FT: CAF Champions League: Simba SC 1-0 Wydad AC.. Mkapa Stadium.. Dar.. 22.4.2023

Pettymagambo

JF-Expert Member
Aug 21, 2017
1,414
7,898
Hayawi hayawi sasa yamekuwa, ile game ngumu na ambayo inafuatiliwa kwa ukaribu sana na watu wote wapenda soccer la africa, game ya robo final ya caf champions league baina ya miamba kwelikweli, timu zenye misuli ya kutosha, Simba sports club vs Wydad athletic club. Ni palepale machinjioni ambapo yeyote akitia maguu pale, hutoka vichwa chini miguu juu.

Hakika mnyama anaitaka hii mechi na hayupo tayari kuona anagota robo final pekee.

Wachezaji mahiri wa mnyama wote watakuwepo kutupa raha watz wote na bila shaka leo kila mtu ataishabikia
simba sports club.
Wanalunyasi.
Taifa kubwa.
Samba loketo.
Mwana kulitaka.
Mwana kulipata.
Wazee wa kidedea.

Timu iliyobarikiwa na MUNGU na inayosakata kabumbu lililothibitishwa na caf na kufurahiwa vilivyo na fifa mpaka kupelekea sikukuu ya eid icheleweshwe hapa nchini kwetu pekee ili kuingoja mechi hii ya kibabe.

Nikuanzia saa 10:00 jioni, tuwe wote mwanzo mpaka mwisho kwa updates zote.

Eid mubarakh

Simba kikosi.jpg

Mchezo umeanza
5' Mchezo umeanza kwa kasi
10' Simba wanajaribu kujipanga kushambulia lakini wapinzani wapo makini
18' Zimbwe Jr anapata nafasi lakini krosi yake inapaa juu ya lango
21' Beki wa Simba anapata kadi ya njano kwa kucheza faulo
22' Wydad wanapata kona ya pili
24' Wageni wanapata kona ya nne
24' Wydad wanapata kona ya tano
GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
31' Baleke anafunga baada ya kutokea faulo langoni kwa wapinzani
38' Mvua imeanza kunyesha, mashabiki wa Simba wanashangilia kwa nguvu
40' Mchezo unasimamishwa kutokana na moyo uwanjani
42' Mchezo umeendelea
45' Zinaongezwa dakika 2
MAPUMZIKO

Kipindi cha pili kimeanza

46' Chama anapiga shuti kali linatoka nje kidogo ya lango
47' VAR, Mwamuzi anafuatilia VAR kaujua kama Baleke alichezewa faulo, anabaini haikuwa faulo
59' Wyad wanaonekana kuchangamka na kufanya mashambulizi
65' Timu zote zinashambuliana kwa zamu
67' Kibu Denis anapiga shuti kipa anadaka
74' Kibu anapiga shuti linatoka nje kidogo ya lango
76' Wydad wanaendelea kuongeza presha kwa kutafuta goli
80' Sakho anaingia anatoka Saido
87' Mchezo unaendelea, mashambulizi ni ya kupokezana
88' Mabadiliko kwa Simba, anatoka Baleke anaingia John Bocco
90' Mashabiki wa Wydad wanaendelea kushangilia licha ya kuwa nyuma
Zinaongezwa dakika 4 za nyongeza

Full time
 
Oyaaaa📢📢📢
Mnyama nakuaminia, leo afe beki, age kiungo uwanjani, mapafu yafunguke kama ya farasi🐎🐎uwanjani. Muhakikishe on targets⚽⚽⚽ za kutosha kwenye lango la waarabu hawa wa kaskazini magharibi mwa Afrika. Taifa lote macho kwenu leo, msituangusheee🇹🇿♥️🇹🇿
SIMBAAAAAAA NGUVU MOJAAAAAAA
 
Hayawi hayawi sasa yamekuwa, ile game ngumu na ambayo inafuatiliwa kwa ukaribu sana na watu wote wapenda soccer la africa, game ya robo final ya caf champions league baina ya miamba kwelikweli, timu zenye misuli ya kutosha,
Simba sports club
vs
Wydad athletic club
Ni palepale machinjioni ambapo yeyote akitia maguu pale, hutoka vichwa chini miguu juug

Hakika mnyama anaitaka hii mechi na hayupo tayari kuona anagota robo final pekee.
Wachezaji mahiri wa mnyama wote watakuwepo kutupa raha watz wote na bila shaka leo kila mtu ataishabikia
simba sports club.
Wanalunyasi.
Taifa kubwa.
Samba loketo.
Mwana kulitaka.
Mwana kulipata.
Wazee wa kidedea.
Timu iliyobarikiwa na MUNGU na inayosakata kabumbu lililothibitishwa na caf na kufurahiwa vilivyo na fifa mpaka kupelekea sikukuu ya eid icheleweshwe hapa nchini kwetu pekee ili kuingoja mechi hii ya kibabe.
Nikuanzia saa 10:00 jioni, tuwe wote mwanzo mpaka mwisho kwa updates zote.
Eid mubarakh
SIMBA GUVU MOYA 🦁
Ila we jamaa unafaa kua promota😂😂🤣😂🤣😂😂🤣🤣
 
41 Reactions
Reply
Back
Top Bottom