Jaji Augustino Ramadhani achukua Fomu kugombea Urais wa JMT

Jiulize kwanza amestaafu lini kuwa jaji, pili kabla ya kuwa jaji alikuwa wapi na je hakuruhusiwa kuwa mwanachama wa CCM au chama chochote cha siasa, na tatu alipokuwa jaji aliendelea kuwa mwanchama wa CCM?

I am not sure if you were trying to answer my questions or you just added more questions to the persons concerned.

In any case, Tanzania's system of governance and likes is quiet complicating and too political.
 
Wana JF,
Hali ya watia nia imekuwa ya wasiwasi baada ya mtia nia mwenzao kutoka Zanzibar kuja na begi zima la vigezo, ni jambo la kushangaza sana jinsi Mzee wa magogoni anayeaga kila kukicha alivyomfikilia na kumtaja kimafumbo baada ya kusema kwamba bado hajaona mgombea na nahodha anayefaa kuvaa viatu vyake na kushika usukani kutupeleka safari ya mafanikio isiyo safari ya matumizi iliyokuwepo.

Mtia nia Profesa, Jaji, Bredgedia Mchungaji Augostini Ramadhani huenda ndiye atakayekuwa chaguo la walio wengi kutoka CCM inayoandamwa na kundi kubwa la mbwa mwitu wanaotaka kula nchi hii kuibakiza mifupa.

Japokuwa mtia nia mwingine aliyeshawishiwa kutokana na mwitikio wa JK kuwaita watia nia wenzake vibaka uenda akaanza kupunguza kasi ya kumwachia huyu mwenye vigezo vyote, aidha ataweza kumaliza matatizo yote ya vikundi vilivyofikia vitatu mpaka sasa na kujenga team za ushindani, team hizi zinaonyeshana ubabe wa matumizi katika kusaka udhamini kama kwamba kuna mashindano ya kuonyeshana nani ana fedha zaidi au marafiki zaidi kumwingiza sehemu nyeti kuchota hazina iliyobaki. Hata hivyo ujio wa Mchungaji Ramadhani utaleta angalau haueni kwa walalahoi wapenzi wa CCM waliopoteza matumaini baada ya chama chao kuvamiwa na kundi la mabwanyenye.
 
Ntafurahi kumuona jaji Ramadhan akipeperusha bendera ya ccm mwaka huu.Nadhani ndiyo chaguo sahihi
 
Upele umepata mkunaji, kizuri chajiuza, wacha vibaya viendelee kujitembeza na maigizo mikoani
 
Raisi aliyelea Rushwa kwenye taasisi yake mpaka akachaguliwa mamba moja ndo aje kuwa eti rais Leo? labda kwa chama chenu cha wala Rushwa, hana uwezo wa kusimama akasema hiki na akaweza, huyu ni mseminari aendelee na kazi za kuhumga kondoo
 
Kwa Tanzania ilipofikia haitoshi kumchagua mtu kwa kuwa ni Muadilifu, je mbali ya uadilifu ana ujasiri wa kukabili wala Rushwa ipasavyo? Jaji Augustine Ramadhani si fisadi wala Mla rushwa lakini hana record ya ujasiri wa kupambana na vitendo vya Rushwa. Rushwa katika Mahakama kaikuta na kaicha hajawahi kuikabili je tutaamini Vipi atawakabili wezi
 
Kiukweli, Mheshimiwa huyu, hana doa, wala mawaa,
Amefurika hikma, na busara sana ( kulingana na kauli zilizotolewa na watu walofanya kazi naye)

labda pengine tu ule UPOLE wake, ndo issue.
Maana nchi hii inahitaji kwa nguvu zote, apatikane DIKTETA

attachment.php
 

Attachments

  • jaji ramadhani.jpg
    jaji ramadhani.jpg
    9.7 KB · Views: 590
Atakuwa yeye au watu wake wa karibu wanapitia uzi huu. Kwa kweli akikabidhiwa nchi aweke upole wake kando kwani tunahitaji kuwekwa kwenye mstari!
 
Huyu ni mzuri .,tatizo mlango aliopitia.....!
Kawekwa na wale wale. Wala hawezi kuwa kinyume nao.kiufupi janja ya nyani.....
 
jaji ramadhani ni kiongozi wa kanisa la anglican kwa kuteuliwa na askofu mkuu wa kanisa hilo wa uingereza,hajaachia nafasi hizo na hatarajii,kanisa hili ni wakala wa uingereza popote lilipo,je ugombea wa jaji ramadhani una msukumo wa uingereza?
 
Na wanataka alete ushoga tanzania. Wameshaweza nchi za SA. Na mozambique huko ushoga umeshalalalishwa kennya nao watahalalisha obama akiondoka ..
Ushoga wanavuleta kama missionary walivyoleta dini. Walipata vipingamizi ila mwishowe mababu zetu wakakaa wenyewe
 
jaji ramadhani ni kiongozi wa kanisa la anglican kwa kuteuliwa na askofu mkuu wa kanisa hilo wa uingereza,hajaachia nafasi hizo na hatarajii,kanisa hili ni wakala wa uingereza popote lilipo,je ugombea wa jaji ramadhani una msukumo wa uingereza?

Kwa nini unathubutu kuandika upuuzi? Kama hujui kitu, kukaa kimya ni hekima kubwa.

Askofu Mkuu wa Uingereza hana mamlaka ya kuiteulia nchi nyingine Askofu, siuze Mchungaji! Askofu mkuu wa Uingereza wala hachaguliwi na Maaskofu wa Anglikana duniani ktk kusanyiko lao.

Utendaji wa Askofu ktk Anglikana ni tofauti sana na Katoliki ambapo Mamlaka ya Papa hufika hadi nchi na jimbo la nchi nyingine ndani ya Kanisa hilo.

Vv
 
Back
Top Bottom