Jaji ajitoa kesi ya Lema wa Arusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jaji ajitoa kesi ya Lema wa Arusha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sumasuma, Feb 7, 2012.

 1. sumasuma

  sumasuma JF-Expert Member

  #1
  Feb 7, 2012
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 331
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mussa Juma na
  Peter Saramba, Arusha
  JAJI wa Mahakama Kuu, Aloyce Mujulizi jana alijitoa kusikiliza kesi ya kupinga ushindi wa Mbunge wa Jimbo la Arusha mjini ,Godbless Lema (Chadema) baada ya upande wa utetezi kuwasilisha notisi ya kutokuwa na imani naye kutokana na Kampuni ya Uwakili ya Imma aliyokuwa akifanya kazi , kutuhumiwa na ufisadi kwa kusaidia kuchotwa fedha Benki Kuu (BOT) fedha ambazo zilidaiwa kusaidia ushindi wa CCM mwaka 2005.

  Wakili wa Lema, Method Kimomogoro, aliwasilisha notisi hiyo ya kuendelea kutokuwa na imani na jaji huyo Januari 31 mwaka huu na jana, aliendelea kusisitiza kuwa mteja wake (Lema) hana imani na Jaji huyo kwani chama chake cha Chadema kilishiriki kuituhumu kampuni ya Imma kwa kusaidia Kampuni ya Deep Green Ltd kuchota fedha BOT.

  “Kwa kuwa maneno haya yalitamkwa na Chadema na yalitolewa pia bungeni na Kampuni ya Imma haikuwahi kukanusha kama ni kweli au la, mteja wangu anaamini, wewe wakati huo ulikuwa mmoja ya wanahisa katika kampuni hiyo, hivyo anahofu hautamtendea haki katika kesi hii hivyo tunaomba kwa busara ujitoe,” alisema Kimomogoro.

  Alisema mteja wake yupo tayari kutoa ushahidi juu ya kutuhumiwa kampuni ya Imma, kuhusika na ufisadi huo ambao ulielezwa fedha zake hizo ndizo ambazo zilisaidia ushindi wa CCM mwaka 2005.

  Jaji Mujulizi alitangaza uamuzi wa kujitoa baada ya mawakili wa pande zote kutoa hoja zao kwa zaidi ya saa mbili huku wakili wa utetezi, Alute Mungwai, akieleza kupinga notisi hiyo ya kutokuwa na imani na jaji kwa maelezo imewasilishwa kinyume cha sheria, haina ukweli, imejaa majungu, inashusha heshma na hadhi ya mahakama na jaji huyo kwani tuhuma za Imma hazijathibitishwa

  Jaji
  Akitoa uamuzi wake, Jaji Mujulizi alisema anachukua uamuzi wa kujitoa kwa kuzingatia heshima na maslahi ya haki hasa kutokana na mlalamikiwa kueleza kutokuwa na imani naye.

  Jaji Mujulizi alisema amechukua uamuzi huo pia ili kuhakikisha kesi hiyo isiendelee kupigwa danadana na lazima ifike kikomo kwani ushahidi unaonyesha upande wa walalamikiwa una lengo la kuchelewesha kesi hiyo.

  Akinukuu kesi mbalimbali zilizowahi kufikiwa uamuzi kama huo, Jaji Mujulizi alisema kimsingi shauri lililopo mbele yake linahusiana na kesi ya uchaguzi ambayo inapangiwa muda maalumu kumalizika na sasa imebaki miezi minne pekee kufikia mwisho.

  “Notisi iliyowasilishwa kuwa hawana imani na mimi , imekiuka kila aina ya utaratibu na ni dhahiri wanachokifanya ni kuchelewesha tu usikilizaji wa kesi hii”, alisema Jaji Mujulizi.

  Hata hivyo, Jaji Mujulizi alitoa siku tano kwa Lema kuwasilisha mahakamani hapo na nakala kumpatia yeye ambapo pia alisema maelezo ya kutokuwa na imani naye, yanatilia shaka uwezo wake na mahakama hiyo, wanapaswa Chadema kuleta mahakamani tuhuma hizo kuwa Kampuni ya Imma ilihusika na fedha za EPA ndani ya siku tano.

  Alisema pia chadema wanaweza kuchukua hatua za kikatiba kuwasilisha maombi rasmi kwa Rais Jakaya Kikwete aunde tume kuchunguza sakata hilo na pia kama yeye hastahili kukalia ofisi ya jaji na wafanye hivyo kwa kuzingatia Katiba.

  “Hatuwezi kukaa kila mtu akae na kuchafua wengine kwa kurudia rudia na hadi kuamini kuwa ni ukweli,” alisema Jaji Mujulizi.

  Awali, Wakili Mungwai alitoa hoja mbali mbali za kisheria kupinga notisi ya kumtaka jaji huyo kutojitoa na kueleza kuwa kama akikubali kujitoa itaonyesha amekubali kuhusika na tuhuma za ufisadi na hivyo itaathiri heshima na hadhi yake na mahakama kwa ujumla.  Lema atamba
  Mara baada ya uamuzi huo, nje ya Mahakama akizungumza na waandishi wa habari, Lema alisema ndani ya siku tano watawasilisha ushahidi wa tuhuma zao bila ya matatizo.

  “Tuna ushahidi wa kutosha juu ya kampuni ya ImmaAdvocate na hatuna shaka juu ya hili”, alisema Lema.

  Wafuasi wachache wa Chadema ambao jana walifika mahakamani, walipokea uamuzi ya Jaji Mujulizi kwa shangwe na mmoja nusura ajikute akitiwa nguvuni baada ya kupiga makofi mahakamani mara baada ya jaji kusema anajitoa.
  :lol:
   
 2. k

  kyoga Member

  #2
  Feb 7, 2012
  Joined: Sep 16, 2011
  Messages: 31
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  mambo naona sasa yameiva , ninauhakika usahahidi utatolewa lakini watautia kapuni kama spika alivyo fanya kwa swala la Lema na Lisu
   
 3. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #3
  Feb 7, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Je ushahidi ukitolewa Mujulizi atakuwa tayari kuuweka hadharani na kukiri kuwa kweli alihusika kuiba jasho la watanzania?
   
 4. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #4
  Feb 7, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 548
  Trophy Points: 280
  Du: sasa nazidi kuamini kwamba hauwezi kukimbia kivuli chako.
   
 5. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #5
  Feb 7, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Mkubwa!

  Mambo iko hapao sasa.
   
 6. s

  sanjo JF-Expert Member

  #6
  Feb 7, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Siku inakuja hata sehemu ya kujificha itakosekana kwa wale walioifisadi nchi hii.
   
 7. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #7
  Feb 7, 2012
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Shukrani Mheshimiwa Lema na Method Kimomogoro kwa kuweka mambo wazi. Vinginevyo, tungetembea katika lindi la giza.
   
 8. K

  KAMANDA HANGA Senior Member

  #8
  Feb 7, 2012
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 158
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wana cdm na wapenzi wake wote ondoeni shaka kwani ushaidi upo na huu ndo mwanzo wa ufunguzi wa mashtaka ya uhakika juu ya yule bwana alipata suport ya immma katika wizi huo; cdm ina watu makini hawasemi bila ushahidi ndg zangu. Saa ya ukombozi ni sasa.
   
 9. M

  Mbonafingi Senior Member

  #9
  Feb 7, 2012
  Joined: Apr 24, 2009
  Messages: 126
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mshahara wa dhambi ni mauti. Ujaji alipewa kulipa fadhila maana fedha za EPA ndizo zilizomuingiza Jk madarakani. Katiba mpya ilete suluhisho la hili. Raisi apunguziwe madaraka hasa ya kuteua watu tumechoka.
   
 10. Idimulwa

  Idimulwa JF-Expert Member

  #10
  Feb 7, 2012
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 3,384
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kimomogoro+Tundu Lisu=HAKI
   
 11. Godlisten Masawe

  Godlisten Masawe Verified User

  #11
  Feb 7, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 739
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kimomogoro ni mtu makini sana huyu, kesi zote zinazohusu chadema na viongozi Arusha yeye ndio anazisimamia. Ana waendesha puta mawakili wa serikali.
   
 12. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #12
  Feb 7, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Mussa Juma na
  Peter Saramba, Arusha
  JAJI wa Mahakama Kuu, Aloyce Mujulizi jana alijitoa kusikiliza kesi ya kupinga ushindi wa Mbunge wa Jimbo la Arusha mjini ,Godbless Lema (Chadema) baada ya upande wa utetezi kuwasilisha notisi ya kutokuwa na imani naye kutokana na Kampuni ya Uwakili ya Imma aliyokuwa akifanya kazi , kutuhumiwa na ufisadi kwa kusaidia kuchotwa fedha Benki Kuu (BOT) fedha ambazo zilidaiwa kusaidia ushindi wa CCM mwaka 2005.

  Wakili wa Lema, Method Kimomogoro, aliwasilisha notisi hiyo ya kuendelea kutokuwa na imani na jaji huyo Januari 31 mwaka huu na jana, aliendelea kusisitiza kuwa mteja wake (Lema) hana imani na Jaji huyo kwani chama chake cha Chadema kilishiriki kuituhumu kampuni ya Imma kwa kusaidia Kampuni ya Deep Green Ltd kuchota fedha BOT.

  “Kwa kuwa maneno haya yalitamkwa na Chadema na yalitolewa pia bungeni na Kampuni ya Imma haikuwahi kukanusha kama ni kweli au la, mteja wangu anaamini, wewe wakati huo ulikuwa mmoja ya wanahisa katika kampuni hiyo, hivyo anahofu hautamtendea haki katika kesi hii hivyo tunaomba kwa busara ujitoe,” alisema Kimomogoro.

  Alisema mteja wake yupo tayari kutoa ushahidi juu ya kutuhumiwa kampuni ya Imma, kuhusika na ufisadi huo ambao ulielezwa fedha zake hizo ndizo ambazo zilisaidia ushindi wa CCM mwaka 2005.

  Jaji Mujulizi alitangaza uamuzi wa kujitoa baada ya mawakili wa pande zote kutoa hoja zao kwa zaidi ya saa mbili huku wakili wa utetezi, Alute Mungwai, akieleza kupinga notisi hiyo ya kutokuwa na imani na jaji kwa maelezo imewasilishwa kinyume cha sheria, haina ukweli, imejaa majungu, inashusha heshma na hadhi ya mahakama na jaji huyo kwani tuhuma za Imma hazijathibitishwa

  Jaji
  Akitoa uamuzi wake, Jaji Mujulizi alisema anachukua uamuzi wa kujitoa kwa kuzingatia heshima na maslahi ya haki hasa kutokana na mlalamikiwa kueleza kutokuwa na imani naye.

  Jaji Mujulizi alisema amechukua uamuzi huo pia ili kuhakikisha kesi hiyo isiendelee kupigwa danadana na lazima ifike kikomo kwani ushahidi unaonyesha upande wa walalamikiwa una lengo la kuchelewesha kesi hiyo.

  Akinukuu kesi mbalimbali zilizowahi kufikiwa uamuzi kama huo, Jaji Mujulizi alisema kimsingi shauri lililopo mbele yake linahusiana na kesi ya uchaguzi ambayo inapangiwa muda maalumu kumalizika na sasa imebaki miezi minne pekee kufikia mwisho.

  “Notisi iliyowasilishwa kuwa hawana imani na mimi , imekiuka kila aina ya utaratibu na ni dhahiri wanachokifanya ni kuchelewesha tu usikilizaji wa kesi hii”, alisema Jaji Mujulizi.

  Hata hivyo, Jaji Mujulizi alitoa siku tano kwa Lema kuwasilisha mahakamani hapo na nakala kumpatia yeye ambapo pia alisema maelezo ya kutokuwa na imani naye, yanatilia shaka uwezo wake na mahakama hiyo, wanapaswa Chadema kuleta mahakamani tuhuma hizo kuwa Kampuni ya Imma ilihusika na fedha za EPA ndani ya siku tano.

  Alisema pia chadema wanaweza kuchukua hatua za kikatiba kuwasilisha maombi rasmi kwa Rais Jakaya Kikwete aunde tume kuchunguza sakata hilo na pia kama yeye hastahili kukalia ofisi ya jaji na wafanye hivyo kwa kuzingatia Katiba.

  “Hatuwezi kukaa kila mtu akae na kuchafua wengine kwa kurudia rudia na hadi kuamini kuwa ni ukweli,” alisema Jaji Mujulizi.

  Awali, Wakili Mungwai alitoa hoja mbali mbali za kisheria kupinga notisi ya kumtaka jaji huyo kutojitoa na kueleza kuwa kama akikubali kujitoa itaonyesha amekubali kuhusika na tuhuma za ufisadi na hivyo itaathiri heshima na hadhi yake na mahakama kwa ujumla.  Lema atamba
  Mara baada ya uamuzi huo, nje ya Mahakama akizungumza na waandishi wa habari, Lema alisema ndani ya siku tano watawasilisha ushahidi wa tuhuma zao bila ya matatizo.

  “Tuna ushahidi wa kutosha juu ya kampuni ya ImmaAdvocate na hatuna shaka juu ya hili”, alisema Lema.

  Wafuasi wachache wa Chadema ambao jana walifika mahakamani, walipokea uamuzi ya Jaji Mujulizi kwa shangwe na mmoja nusura ajikute akitiwa nguvuni baada ya kupiga makofi mahakamani mara baada ya jaji kusema anajitoa.

  Source:Mwananchi.
   
 13. M

  Mokerema JF-Expert Member

  #13
  Feb 7, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 236
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jakaya kumteua Alyoce kuwa Jaji ni kichekesho cha mwaka. Ni ukweli mtupu kwamba akina Masha na Mujulizi walianzisha Kampuni ya Deep Green na pia ndiyo waliifilisi baada ya kuchota 10 billion za EPA. Then huu ni uhuni na uzumbukuku wa **** Kalulu hii inachefua?
   
 14. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #14
  Feb 7, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Wanajamvi.

  Maoni yangu kuhusiana na hii kesi yatafuata baadae.

  Karibuni nasubiri maoni yenu kwa hamu kubwa.
   
 15. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #15
  Feb 7, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,671
  Trophy Points: 280
  Hakuna kosa kubwa alilofanya Lema, kama kumkataa Jaji wa Mahakama Kuu, Aloyce Mujulizi.

  Lema, na wakili wake Method Kimomogoro, sijui watasemaje Jaji mpya akitoa hukumu kuwa Lema, kashindwa kesi nadhani itakuwa hakuna sababu yoyote ya kulalamika..

  Kesi hiyo haina muda mrefu itakuwa imekwisha bado miezi minne tu tutajua yetu macho na masikio.
   
 16. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #16
  Feb 7, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Na Saed Kubenea

  MTOTO wa Rais Jakaya Kikwete anafanya kazi katika kampuni iliyoshiriki kusajili kampuni ya Deep Green Finance Ltd., ambayo ilikwapua mabilioni ya shilingi kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

  MwanaHALISI linazo taarifa kwamba kampuni ya mawakili ya IMMA Advocates and Co. ya Dar es Salaam ndiyo ilisadia usajili wa Deep Green Finance Ltd iliyochota Sh. 8 bilioni kutoka BoT.

  Hakuna maelezo yoyote yaliyowahi kutolewa kueleza kwa nini Deep Green Finance Limited ililipwa mabilioni hayo na BoT wakati wa uongozi wa gavana Daudi Billali ambaye Rais Jakaya Kikwete alifukuza kazi miezi miwili iliyopita.

  Mtoto wa rais, ambaye anafanya kazi katika kampuni iliyosaidia kusajili Deep Green Finance Ltd., ni Ridhwani Kikwete.

  Deep Green Finance Limited ilichota fedha hizo kati ya Septemba na Desemba 2005 wakati wa mchakato kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2005.

  IMMA inasimamia majina ya wamiliki wa kampuni hiyo ya mawakili ambao ni Protase Ishengoma, Lawrence Masha, Aloysius Mujulizi na Sadock Magai.

  Mmoja wa wamiliki wa kampuni hiyo, Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha aliithibitishia MwanaHALISI kwamba ni mwanzilishi na mmiliki wa IMMA.

  Hata hivyo aliharakisha kusema kwamba kwa sasa amekabidhi majukumu yake kwa wakurugenzi wake wengine baada ya kuchukua wadhifa serikalini.

  “Ni kweli kwamba mimi ni mmoja wa wakurugenzi waanzilishi wa IMMA, lakini kwa sasa siko huko. Nimeacha kujishughulisha na shughuli za kampuni hiyo tangu mwaka 2005 nilipoingia serikalini,” alisema Masha.

  Aidha, Masha alithibitisha pia kwamba kampuni ya IMMA ndiyo iliyosajili kampuni ya Deep Green Finance Limited na kwamba ni kweli kuwa inamwajiri Ridhwan.

  Hata hivyo, Masha amesema mwenye nafasi nzuri zaidi ya kuzungumzia masuala ya IMMA hivi sasa ni mkurugenzi mwendeshaji, Protase Ishengoma.

  Ridhwani alifanya kazi katika kampuni hiyo ya uwakili akiwa bado kwenye mafunzo mara baada ya kupata shahada yake ya sheria kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

  Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye amezungumza kwa sharti la kutotajwa jina ameliambia MwanaHALISI, “Tuombe kusipatikane ushahidi wa moja kwa moja kati ya IMMA na mafisadi; vinginevyo hadhi ya rais wetu itaathirika vibaya sana.”

  Wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, kipindi mabilioni ya shilingi yalipokwapuliwa na Deep Green Finance Limited iliyoanzishwa kwa msaada wa IMMA, Ridhwani alikuwa tayari anafanya kazi katika kampuni ya mawakili.

  Masha amethibitisha kuwa Ridhwani bado anafanya kazi kwenye kampuni hiyo hadi sasa.

  Ridhwani hakupatikana hadi tunakwenda mitamboni kujibu swali iwapo hana wasiwasi wa kufanya kazi katika kampuni inayotuhumiwa kuibia taifa.

  Kuhusu vigezo vya kuajiriwa, Masha amesema Ridhiwani alitimiza vigezo vyote na kwamba ana sifa zinazohitajika.

  Imefahamika pia kuwa Fatuma Karume, mtoto wa Rais wa Zanzibar, Abeid Amani Karume, anafanya kazi IMMA.

  Ni katika kampuni ya IMMA pia rais aliteua wakili Aloysius Mujulizi, ambaye ni mmoja wa wanahisa, kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.

  Hivi karibuni kumekuwa na minong’ono na tuhuma za chichini kuhusu kampuni iliyosaidia kusajili Deep Green Finance Limited ambako mtoto wa rais anafanya kazi na ambako rais ameteua wakili kuwa jaji na wakili mwingine kuwa waziri.

  Taarifa kutoka kwa Msajili wa Makampuni zinawataja watu wawili, Protase Ishengoma na Stella Ndikimi kuwa wakurugenzi waanzilishi wa Deep Green Finance Limited.

  Ishengoma alithibitisha katika mahojiano yake na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu juzi Jumatatu, kwamba alishiriki kusajili Deep Green Finance Limited.

  Kampuni ya Deep Green ilifilisiwa mwaka 2006, kabla ya kufikisha hata mwaka moja wa uhai wake, katika kile wachunguzi wa mambo wanasema, “baada ya kukidhi matakwa na matarajio yake.”

  Hadi sasa haijafahamika Sh. 8 bilioni zilizochotwa zilichukuliwa ili zifanye kazi gani na wapi.

  Wakili Ishengoma alikiri pia kuwa ni yeye aliyeteuliwa kuifilisi kampuni aliyoanzisha.

  MwanaHALISI ina ushahidi wa malipo kutoka Deep Green Finance Limited kwenda IMMA ingawa haikufahamika ilikuwa kwa kazi gani; kama vile ambavyo malipo kutoka BoT kwenda Deep Green hayajapatiwa maelezo hadi sasa.

  Taarifa za ukwapuaji mabilioni ya shilingi kutoka BoT ziliwahi kuanikwa na kundi la wanasiasa likiongozwa na Mbunge wa Karatu, Dk. Willibrod Slaa siku lilipotangaza “orodha ya mafisadi” kwenye viwanja vya Mwembeyanga jijini Dar es Salaamn mwaka jana.

  Kutopatikana maelezo halisi juu ya kazi ya Deep Green Finance Limited; maelezo kuhusu matumizi ya mabilioni yaliyochukuliwa benki na sababu za kufilisiwa haraka kwa kampuni hiyo, vinamweka mtoto wa rais karibu na lawama na tuhuma lukuki.

  Shutuma na tuhuma, za chinichini na za wazi zinatokana na matukio makuu yafuatayo:

  Kwanza, IMMA ndio walirahisisha usajili wa kampuni ya Deep Green Finance Limited iliyokwapua mabilioni ya shilingi kutoka benki kuu.

  Pili, baadhi ya wakurugenzi wa IMMA ndio walikuwa waanzilishi wa Deep Green Finance Limited inayotuhumiwa kufanya ufisadi.

  Tatu, kampuni ya mawakili waliohusika katika shughuli zinazotiliwa mashaka, ndiyo imepata “ngekewa” ya mawakili wake kuteuliwa, mmoja kuwa jaji na mwingine kuwa waziri.

  Nne, ni kampuni hiyohiyo ambayo inamwajiri mtoto wa Rais wa Jamhuri ya Muungano na mtoto wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Hata kama malalamiko hayana msingi, mlolongo huo unastua watazamaji.

  Deep Green inadaiwa kuwa na uhusiano wa karibu na makampuni ya Meremeta Gold Limited na Tangold Limited. Meremeta ambayo nayo imefilisiwa. Ndiyo ilikuwa ikiendesha mgodi wa dhahabu wa Buhemba ulioko mkoani Mara. Tangold ndiyo ilirithi mali za Meremeta.

  Makampuni yote yalichota mabilioni ya shilingi nchini na kutokomea.

  Deep Green Finance Limited ambayo wakurugenzi wake wote watatu wanatajwa kuwa raia wa nje, Mark Ross Weston (New Zealand), Anton Taljaard na Rudolph van Schalkwyk wa Afrika Kusini), ilichotewa fedha hizo katika kipindi ambacho taifa hili lilikuwa katika hekaheka za uchaguzi mkuu mwaka 2005.

  Baada ya kujineemesha kwa mabilioni ya shilingi kutoka BoT, Deep Green Finance Limited iliamua, Aprili mwaka jana, kujifilisi na kuteua kampuni ya Protase Rwezahura Gervas Ishengoma (IMMA) kuwa mfilisi kuanzia Julai 27 mwaka jana.

  Waziri Masha, mmoja wa wamiliki wa IMMA, aligombea ubunge mwaka 2005 katika jimbo la Nyamagana, mkoani Mwanza na kushinda. Rais alimteua kuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini kabla ya kumhamishia Wizara ya Mambo ya Ndani kwa nafasi ya unaibu wakati wa mlipuko wa kwanza wa sakata la Richmond.

  Katika mabadiliko makubwa ya baraza la mawaziri ya hivi karibuni, ambapo Wizara ya Usalama wa Raia na ile ya Mambo ya Ndani ziliunganishwa kama zamani, Masha aliteuliwa kuwa waziri kamili wa wizara hiyo.

  Kama itathibitika kuwepo mahusiano ya kifisadi kati ya IMMA na Deep Green Finance Limited; wakati huohuo mtoto wa rais akiwa na ajira katika kampuni ambamo tayari rais ameteua mawakili kwa kazi za uwaziri na ujaji, hadhi ya rais inaweza kuwa mashakani.

  Mwisho

  [​IMG]
   
 17. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #17
  Feb 7, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  ETI HUYU MUJULIZI anataka ushahidi. Sasa huu hapa.[FONT=&quot]Kwanza[/FONT][FONT=&quot], IMMA ndio walirahisisha usajili wa kampuni ya Deep Green Finance Limited iliyokwapua mabilioni ya shilingi kutoka benki kuu.

  Pili, baadhi ya wakurugenzi wa IMMA ndio walikuwa waanzilishi wa Deep Green Finance Limited inayotuhumiwa kufanya ufisadi.

  Tatu, kampuni ya mawakili waliohusika katika shughuli zinazotiliwa mashaka, ndiyo imepata "ngekewa" ya mawakili wake kuteuliwa, mmoja kuwa jaji na mwingine kuwa waziri.
  [/FONT]
  [FONT=&quot]
  Nne, ni kampuni hiyohiyo ambayo inamwajiri mtoto wa Rais wa Jamhuri ya Muungano na mtoto wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Hata kama malalamiko hayana msingi, mlolongo huo unastua watazamaji.

  [/FONT]
   
 18. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #18
  Feb 7, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  kimebaki nini tena
   
 19. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #19
  Feb 7, 2012
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  lema anapambana na kesi zake tu!
   
 20. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #20
  Feb 7, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
   
Loading...