Jaji amuonya Manji kesi ya Mengi

Status
Not open for further replies.

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,422
911,172
Jaji amuonya Manji kesi ya Mengi

Na Mwandishi Wetu

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania imemwonya mfanyabiashara wa jijini Dar es Salaam Bw. Yusuf Manji kuacha kuchelewesha usikilizaji wa kesi dhidi yake kwa kubadilisha mawakili kila inapopangwa kuanza kusikilizwa.Onyo hilo lilitolewa jana na Jaji wa
Mahakama hiyo, Bw. John Utamwa wakati akitoa uamuzi huo katika kesi ya kashfa iliyofunguliwa dhidi yake na Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni za IPP, Bw. Reginald Mengi.

Uamuzi huo ulitokana na pingamizi lililowekwa na wakili wa mlalamikaji, Bw. Michael Ngalo aliyelalamikia ucheleweshwaji wa kesi hiyo ya mwaka 2006 na kudai umekuwa ukifanywa kwa makusudi na Bw. Manji kwa kuleta mawakili wapya kila shauri hilo linapokuja mahakamani kwa ajili ya kuanza kusikilizwa.

Mbele ya mawakili wa pande zote mbili, huku Manji akiwakilishwa na mawakili watano, Jaji Utamwa alisema mara ya mwisho kesi hiyo iliahirishwa Oktoba 25 mwaka huu na kupangwa kuanza kusikilizwa Desemba 13 mwaka huu lakini iliahirishwa tena baada ya jopo la mawakili wa Bw. Manji kutotokea mahakamani.

Badala yake siku hiyo, alifika wakili Cuthebert Tenga ambaye aliomba kesi hiyo iahirishwe kwa madai kuwa Bw. Manji ameweka mawakili wapya na siku hiyo walikuwa na kesi zingine.

Jaji Utamwa alikubaliana na Bw. Ngalo kuwa utaratibu wa kubadilisha mawakili kila kesi hiyo inapokuja kwa ajili ya kuanza kusikilizwa unachelewesha mwenendo wa kesi na kuanzia sasa hatakubali tena hali hiyo ijitokeze.

Tangu kesi hiyo ipowasilishwa mahakamani hapo, baadhi ya mawakili waliojitokeza kutetea na baadaye kujitoa ni pamoja na Rattansi, Theonist Rutashoborwa, Muganyizi, Jamal na baadaye alirejea tena Rattansi.

Jopo la mawakili linalomtetea sasa Bw. Manji katika kesi yake na Bw. Mengi ni Bw. Yuda Tadey, Dkt. Ringo Tenga, Bw. Mabere Marando, Bw. Richard Rweyongeza, Tausi Abdallah na Bw. Cuthbert Tenga.

Baada ya kutoa uamuzi huo, jopo hilo la mawakili wa Bw. Manji ambalo jana liliongozwa na Bw. Marando, waliingia katika mzozo mwingine wa kutaka Wazee Baraza katika kesi hiyo, wajitoe. Hoja hiyo iliyosababisha kesi ya msingi isimame kwa takribani nusu saa, iliibuliwa na Bw. Marando akitaka wazee hao wa Baraza, Bw. Ndimara Tegambwage, Bi. Rose Haji na Bw. Lugano Mbwina wasiwepo kwenye kesi hiyo kwa madai kuwa ni wana habari, hivyo wanaweza kuwa na mawasiliano na Bw. Mengi kwa vile ni mmiliki wa vyombo vya habari na pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari nchini (MOAT).

“Mheshimiwa Jaji, kwa kuwa sheria inayowapa nguvu Wazee wa Baraza kuwepo mahakamani imeshabadilishwa na kwa kuwa Bw. Mengi ni mmiliki wa vyombo vya habari na kiongozi wa MOAT na kwa kuwa wazee wote wa Baraza ni wanahabari kuna uwezekano wa wao kukutana na Bw. Mengi na kuathiri haki ya mteja wetu, hivyo wasiwepo kwenye kesi hiyo,” alidai Bw. Marando.

Hata hivyo Jaji Utamwa alitupilia mbali madai hayo na kutaka kesi hiyo ianze kusikilizwa. Shahidi wa kwanza kupanda kizimbani jana alikuwa Bw. Mengi ambaye alidai kuwa Bw. Manji alimkashifu na kumchafulia jina kupitia matangazo aliyoyatoa kwenye magazeti ya Tanzania Daima, Mtanzania, Tazama Tanzania na Majira.

Huku akihojiwa na Wakili Ngalo, Bw. Mengi alidai kuwa Manji kupitia matangazo hayo, alimwita mwongo, mzushi na kwamba amezoea kuzusha uongo kwamba anatishiwa maisha, kauli ambazo alidai zimemchafulia jina na kumuathiri kisaikolijia.

Kutokana na hali hiyo, Bw. Mengi amedai fidia ya mabilioni ya fedha. Kesi hiyo inayovuta hisia za wengi, imeahirishwa hadi Februari 15 mwakani.
 
Kweli Manji ana kesi nyingi kuliko umri wake na nina imani atazipangua zote.
 
hivi hii imekaaje waungwana. Mabere Marando hivi juzi tu alikuwa anazunguka nchi nzima katika kampeni za chadema akilaani chama cha CCM kuwa kimebeba mafisadi na wala rushwa. Huyu Manji ni mwanachama wa CCM na ambaye amekuwa akitajwa na Mengi kuwa ni fisadi( rejea list yake ya mafisadi papa) na hata hiyo kesi iliyoko mahakamani chanzo chake ni hili zogo la ufisadi.

Suala linalosumbua ubongo wangu ni je iweje Mabere Marando leo asimame mahakamani kumtetea fisadi dhini ya mpinga ufisadi halafu kesho asimame tena majukwaani akiwapinga na kuwalaani mafisadi kuwa wanaiharibu nchi hii. katika sheria wanasema 'every person has the right to legal representation' hili nakubaliana nalo lakini pia upande wa pili wakili anaweza kujitoa kumtetea mteja endapo ataona ana interest katika hilo jambo....sasa huyu Marando yeye ni Anti-ufisadi then anasimama kumtetea fisadi, hii imekaaje wana-JF
 
hata mm inanichanganya..ladba ni njaa inamsumbua huyu jamaaaaaaa.
hapo umenena mkuu...
 
hana ishu huyo manji ni kaburu kama hotuba ya nyerere siku za nyuma ,asinge kubali hili kaburu lituendeshe na vijisent vyake
 
hivi hii imekaaje waungwana. Mabere Marando hivi juzi tu alikuwa anazunguka nchi nzima katika kampeni za chadema akilaani chama cha CCM kuwa kimebeba mafisadi na wala rushwa. Huyu Manji ni mwanachama wa CCM na ambaye amekuwa akitajwa na Mengi kuwa ni fisadi( rejea list yake ya mafisadi papa) na hata hiyo kesi iliyoko mahakamani chanzo chake ni hili zogo la ufisadi.

Suala linalosumbua ubongo wangu ni je iweje Mabere Marando leo asimame mahakamani kumtetea fisadi dhini ya mpinga ufisadi halafu kesho asimame tena majukwaani akiwapinga na kuwalaani mafisadi kuwa wanaiharibu nchi hii. katika sheria wanasema 'every person has the right to legal representation' hili nakubaliana nalo lakini pia upande wa pili wakili anaweza kujitoa kumtetea mteja endapo ataona ana interest katika hilo jambo....sasa huyu Marando yeye ni Anti-ufisadi then anasimama kumtetea fisadi, hii imekaaje wana-JF

Kumbuka ndugu yangu "every person has a price" Tanzania hakuna wapiganaji wa ufisadi, bado hawajazaliwa, waliopo ni nwale wanaona wanaweza kushibisha matumbo yao kwa kujifanya ni wapambanaji dhidi ya ufisadi!
 
Status
Not open for further replies.
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom