Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 233
mambo naona sasa yameiva , ninauhakika usahahidi utatolewa lakini watautia kapuni kama spika alivyo fanya kwa swala la Lema na Lisu
IMMA inasimamia majina ya wamiliki wa kampuni hiyo ya mawakili ambao ni Protase Ishengoma, Lawrence Masha, Aloysius Mujulizi na Sadock Magai.
Mmoja wa wamiliki wa kampuni hiyo, Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha aliithibitishia MwanaHALISI kwamba ni mwanzilishi na mmiliki wa IMMA.
Hata hivyo aliharakisha kusema kwamba kwa sasa amekabidhi majukumu yake kwa wakurugenzi wake wengine baada ya kuchukua wadhifa serikalini.
"Ni kweli kwamba mimi ni mmoja wa wakurugenzi waanzilishi wa IMMA, lakini kwa sasa siko huko. Nimeacha kujishughulisha na shughuli za kampuni hiyo tangu mwaka 2005 nilipoingia serikalini," alisema Masha.
Aidha, Masha alithibitisha pia kwamba kampuni ya IMMA ndiyo iliyosajili kampuni ya Deep Green Finance Limited na kwamba ni kweli kuwa inamwajiri Ridhwan.
Hata hivyo, Masha amesema mwenye nafasi nzuri zaidi ya kuzungumzia masuala ya IMMA hivi sasa ni mkurugenzi mwendeshaji, Protase Ishengoma.
Ridhwani alifanya kazi katika kampuni hiyo ya uwakili akiwa bado kwenye mafunzo mara baada ya kupata shahada yake ya sheria kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.