Mimi sikupangwa kwenye kikosi. Sasa wachambuzi wa soka wanaposema kiungo fulani amezunguka kilometa kadhaa ndani ya dakika tisini, nao ni umbea? Hakuna umbea hapo, soka ni mchezo unaochezwa hadharani, kila mtu anayeweza kushuhudia atashuhudia tu!Umbea tu ww umepiga mangapi
Salute kwako mkuu kwa kuongea kimpira inaonekana wewe ni mfuatiliaji wa soka sio Jabulani yeye atakuwa mfuatiaji wa netball...Cha kuangalia ni nafasi ngapi zilitengenezwa. Inajulikana Jaja ni mmaliziaji mzuri, je wale wa kumtengenezea walitengeneza nafasi ngapi? na huyo kiiza baada ya kuingia, alizitengeneza hizo nafasi mwenyewe?
BTW mi ni mnyama.
Mshambuliaji ghali wa Yanga, Mbrazili, Geilson Santos Jaja, juzi Jumamosi alicheza mchezo wake wa nne wa Ligi Kuu Bara alipokutana na Simba kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, lakini alishindwa kuisaidia timu yake baada ya kupiga shuti moja tu langoni.
Jaja aliyesajiliwa na Yanga akitokea nchini Brazil ambapo analipwa mshahara wa dola 3,000 kwa mwezi (zaidi ya shilingi milioni nne za Kitanzania), alipiga shuti hilo dakika ya 73 akiunganisha pasi aliyopewa na beki wa kushoto wa timu hiyo, Oscar Joshua.
Straika huyo mwenye mwili uliojengeka kimazoezi, alicheza mchezo huo kwa dakika 82 na kulazimika kwenda benchi kumpisha Mganda, Hamisi Kiiza Diego ambapo mpaka anatoka alifanikiwa kupiga mipira sita ya vichwa huku vichwa viwili vikiwa fyongo.
cc: mkolaj, Makoye Matale, Ududu, bujashi25, Balantanda
Cha kuangalia ni nafasi ngapi zilitengenezwa. Inajulikana Jaja ni mmaliziaji mzuri, je wale wa kumtengenezea walitengeneza nafasi ngapi? na huyo kiiza baada ya kuingia, alizitengeneza hizo nafasi mwenyewe?
BTW mi ni mnyama.