Iwepo siku ya Philosphers wa Tanzania

Nikupateje

JF-Expert Member
Dec 22, 2009
1,334
988
Waheshimiwa,

Nadhani tunapomuenzi Julius Nyerere basi kisiasa hatuwezi kupishana na hilo. Lakini tupomuenzi kwa fikra ndipo hapo tunapofanya makosa. Kwa sababu kama ni fikra basi sifa ye kuenziwa fikra zako ni kuitwa wewe Philosopher.

Na kama ni hivyo basi, philosopher hakuwa yeye tu hapa Tanzania. Mitizamo yake zimo kwenye vitabu vyake kama zilivyo fikra za wenzake kwenye vitabu vyao.

Nimetumia neno mitizamo yake. Ningekuwa na uhakika ningejiunga na wale wengi walisema zidumu fikra zake. Kwangu hoja si kudumu au hata kuishi kwa fikra zake kwa muda gani. Kwangu hoja ni kwamba je zilikuwa au zake au za wengine.

Najiuliza hivi kwa sababu Nyerere angekuw hasomi hata kitabu kimoja basi hakika ningesema ni fikra zake. Lakini naambiwa kwamba ile maktaba yake pale Butiama ina vitabu zaidi ya 8,000. Yeye mwenyewe aliwahi kukiri kuwa utajiri wake ni vitabu. Kuwa na vitabu vingi maana yake una fikra za watu wengi, unasoma fikra zao.

Maadamu hatujui kuwa ni sehemu gani za hotuba au mandishi yake ilijazwa na hayo aliyosoma sasa tutasemaje tuzienzi fikra zake.

Hivyo ninaomba tujadili umuhimu wa kuwa na Tanzanian Philosophers Day. Kwamba siku hiyo au wiki hiyo tujadili michango ya mawazo ya philosphers wengi kama si wote waliojitokeza kuweka hadharani ideas zao.

Ninaona hatari ya kuendelea hivi tulivyo. Hatari moja ni kwamba jinsi tunavyo-publicize idea ya philosopher mmoja basi wajukuu zetu hawatasubiri tufe wafunue vichwa vyetu bali bado tukiwa hai watatuuliza "hivi babu, kwani mwenye mawazo nchi hii alikuwa mtu mmoja tu?".

Kingine, ni kwamba tunapiga kelele kila siku kuwa historia imepindishwa tutafiti historia ya kweli. Sasa tunachofanya ni kilekile. Kijana wa siku hizi kama mimi haoni kama sentensi yake itapata usikilizwaji bila kupachika maneno kama "kumuenzi Baba wa Taifa", "Kama alivyosema Nyerere", "Kama hotuba fulani ya Nyerere" na mengine mengi mradi tu litamkwe jina Nyerere na walau neno moja alilolisema wakati fulani.

Ukitamka neno "Kama alivyosema Shivji" wanaweza kukusikiliza kwa sababu yuko hai lakini akifa wanaweza kusahahu. Ni wangapi wanasema "Kama alivyosema Shaban Robert" na wanasikilizwa. Nyerere mwenyewe alikuwa anarejea na kuwataja maphilosopher kama Plato wala si kusema "Kama nilivyosema mimi".

Hivyo, nadhani tutaelewa vizuri nia yangu kuwa kuna maphilosopher wengi na wametoa mawazo yao mengi lakini hawajapata populality kama Nyerere na tusipokuwa makini tutapoteza mawazo yao au watakuja watu toka Ulaya na kutuambia kwamba mtanzania mwenzenu alisema haya na tukaishia kushangaa.

Hivyo, badala ya kutengeneza kongamano la kumuenzi philosopher mmoja na tukaliita "kongamano la kumuenzi Mwalimu Nyerere" basi ni bora tuwe na wiki nzima ya philosophers wa Tanzania. Huko vitabu vyao viuzwe ili tujue ukweli au udhaif wa mawazo yao. Watu kama Oscar Kambona tuna haki ya kusoma vitabu vyao ili tuwahukumu wenyewe kwa akili zetu binafsi kwa kusoma walichoandika kama tunavyowahukumu waandishi na philosopher wengine duniani. hatutaki kusimuliwa na aliyesoma au aliyekuwepo.


Narudia, msiponielewa basi tusiwalaumu baba na mama zetu ambao tunasema walipindisha historia wakati kumbe afadhali wakati wao maana usipotaja majina ya wanasisa hata kazi ilikuwa mbinde kupata, sasa leo hatubabaiki kwa kuwa na alternatives nyingi maishani bado tunaendeleza kutaja jina moja tu na matokeo yake dunia inatushangaa kama tulikuwa na thinker mmoja tu.

Nawasilisha
 
Philosophy gani unayotaka ienziwe kwa Tanzania? Philosophy yenyewe ina deal na mambo mengi na ina branch nyingi. Based on your post assumption ni kwamba unaongelea 'Ethical Philosophy' ambayo ni sawa sawa na politics in our times to a large extent.

Kwa Tanzania hatuna philosophers yet, zaidi ya mwalimu na hata yeye mwenyewe alikuwa philosophical mwanzoni mwa uongozi wake especially with his ideas of building a nation of one people. He succeeded in the part by creating a sense of national identity but failed misery in other aspects of his philosophical approach especially in tackling poverty, embedding patriotism (kumbuka viongozi wengi wa leo walikua chini ya mwalimu this should tell you somen), alleviating people's social problems and in the end he opted for a dictatorial form of leadership to cling to his leadership.

Leo mwalimu kabaki na wafuasi wa aina mbili waweza waita 'hatar'i na wale walio 'unrealistic'. Hatari ni wale wanaosukumwa kidini zaidi kuliko kingine na unrealistic ni people like shivji ambao bado wana ideas za pan-africanism in this era. Hila Shivji ni kweli unaweza mwita a true philosopher kwa sababu ana mi theory yake ambayo anaona if implemented today it would improve the ethics of our society today be it nyingi ni unrealistic.

Wengine kama kina Kambona atuja wasoma na its not fair in your part kuchanganya history na philosophy unless unaiangalia in the mode of benefiting the social with the context of the time. But then kama utaifuatilia historia yetu vizuri utagundua Mwalimu was a total failure and his philosophy needs to be abandoned completely just as the Chinese did with the old socialists ideas.
 
Mkuu,

Whether nimetumia incorrect logo "Philosopher" sidhani kama incorrectness hiyo inafuta ukweli kwamba tunataka collection ya Thinkers wote wa Tanzania tujue mawazo yao.

Suala la kupitwa na wakati kwa mawazo ya Nyerere silipingi, tunachotaka ni information sahihi za walichosema waliowahi kuishi katika nchi hii. Kama msomaji anataka apitwe na wakati hilo ni suala lake. hakuna idea zilizopitwa na wakati kama theory nyingi za Kabla hajazaliwa Yesu lakini vitabu vyake havichomwi moto na badala yake kuna watu bado wanapata PhD kwa kuresearch zaidi hizohizo ancient theories.

Kama theory za Nyerere zilianguka, basi si kwamba watanzania wote kipindi chake hawakuwa na akili. Na si kwamba hawakuandika lolote. Zipo simulizi nyingi kwamba alielezwa na alsioma idea za watu wengi akapuuza hadi akaitwa haambiliki.

Sisi tunataka hawa ambao ni "unsung heroes" tuchambue walivyoiona Tanzania.
 
Back
Top Bottom