Jaji ahongwa mil 60 kesi ya uchaguzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jaji ahongwa mil 60 kesi ya uchaguzi

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by GAZETI, Feb 27, 2011.

 1. GAZETI

  GAZETI JF-Expert Member

  #1
  Feb 27, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 3,532
  Likes Received: 1,020
  Trophy Points: 280
  Uchaguzi umeisha lakini kuna kesi mbalimbali zimefunguliwa kupinga matokeo ya baadhi ya majimbo. Moja ya majimbo ambayo CCM ilitumia nguvu za wazi na kunyangÂ’anya ushindi (si Kuchakachua) ni jimbo la Tandahimba Mkoani Mtwara.


  Tar. 21. Feb. Zilipatikana taarifa kuwa MRATIBU WA TUME YA UCHAGUZI (W) Ndg. Peter Chuka alikabidhiwa Tsh. Milioni sitini ampatie Jaji anayesimamia kesi ya uchaguzi wa jimbo la Tandahimba ikiwa ni rushwa ili aweze kuhalalisha ubunge wa mbunge wa CCM Ndg. Juma Njwayo. Fedha hizo alikabidhiwa na Mkurugenzi H/W (Chanzo: Watu wa karibu wa Mratibu na baadhi ya watendaji wa Halmashauri ya Wilaya) Siku iliyofuata Bw. Chuka akaonekana na watu mbalimbali ambao walizipata tetesi hizo na kuamua kukaa maeneo ya barabara ya kuelekea Mtwara ili kupata uhakika. Siku hiyo ambayo ni Tar. 22 Feb. Ndg. Chuka alisafiri kwa gari la Idara ya Elimu ambalo ni maalum kwa ukaguzi wa shule za msingi. Hakuna mwenye uhakika kama hizo fedha zimepokelewa na Jaji au la! Ingawa baadhi ya wana CCM wamekuwa wakijigamba kuwa wamemaliza kazi.


  MAMBO YALIVYOKUA


  Baada ya matokeo kuonyesha kuwa mbunge wa upinzani Ndugu Katani Ahmad Katani ameshinda Baraza la usalama la wilaya lilikutana na kupendekeza kuwa asipewe ushindi mbunge huyo wa upinzani. Pendekezo hilo lilipingwa vikali na Kamanda wa taasisi ya kuzuia Rushwa wa wilaya Ndugu. Mtera ambaye kwa kuonyesha msimamo wake alitoka nje ya kikao na kuahidi kuwa kwa lolote litakalotokea yuko tayari kutoa ushahidi na kuwa mkweli kabisa. Baada ya mgombea ubunge wa CCM kutangazwa, ndani ya siku zisizozidi tano Ndugu Mtera akapewa uhamisho jambo lililotafsirika kuwa ni kuhofia kauli yake kwamba atatoa ushahidi wa ukweli. Kutangazwa kwa mbunge wa CCM kuliwashangaza hata wasimamizi wengine kwani mbunge huyo alikataliwa kwa kiwango ambacho kubadilisha matokeo ni kukaribisha umwagaji damu.


  YALIYOTOKEA BAADA YA MATOKEO KUTANGAZWA.


  1. Mbunge aliyeshinda kupigwa hadi kuvunjwa mkono akilazimishwa kusaini
  2. Mkuu wa wilaya kumuahidi Mbunge kuwa Rais atamteua kwenye nafasi nyingine iwapo atakubali
  3. Polisi kuzunguka mitaani na kupiga mabom ya machozi hovyo
  4. Wananchi kupigwa na kuishi maporini kwa siku kadhaa.
  5. Wananchi wenye hasira kuchoma moto baadhi ya nyumba za wana CCM (walioonekana kuwa na ushabiki mkubwa)

  KUFUNGULIWA KWA KESI


  Kesi ilianza kusikilizwa mwezi January ambapo upande TUME YA UCHAGUZI waliomba siku 21 ili waweze kupeleka vielelezo Mahakamani. Siku ya kesi ilipofika ambayo ni Tar. 17 Feb. 2011 Wakasema vielelezo viko Dar es salaam kwa Mwanasheria, Wakaomba muda tena wakapewa mpaka Tar 25 Feb. Wawe wamepeleka vielelezo hivyo.
  Hivyo ndivyo ilivyotokea.
   
 2. GAZETI

  GAZETI JF-Expert Member

  #2
  Feb 27, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 3,532
  Likes Received: 1,020
  Trophy Points: 280
  Mratibu wa TUME (W) amefanya mawasiliano na Waratibu kata elimu akitaka apewe Fom za B. 21 ambazo hazijaandikwa jambo linalohofiwa kuwa ni kutaka kutengeneza matokeo mengine ambayo si halali (Chanzo. Baadhi ya waratibu Elimu kata)
   
 3. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #3
  Feb 27, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Tanzania iko siku tutapigana nasiyo siku nyingi kama watanzania walala hoi wataendelea kunyang'anywa haki zao kwa ubabe naamini tukitwangana tutaheshimiana na tutaacha kuchezea haki za walala hoi na kutumia pesa zao kuwaangamiza....
  Kupigana ni neno ambalo watanzania wengi hawalipendi kulisikia lakini kwa mwendo huu watu hawawezi kuendelea kuvumilia.....
   
 4. M

  Mtu wa Mungu JF-Expert Member

  #4
  Mar 3, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 445
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Sisiemu wameyataka wenyewe; wimbi la pipooooooooos pawa imeanza kujengwa na CDM kuanzia kanda ya ziwa; na mkwere ameanza kuhofu!!!!!!!!!!!!!!! Sisiemu wajiandae tu kung'oka kwa nguvu ya umma kwa sababu ya kuzidi kwa vitendo vya dhuluma. Ya Tunisia , Misri na Libya hayakwepeki Tz kwa dhuluma hizi za sisiemu. Kule ni mtawala yule yule kwa miaka 40; Tz chama kile kile kwa miaka 50!!! Nyakati za waasisi mambo yalikuwa ahueni, lakini sasa nyakati hizi za sisiemu ya kizazi kipya cha sisiemu chini ya makamanda mafisadi ni dhuluma tupu!!!!!!!!!!!!!! Wa kuwaweza ni nguvu ya pipos tu-maana hata wafadhili wakishaona nguvu hiyo at work wanasimamisha misaada mara moja!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! PIPOOOOOOOOOOOOOOOSSSSSSSSSSSSSS!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! PAWAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 5. Silas Haki

  Silas Haki JF-Expert Member

  #5
  Mar 5, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 368
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Dawa ya hayo yote ni kubadili katiba ili itoe nguvu kwa wananchi ya kuwaajibisha viongozi wabovu. Wakati ndo huu wa kufanya mabadiliko ya mfumo wote wa uchaguzi na serikali kwa ujumla
   
 6. minda

  minda JF-Expert Member

  #6
  Mar 8, 2011
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 1,070
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  nilidhani fitna za uchaguzi zimeisha. kumbe bado.
  nchi hii kuna mambo ya ajabu yanafanyika lakini watanzania hawajui kabisa. inasikitisha. asante sana mkuu; huu ni mchango mwingine kwamba nec sio huru kama inavyodhaniwa.
   
Loading...