Iwe mwiko kuwa na sheria na ahadi za kidini Tanzania

Ina maana waisilamu wa nchi hii hawajui hizi sheria zilizopo "common law" zimetokana na mfumo wa kikristo? Mbina hawalalamiki kuwa kodi zao zinatumiwa na mahakama zinazotumia sheria za kikristo
 
Hiyo MOU siyo sheria kwamba lazima ifuatwe na wala haipo kwenye sheria yoyote wala katika katiba. By the way. huduma za jamii zinazotolewa na taasisi za kdini ikiwemo BAKWATA, si kwa waislam pekee wala wakristo pekee. Ni tofauti na Mahakama ya kadhi inayoshughulikia masuala ya kidini na kwa waislam pekee. Serikali haiwezi kuendesha mambo ya ibada na kuwafanya wananchi wote hata wasio waislam kwa lazima kushiriki ibada ya dini waisiyoiamini. Mambo ya dini na imani yaendeshwe na wanaoamini dini hiyo, na huu ndiyo uhuru wa kuabudu. Mtu haabudu kwa kulazimishwa, na wala Tanzania siyo nchi ya kidini. Si ya kiislamu, wala kihindu wala kikristo. Unajua, mahakama ya kadhi inayoendeshwa na serikali ina mambo mengi yaliyojificha na naweza kuyaeleza yote hatua kwa hatua, hapa niseme moja. Zaidi ya kuwa mahakama hiyo inashughulika na mambo ya ibada kwa waislamu pekee (mambo ya kidini), kadhi na wasaidizi wake wanateuliwa na rais wa nchi. Hivyo inatoa dhana kwamba rais wa Tanzania lazima awe muislamu kwa sababu rais "kafri" hawezi kuteua kadhi anayeshughulikia mambo ya kiislamu. Maana yake ni kwamba mahakama ya kadhi ya serikali inaisilmisha nchi. Hutataki kufika huko, ndiyo maana tunasema iwe mwiko kuwa na sheria, katiba wala ahadi ya mambo ya kidini katika nchi yetu.

Mkuu,
Kama mtu hajakuelewa ana shida kubwa sana kichwani!
 
Ina maana waisilamu wa nchi hii hawajui hizi sheria zilizopo "common law" zimetokana na mfumo wa kikristo? Mbina hawalalamiki kuwa kodi zao zinatumiwa na mahakama zinazotumia sheria za kikristo

unashauri nini??Au ziwekwe na zile za kwenye kadhi kuwa mtoto wa kike arithi nusu ya mirathi ya mtoto wa kiume,kwamba mtoto akizaliwa nje ya ndoa au muislamu akizaa na asiye muislamu basi mtoto ni haramu na hana stahiki yoyote???
 
Kuna watu wanahamu kukatakata mikono na kuponda mawe watu hadharan roho isuuzike kwa mgongo wa dini...amani iloyopo ni kikwazo kufanya yao...
 
Tatizo la wakristo hawasomi maandiko yao ukiangalia hukumu nyingi ambazo waislamu wanazitetea ni za kijamii sio kinyonyaji lakini kutokana na umagharibi uliopo vichwani mwao wanakuwa hawatafakari kabisa
 
unashauri nini??Au ziwekwe na zile za kwenye kadhi kuwa mtoto wa kike arithi nusu ya mirathi ya mtoto wa kiume,kwamba mtoto akizaliwa nje ya ndoa au muislamu akizaa na asiye muislamu basi mtoto ni haramu na hana stahiki yoyote???
Mkuu kuna mambo yamejificha mno kwenye hii kitu ya kadhi ya serikali. Wenyewe wanasema itaamua masuala yanayohusiana na jamii ya waislamu kwa sasa. Lakini pia wanasema maisha hayo ya jamii yanaongozwa na kurani na hadithi za mtume. Kwamba kwao masuala ya mirathi, malezi ya watoto, ndoa, ramadhani ni ibada. Hii ni wazi kuwa ni masuala ya kidini. Lakini pia mahitaji ya kijamii kulingana na maelekezo ya mtume na kuran yanaweza kubadilika kwa waislamu wa Tanzania, kwa mfano namna ya kuhukumu wezi. Hivyo mahakama hiyo ya kadhi ya serikali inaweza kuingiza hitaji hili siku za usoni. Na serikali si kazi yake kuzijadili hizo sheria kwa sababu ni za ibada na imani. Sasa unaweza kuona mambo mengi yaliyojificha kwenye hii kitu. Ndiyo maana tunasema masuala ya kdini yabaki kuendeshwa na watu wenye imani husika na siyo kuendeshwa na serikali na wananchi wote, hata wale wasio na imani hiyo.
 
Tatizo la wakristo hawasomi maandiko yao ukiangalia hukumu nyingi ambazo waislamu wanazitetea ni za kijamii sio kinyonyaji lakini kutokana na umagharibi uliopo vichwani mwao wanakuwa hawatafakari kabisa
Siyo kweli. Hukumu hizo ni ibada pia na ndiyo maana zinawahusu waislamu pekee, na makafiri hawaruhusiwi kuamua katika mahakama ya kadhi. Hukumu hizo zinaendana na mafundisho ya mtume na kurani. Haya ni masuala ya imani yaendeshwe na watu wenye imani hiyo peke yao.
 
Ina maana waisilamu wa nchi hii hawajui hizi sheria zilizopo "common law" zimetokana na mfumo wa kikristo? Mbina hawalalamiki kuwa kodi zao zinatumiwa na mahakama zinazotumia sheria za kikristo
Ni wapi katika katiba ya nchi ambapo mahakama za kikristo zinaendeshwa na serikali. Face the reality, kuna watu wa mila wanaamua kesi za kimila, serikali inagharimia hizo?. Vipi kuhusu mahakama za madhehebu mengine zinazoendeshwa na wenye imani husika?. Iweje mahakama ya kadhi iendeshwe na serikali na wananchi wote?. Kwani Tanzania ni nchi ya kidini? Siyo ya kihundu, kikristo wala kiislam.
 
Tatizo la wakristo hawasomi maandiko yao ukiangalia hukumu nyingi ambazo waislamu wanazitetea ni za kijamii sio kinyonyaji lakini kutokana na umagharibi uliopo vichwani mwao wanakuwa hawatafakari kabisa

Failures zenu mnasingizia wamarekani! Kwanza tunaliombea lidumu Taifa hilo ambalo ndilo polisi wa dunia! Ndilo lenye nguvu ya kuzuia dunia isivamiwe na giza la mashariki ya kati!
Ndiyo sababu mna uhasimu nalo!
 
Siyo kweli. Hukumu hizo ni ibada pia na ndiyo maana zinawahusu waislamu pekee, na makafiri hawaruhusiwi kuamua katika mahakama ya kadhi. Hukumu hizo zinaendana na mafundisho ya mtume na kurani. Haya ni masuala ya imani yaendeshwe na watu wenye imani hiyo peke yao.

Hao waongo wanasema blue kumbe njano! Unakumbuka hadithi ya ngamia na bwana wake! Kaomba kuingiza kichwa kujihifadhi, akiporuhusiwa kichwa kaanza kusema mgongo na hatimaye mwili mzima na akavunja kibanda cha bwana wake!
 
Mkuu, nimependa kufananisha na hadithi ya ngamia. Hebu ielezee kwa marefu yake.
 
Ina maana waisilamu wa nchi hii hawajui hizi sheria zilizopo "common law" zimetokana na mfumo wa kikristo? Mbina hawalalamiki kuwa kodi zao zinatumiwa na mahakama zinazotumia sheria za kikristo
Kusoma sana madrasa na kuacha medium and prmary school kunasababsha madhara ya akili....ndio maana mnalalamika kila sku whle hamtak kufanya kazi mnacheza bao kutwa na usku mnakesha kwenye michrku na taarabu alafu mnasema wakrsto wanapendelewa wakati wanafanya kazi kwa kujtuma 24hrs
 
Wakristo kila mwaka wanapewa zaidi ya 12billion kwa kupitia mou ya kuendesha makanisa yanayosimamia huduma za jamii je hili sio udini?
 
Wakristo kila mwaka wanapewa zaidi ya 12billion kwa kupitia mou ya kuendesha makanisa yanayosimamia huduma za jamii je hili sio udini?
Nyie waislam ndio mnaongoza kwa kutibiwa katka hosptali za makanisa na mkatkakukatka mashule ya taasisi za kkrsto chuo chenu cha kiislam morogoro mmekataa kufuata ata mfumo wa TCU kutokana na dhambi ya ubaguzi inayowatafuna
 
Nimegundua kuwa wengi hawaijui hata kataba tunayoitumia, hayo mnayo yazungumza mbona yapo kitambo lakini hayafuatwi? soma ibara ya 19 na 20 zinasemaje.

Na.15 ib.6 Sheria ya 1992 Na.4 ib…
19.-(1) Kila mtu anastahili kuwa na uhuru wa mawazo, Imani na uchaguzi katika mambo ya dini, pamoja na uhuru wa mtu kubadilisha dini au imani yake.
(2) Bila ya kuathiri sheria zinazohusika za Jamhuri ya Muungano, kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza dini itakuwa ni huru na jambo la hiari ya mtu ya binafsi, na shughuli na uendeshaji wa jumuiya za dini zitakuwa nje ya shughuli za mamlaka ya nchi.
(3) Kila palipotajwa neno "dini" katika ibara hii ifahamike kwamba maana yake ni pamoja na madhehebu ya dini, na maneno mengineyo yanayofanana au kuambatana na neno hilo nayo yatatafsiriwa kwa maana hiyo.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________
20 Uhuru wa mtu kushirikiana na wengine Sheria ya 1984 Na.14 ib.6
20.-(1) Kila mtu anastahili kuwa huru, bila ya kuathiri sheria za nchi, kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani, kuchanganyika na kushirikiana na watu wengine, kutoa mawazo hadharani, na hasa zaidi kuanzisha au kujiunga na vyama au mashirika yaliyoanzishwa kwa madhumuni ya kuhifadhi au kuendeleza imani au maslahi yake au maslahi mengineyo.
(2) Bila ya kujali masharti ya ibara ndogo ya (1) haitakuwa halali kwa chombo chochote cha siasa kuandikishwa ambacho kutokana na Katiba au sera yake-
(a) kinakusudia kukuza au kupigania maslahi ya-
(i) imani au kundi lolote la dini;

(ii) kundi lolote la kikabila pahala watu watokeapo, rangi au jinsia;
(iii) eneo fulani tu katika sehemu yoyote ya Jamhuri ya Muungano;
(b) kinapigania kuvunjwa kwa Jamhuri.

View attachment ILANI YA UCHUGUZI YA CCM 2005 CHANZO CHA UDINI.doc
 
Nyie waislam ndio mnaongoza kwa kutibiwa katka hosptali za makanisa na mkatkakukatka mashule ya taasisi za kkrsto chuo chenu cha kiislam morogoro mmekataa kufuata ata mfumo wa TCU kutokana na dhambi ya ubaguzi inayowatafuna[/QUOTE

Kwani tunatibiwa bure? Hiyo mou ikifa ujue na huko kijifanya kwenu kuwa mpo mbali kutatoweka kama mshumaa, acheni kufanya waislamu wajinga tena mmekuta ni watu wenye upendo na wenye kujua uvumilivu
 
Back
Top Bottom