Mkuu rombo
JF-Expert Member
- Oct 18, 2012
- 1,556
- 422
mkuuu wa nchi sijui kama atakwenda kutowa salamu za rambi rambi atadai amechoka na safari ya dodoma anaitaji kupumzika
MUNGU akurehemu upumzike kwa amani
MUNGU akurehemu upumzike kwa amani
Mzee huyu alikuwa ni miongoni mwa viongozi wachache wa CCM waliotumikia taifa lao kwa uadilifu na kwa uzalendo wa hali ya juu, akiwa waziri wa serikali kwa miaka 25 mfululizo (1975 - 2000), lakini hakuna mahali alitumia vibaya madaraka yake kwani inasemekana kwamba hata nyumba ya kuishi nje kidogo ya jiji la Dar-es-salaam alijengewa na wanae kabla ya kustaafu na hata hivyo haikukamilika ipasavyo; na katika kipindi karibia chote cha ustaafu wake alikuwa anaishi kwao kijijini;
Lakini kwa vile serikali yetu ya CCM haijali watu kama hawa, msiba wake utaendeshwa kinafiki tu; Misiba yenye kupewa uzito ni ile ya viongozi wasiokuwa wazalendo ambao utashi wao unapimwa kwa utajiri wao; Lakini ipo siku yote haya yatabadilika;
Poleni wafiwa; Mwenyezi mungu amlaze mahali pema peponi Mzee wetu Makweta, Amen;
Mkuu hapo kwenye Red sidhani kama unaongea sawa! Jee, mazishi ya Mwalimu Nyerere hayakupewa uzito unaostahili? jee, vipi mazishi ya Sokoine, Kawawa, Mzee Rupia, Bibi Titi, nk? jee, hawa viongozi hawakuwa Wazalendo? kama jibu lako ni ndio basi utakuwa Mtanzania wa kwanza kuwatuhumu viongozi hawa kwa utovu wa uzalendo!
Vinginevyo nakuomba ukanushe kauli yako na kuwaomba msamaha familia ya wazalendo hawa!
R. I. P Makweta umelitumikia taifa lakini mchango wako haujatambulika mpaka wameshindwa kukupeleka lndia.