Jaji Joseph Sinde Warioba; Mzalendo aliyebaki Tanzania

Uncle Jei Jei

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
1,493
2,000
Tangu nimemfahamu huyu mzee, binafsi nimejifunza vitu vingi kwake. Ni mpole, mtulivu, mwenye kutafakari kabla ya kusema na mwenye kusema baada ya kuamua.

Katika mchakato wa kukusanya maoni ya katiba mpya, wengi tunafahamu vikwazo na misukosuko aliyokutana nayo ikiwemo kugeukwa hadharani na Boss aliyempa kibarua hicho baada ya kuonekana kujali kilichosemwa na watu kuliko kinachosemwa na wakubwa zake.

Baada ya yote hayo, alikaa kimya, alitulia na akavumilia kila aina ya kejeli zilizo vurumishwa kwake! Ilifikia hatua ya watu kudhani pengine angehama chama chake cha siasa na kujiunga na siasa za upinzani! Lakini, alidhihirisha kuwa ili ukosoe viongozi wako si lazima uhame chama. Hili alilifanya hata Martin Luther alipoukosoa mfumo wa U-Katoliki. Hakuanzisha dhehebu ila wafuasi wake ndio walioanzisha baada ya yeye kufariki. Alipigania "reformation".

Katika kutoa maoni yake kuhusu kinachoendelea kwenye Makinikia; wimbo uliovuma zaidi wiki hii, yeye amempongeza Rais kwa uthubutu aliouonyesha. Baada ya pongezi zake, hakusita kutoa maoni yake kuwa si vema sana watu wakijikita kujadili nani alifanya kosa gani na achukuliwe hatua gani, bali ameshauri kwasababu kosa limeonekana ni vema sana tusonge mbele kwa kurekebisha makosa hayo kwa kuweka mfumo thabiti wa kulinda rasilimali zetu ili makosa hayo yasitokee tena.

Yeye ni mbobezi wa sheria, huenda hadi kufikia hapo ameona kasoro zilizokuwepo kisheria zilizowapo mwanya wafanya makosa hao kuyafanya! Sasa anajaribu kushauri mianya hiyo izibwe. Mimi naungana naye hasa baada ya kuonekana wengine wanapewa kinga na wengine wananyang'anywa kinga! Hii itasababisha mdogo kuumia kwa kosa la mkubwa. Hivyo kama nchi, yaliyopita si ndwele hatuna budi kuganga yajayo! Kiongozi mzuri hana budi kuchora msatari na kuweka alama ya "starting point". Tukisha chora mstari, itakuwa rahisi kuwashughulikia waliotoka nje ya mstari! Huenda waliopita hawakuchora huo mstari kwa level ya nchi, au waliochora kisha wakaufuta. Ni muda sasa umefika tuchore mstari kwa rangi nzito kisha ufuto wa rangi hiyo tuutumbukize baharini ambapo kila ajaye hatakuwa na ufutio wa kuufuta bali kurekebisha kulingana na mazingira ya wakati husika!
 
Aaron

JF-Expert Member
Nov 18, 2010
3,020
2,000
Magu nitamuelewa kuwa ni mzalendo kama atasimama hadharan na kutamka kuiunga mkono tume ya warioba kwa mapendekezo ya katiba ya wananchi.... Asipofanya hivyo nae ni mpiga dili kama wengine
 
xaracter

JF-Expert Member
Jul 28, 2015
1,027
2,000
Tangu lini CCM kukawa na mzalendo? Huyu nae ni mfia chama bora nchi iteketee chama kibaki. Kapigwa vibao na DAB na bado kaenda kukipigia chama kampeni kwa kuogopa mwanae kukosa uteuzi kugombea jimbo la kawe.eti Mzalendo kama hujui maana ya uzalendo ctfu!
 
Lambardi

JF-Expert Member
Feb 7, 2008
10,814
2,000
Kashfa za Tangold na Meremeta....jumlisha hili la Airtel.....bado tunae tu mzalendo wetu Jaji Warioba?? Au tatizo ni mfumo ndani ya fisiemu...? Usafi wake uko wapi? Tupeni report zote za hayo makampuni ma 3......mumsafishe ili abakie na uzalendo wake....ama la kuna doa zito sana hapo!!!
 
Hawaki

JF-Expert Member
Mar 29, 2017
534
1,000
Kwani uzalendo maana yake nini? Huyo si ndio aliyekuwa awamu ya kwanza na kuwaletea nguo za marikani na kaniki Tanzania?
 
johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
36,640
2,000
Tangu nimemfahamu huyu mzee, binafsi nimejifunza vitu vingi kwake. Ni mpole, mtulivu, mwenye kutafakari kabla ya kusema na mwenye kusema baada ya kuamua.

Katika mchakato wa kukusanya maoni ya katiba mpya, wengi tunafahamu vikwazo na misukosuko aliyokutana nayo ikiwemo kugeukwa hadharani na Boss aliyempa kibarua hicho baada ya kuonekana kujali kilichosemwa na watu kuliko kinachosemwa na wakubwa zake.

Baada ya yote hayo, alikaa kimya, alitulia na akavumilia kila aina ya kejeli zilizo vurumishwa kwake! Ilifikia hatua ya watu kudhani pengine angehama chama chake cha siasa na kujiunga na siasa za upinzani! Lakini, alidhihirisha kuwa ili ukosoe viongozi wako si lazima uhame chama. Hili alilifanya hata Martin Luther alipoukosoa mfumo wa U-Katoliki. Hakuanzisha dhehebu ila wafuasi wake ndio walioanzisha baada ya yeye kufariki. Alipigania "reformation".

Katika kutoa maoni yake kuhusu kinachoendelea kwenye Makinikia; wimbo uliovuma zaidi wiki hii, yeye amempongeza Rais kwa uthubutu aliouonyesha. Baada ya pongezi zake, hakusita kutoa maoni yake kuwa si vema sana watu wakijikita kujadili nani alifanya kosa gani na achukuliwe hatua gani, bali ameshauri kwasababu kosa limeonekana ni vema sana tusonge mbele kwa kurekebisha makosa hayo kwa kuweka mfumo thabiti wa kulinda rasilimali zetu ili makosa hayo yasitokee tena.

Yeye ni mbobezi wa sheria, huenda hadi kufikia hapo ameona kasoro zilizokuwepo kisheria zilizowapo mwanya wafanya makosa hao kuyafanya! Sasa anajaribu kushauri mianya hiyo izibwe. Mimi naungana naye hasa baada ya kuonekana wengine wanapewa kinga na wengine wananyang'anywa kinga! Hii itasababisha mdogo kuumia kwa kosa la mkubwa. Hivyo kama nchi, yaliyopita si ndwele hatuna budi kuganga yajayo! Kiongozi mzuri hana budi kuchora msatari na kuweka alama ya "starting point". Tukisha chora mstari, itakuwa rahisi kuwashughulikia waliotoka nje ya mstari! Huenda waliopita hawakuchora huo mstari kwa level ya nchi, au waliochora kisha wakaufuta. Ni muda sasa umefika tuchore mstari kwa rangi nzito kisha ufuto wa rangi hiyo tuutumbukize baharini ambapo kila ajaye hatakuwa na ufutio wa kuufuta bali kurekebisha kulingana na mazingira ya wakati husika!
Nasikia kaharufu ka Airtel!!
 
Kunta Kinte

JF-Expert Member
May 18, 2009
3,689
2,000
MZALENDO? mzalendo aliyetumia mabilioni ya nchi kupata maoni ya katiba mpya halafu chama chake kimeyakataa nayeye kakaa kimya!? Huyo ni mjali maslahi binafsi hana tofauti na wenzie huko aliko!
 
dume kubwaaaa

JF-Expert Member
Jan 18, 2014
256
195
Hayo yote yatawezekana kupitia katiba mpya tena iliyobora kwa maslahi mapana ya nchi sio maslahi ya vyama au vikundi fulani fulani
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom