Jaffo: Hakuna kitu muhimu kwa binadamu kama familia yake hivyo nawaasa Wananchi lindeni Amani

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,932
141,896
Serikali imewataka viongozi wa dini kuhubiri amani bila kuchoka wakati huu tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu.

Waziri wa Tamisemi mh Jaffo akizungumza na viongozi wa BAKWATA jijini Dodoma amesema hakuna kitu muhimu kwa binadamu kama familia yake hivyo amewaasa wananchi kuizingatia Amani kwasababu Amani haina mbadala.

Source ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
 
Hamjui anayeweka amani rehani?

Hajui amani inatokana na haki?

Mataga mwaka huu mtataga sana tu.
 
Muulizeni huyu mzaramo anahubiri amani ipi juzi tumeona uvunjifu wa amani huko Ruangwa,Morogoro,Lindi kwa nape sijui anataka amani gani
 
Muulizeni huyu mzaramo anahubiri amani ipi juzi tumeona uvunjifu wa amani huko Ruangwa,Morogoro,Lindi kwa nape sijui anataka amani gani
Mtu yeyote anayehubiri amani wakati huu ni mnafiki mkubwa. Mtu kaja nyumbani kwako kaiba ngombe zako halafu anakwenda hadharani kudai amani. Kama kweli wanataka amani wawarudishe wagombea wote waliowaengua kwa sababu yoyote, tufanye uchaguzi huru na wa haki, anayeshinda kwa halali na haki atangazwe kuwa mshindi. Lakini watu wamenyanganywa fomu wakati wanarudisha, wamekamatwa na polisi, wameenguliwa kwa maelekezo toka juu halafu mnataka tutangaze poooo! Thubutu!
 
Tulinde amani ili yeye azidi kushiba bila bughuda siyo?
EgAHm5WWoAEKSjs.jpg
 
Back
Top Bottom