!
Mtanzania hana fedha mfukoni. Utamsikia anasema nina changamoto ya kutokuwa na fedha naomba unikopeshe.
Mtanzania amefiwa na baba/mama yake, Utasikia anasema nina changamoto ya kufiwa na baba/mama yangu!
Sasa sikia huyu ni Judge, NEC haina vifaa vya kutosha vya kuandikisha wapiga kura. Vifaa vilivyopo kwasasa ni 250 badala ya 5,000 vinavyotakiwa kuandikisha Watanzania wote wenye sifa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura.
Yeye tatizo hilo la ukosefu wa vifaa vya kukidhi mahitaji anaita chagamoto!
Kukosa vifaa vya kutosha inakuwa CHANGAMOTO kweli?!
Msamiati wa matatizo umegeuzwa kuwa changamoto!