Ivory Coast Vs Tanzania

Mkuu mpira hauko hivyo, mpira sio uwezo tu ni pamoja na bahati, unaweza kuamini kama Ufaransa waliondoka bila kushinda mechi hata moja kombe la dunia 2002 na walikuwa na washambuliaji nyota kabisa watatu wa daraja la dunia, huwezi jua leo bahati inaweza kuwa upande wetu ukashangaa kila cross ya Gervinho Drogba akipiga kichwa inagonga mwamba au inatoka nje au Kaseja anadaka halafu ghafla dakika ya 88 Ngasa akanasa pass ya Salum Abubakar na kukimbia nao huku Samatta akifuatia kwa kasi na mara Ngasa anafyatua Kombora ambalo Barry anapangua na kurudi uwanjani halafu inakutana na Samatta anamaliza kazi. Itakuwaje hapo? lazima uzime TV.

Hizo ni ndoto za alinacha,mimi naona Kaseja akiomba apigwe subb kuepusha kuzidi kuchafua record kwa kufungwa magoli mengi.
 
hapa bongo tutaona kupitia tv gani jamani, msaada please, dakika chache kabla mpira haujaanza....
 
Lazima tuandamane manake timu yetu haina uwezo huo na hata wachezaje wetu pia wanajua hilo wamekula lift mpaka huko tu na selection yenyewe siyo nzuri ni simba tupu.

Wenyewe (reffering to Salum Aboubakar) walishajiona ni kama waokota mipira mbele ya wachezaji wa Ivory Coast,wakiongozwa na nahodha wao atakayeongoza kuokota mipira ya wavuni,sasa kunanini tena hapo?
 
Gambia anaongoza bao 1-0 dhidi ya Moroko now dakika ya 26. Hawa tuko nao kundi moja na tukumbuke Moroko alishatufanyia mchezo mbaya Uwanja wa taifa na kwao Rabat. Nafasi yetu labda leo tushinde
 
Kaseja anaonekana kuwapa moja vijana,lakini ivory kiukweli wapo full ngwamba,yaani mashine zote ndani
 
Game saa mbili usiku kwa saa za Tanzania ambapo ni saa 11 jioni kwa saa za Ivory Coast. Inaonyeshwa na RTI 1 TV ya Abidjan. Kazi kwako!
Je hakuna online TV nyingine inaonyesha hii mechi?? maana huku nadhani siwezi ipata hiyo TV, naombeni mwenyeonline link atuwekee hapa tuone
 
Game limeanza dakika saba now hakna bao. Nacheki pia game la Sudan vs Zambia nitawapeni updates mechi zote hizi
 
Game limeanza dakika saba now hakna bao. Nacheki pia game la Sudan vs Zambia nitawapeni updates mechi zote hizi

Unatumia hizi link ulizonitumia? Zinafanya kazi .. Nipo barabarani kijana kama zinafanya kazi nipe feedback nitulie sehemu nicheki game.
 
Back
Top Bottom