Jack Ma awa tajiri namba moja nchini China.

Jack Ma awa tajiri namba moja nchini China.

Joined
Jun 3, 2014
Posts
28
Reaction score
16
​

Mwenyekiti mtendaji wa makampuni ya Alibaba, Jack Ma, sasa ndio tajiri nambari moja nchini China.
Bwana Ma mwenye umri wa miaka 49, amepiga hatua hiyo baada ya kundi la makampuni yake ya Alibaba kuorodheshwa kwenye soko la hisa la New York (NYSE).
Makapuni chini ya kundi la Alibaba yanashughulika na biashara mbali mbali za mtandaoni (e-commerce) nchini china. Mojawapo ya biashara zake ni soko la mtandao Alibaba.com ambalo linaunganisha wauza bidhaa wakubwa wa china na wanunuzi dunia nzima, mfumo wa malipo wa Alipay ambao unashabihiana na mfumo maarufu wa PayPal, pamoja na soko la bidhaa kati ya mtu na mtu, Taobao, soko ambalo mafanikio yake yalisababisha kampuni ya marekani Ebay inayofanya shughuli kama hiyo, kuamua kufunga tawi lake nchini China mwaka 2006 kutokana na kuzidiwa kibiashara na Taobao.
Mabilionea wengine wa sekta ya teknolojia nchini china wanaomfuatia Bwana Jack Ma, ni Pony Ma wa kampuni ya mawasiliano ya Tencent pamoja na Robin Li wa search engine Baidu.

source: Jack Ma awa tajiri namba moja nchini china.
 
mbona nilijua hivi muda mrefu sana,mpaka nikiwa nasoma kichwa cha habari leo nikajua kawa no 1 duniani[emoji1787][emoji1787]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom