- Source #1
- View Source #1
Kuna taarifa zisizo lasim kwamba Raisi wa Ivory Coast kapinduliwa na haijulikana alipo, Sasa sijapatavtaarofa rasimi. Huenda Wafaransa wamefanya yao huko.
- Tunachokijua
- Madai
Mei 21, 2025 zilizuka taarifa katika mitandao mbalimbali ya kijamii zikidai kuwa kuna mapinduzi yametokea nchini Ivory Coast.
Mtumiaji mmoja wa mtandao wa X aliandika “BREAKING NEWS “There's a coup d'état going on currently in Ivory Coast. Abidjan is burning. Alassane Ouattara the French puppet President of Côte d'Ivoire has either been killed yesterday or has flee the country. GOD is busy freeing Africa from the sheckles of oppression” akimaanisha kuwa;
“kuna mapinduzi ya kijeshi yanaendelea nchini Ivory Coast, Abdijan inawaka moto
Rais wa Côte d'Ivoire, Alassane Ouattara, ambaye ni kibaraka wa Wafaransa, ama ameuawa jana au amekimbia nchi.
MUNGU yuko kazini kuiweka Afrika huru kutoka kwenye minyororo ya uonevu”
Uhalisia wa madai hayo
JamiiCheck imefuatilia madai hayo na kubaini kuwa si ya kweli. Hakuna chanzo chochote cha kuaminika kilichochapisha taarifa hiyo ya mapinduzi ya kijeshi huko Ivory Coast.
Rais wa Ivory Coast Outarra alionekana amehudhuria baraza la mawaziri katika makazi ya Rais Mei 21, 2025. Ukurasa wa Facebook wa Rais wa Ivory Coast ulipost taarifa iliyosomeka “Rais wa Jamhuri, Alassane Ouattara, aliongoza Baraza la Mawaziri siku ya Jumatano, Mei 21, 2025, katika Ikulu ya Jamhuri”.
Tovuti ya baraza la Ulaya Mei 21, 2025 iliripoti kuwa Rais wa Baraza hilo atakwenda nchini Ivory Coast ambapo atapewa tuzo ya UNESCO lakini pamoja na mambo mengine atakutana na Rais wa taiafa hilo, Ouattara. Baadhi ya maneno yaliyosomeka kwenye taarifa hiyo ni;
“Rais wa Baraza la Ulaya, António Costa, atasafiri kwenda Abidjan, Côte d'Ivoire kupokea Tuzo ya Amani ya UNESCO Félix Houphouët-Boigny tarehe 22 Mei 2025.
Pamoja na hafla hiyo, atakutana pia na Rais wa Côte d'Ivoire, Alassane Ouattara, kujadili mahusiano ya pande mbili, utulivu wa kikanda, na maandalizi ya mkutano ujao wa kilele kati ya Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika utakaofanyika baadaye mwaka huu”.
Ukurasa wa Facebook wa Rais wa Ivory Coast ulichapisha taarifa kuelezea ajenda ya Rais wa nchi hiyo kwa siku ya Alhamisi Mei 22, 2025, saa 4:00 asubuhi ni kuhudhuria Sherehe ya Kiheshima ya Tuzo ya Félix HOUPHOUËT-BOIGNY – UNESCO kwa Ajili ya Utafutaji wa Amani.