Ivi inawezekana kweli????

Ivi inawezekana kweli????

SIS DREAD

Member
Joined
Jan 3, 2013
Posts
33
Reaction score
2
Wadau habari za mchana huu jana nilisafiri na kaka mmoja kwenye ndege alikuwa ni mtu mwenye mawazo mengi sana badae akaamua kuzungumza namnukuu kama ifuatavyo. (Dada mm naitwa .......................... akataja jina lake naishi Arusha nafanya kazi katika mgodi wa Tanzanite nimeoa na nina mtoto mmoja sijui wewe unaitwa nani nami nikataja jina langu nakumweleza naishi Dar es salaam nimetoka Arusha kwa matembezi tu akaendelea samahani dada mm nina matatizo makubwa na mke wangu nikastuka kdg na kwa haraka moyoni nikajiambia sasa matatizo yako na mkeo mm yananihusu nn? kama vile alinisoma akilini mwangu akanambia najua hili nalokuelezea hapa halikuhusu lakini nakuomba tu univumilie na unisikilize tafadhari nikamwambia usijali endelea akasema dadahuu ni mwaka wa 3 nalala kitanda kimoja na mke wangu lakini hatushirikiani chochote katika tendo la ndoa jaman mwenzenu nilistuka mno yani naomba niweke wazi nilistuka na kutomwamini huyu kaka nilijiuliza maswali mengi sna haraka haraka wanawezaje kulala kitanda kimoja miaka 3 na awashirikiani kwa chochote lakini huyu kaka alivyoendelea kunielezea nikaanza kupata picha kamili kwamba akisemacho ni kweli nilimuuliza kitu kimoja unadhani kuna wakati utafika mtashilikiana tena na mke wako akajibu hata wakati ukifika yy binafsi hayuko tayari tena wataishi hivyo hivyo hd kifo kiwatenganishe kwani hayuko tayari kumtaliki mkewe sasa wadau mm nko njia panda na ndoa hii ivi tunaiitaje ndoa hii? na je kwa umri niliomwona nao huyu mkaka ni age ya miaka 30 na kitu tena azidi 35 it means na mkewe hatakuwa 30 ivi sasa mbona bado vijana je haja zao wanatimizia wapi? nikamuuliza umewahi kwenda Kanisani au hata kwa wasimamizi wenu mkakaa chini kuongea akasema yote wamefanya tena wakiyaongea wanakubaliana yameisha ila wakifika kitandani hakuna kinachoendelea kiukweli nilikosa cha kumshauri nimebaki naona kama mchezo wakuigiza labda ww mdau kama unaushauri wwte utoe.
 
Umeamua kuja kunianika mtandaoni? Sawa, Mungu akubariki sana.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Sasa mleta mada mbona umeongea nusu nusu? Alikwambia chanzo cha ugomvi wao ni nini hasa? Labda tukijua hilo tunaweza kuona cha kushauri
 
Hahaaa, nadhani kujitambulisha kitanzanite tanzanite, kabla hamjaongea mengine keshachomeka matatizo ya ndoa, nadhani ilikuwa ni njia labda ya kutaka kukutongoza wewe akaanzia hapo ili usimuulize tena maswali ya usaliti n.k. We unafikiri alikuambia ili umshauri? wakati anasema hata mkewe akubali yeye hayuko tayari tena? kama hayuko tayari anataka ushauri au anataka huruma yako? Hahaaaa, cheyeya chalii ...!
 
Si ulimpa email na namba yako ya simu, ndio ulishatongozwa hivyo. We shangaa tu!
 
mbona umesahau kumalizia kwamba ume-fall in love na huyo kijana?
 
wadau habari za mchana huu jana nilisafiri na kaka mmoja kwenye ndege alikuwa ni mtu mwenye mawazo mengi sana badae akaamua kuzungumza namnukuu kama ifuatavyo. (dada mm naitwa .......................... Akataja jina lake naishi arusha nafanya kazi katika mgodi wa tanzanite nimeoa na nina mtoto mmoja sijui wewe unaitwa nani nami nikataja jina langu nakumweleza naishi dar es salaam nimetoka arusha kwa matembezi tu akaendelea samahani dada mm nina matatizo makubwa na mke wangu nikastuka kdg na kwa haraka moyoni nikajiambia sasa matatizo yako na mkeo mm yananihusu nn? Kama vile alinisoma akilini mwangu akanambia najua hili nalokuelezea hapa halikuhusu lakini nakuomba tu univumilie na unisikilize tafadhari nikamwambia usijali endelea akasema dadahuu ni mwaka wa 3 nalala kitanda kimoja na mke wangu lakini hatushirikiani chochote katika tendo la ndoa jaman mwenzenu nilistuka mno yani naomba niweke wazi nilistuka na kutomwamini huyu kaka nilijiuliza maswali mengi sna haraka haraka wanawezaje kulala kitanda kimoja miaka 3 na awashirikiani kwa chochote lakini huyu kaka alivyoendelea kunielezea nikaanza kupata picha kamili kwamba akisemacho ni kweli nilimuuliza kitu kimoja unadhani kuna wakati utafika mtashilikiana tena na mke wako akajibu hata wakati ukifika yy binafsi hayuko tayari tena wataishi hivyo hivyo hd kifo kiwatenganishe kwani hayuko tayari kumtaliki mkewe sasa wadau mm nko njia panda na ndoa hii ivi tunaiitaje ndoa hii? Na je kwa umri niliomwona nao huyu mkaka ni age ya miaka 30 na kitu tena azidi 35 it means na mkewe hatakuwa 30 ivi sasa mbona bado vijana je haja zao wanatimizia wapi? Nikamuuliza umewahi kwenda kanisani au hata kwa wasimamizi wenu mkakaa chini kuongea akasema yote wamefanya tena wakiyaongea wanakubaliana yameisha ila wakifika kitandani hakuna kinachoendelea kiukweli nilikosa cha kumshauri nimebaki naona kama mchezo wakuigiza labda ww mdau kama unaushauri wwte utoe.
matatizo ya miaka mitatu,aje kukwambia wewe mkiwa kwanye usafiri usiozidi masaa mawili?labda una ngekewa naye,mtafute!
 
My godness!..ndo ushatongozwa hivyo mdada..hapo hakuna cha eti ushauri wala nini?
'Eti ana miaka mitatu hashirikiani na mkewake'?..my foot..yaani umeshindwa kung'amua mtego mrahisi hivi?..
mkubalie tu umsaidie manake wewe ndo umemsikiliza mwanzo mwisho....
 
Wanaume mashetani sana, akimtamani mwanamke hutumia trick za aina mbali mbali ili aonewe huruma atimiziwe lengo lake.
 
Wanaume mashetani sana, akimtamani mwanamke hutumia trick za aina mbali mbali ili aonewe huruma atimiziwe lengo lake.

Uko too general sana dadangu,hata kama umetendwa na kutoswa sio kututukana kiasi hiko
Futa kauli
 
hii gia inajulikana muda kwa kutongozea hujawahi kuisikia shoga? wewe ni mgeni wa wanaume haswaa.
 
mshamba tu huyo .... kuna mmoja nilishapanda nae bus akanipa story zake mbovu akasema eti ana watoto wa nne wa kiume akasema anatamani mtoto wa kike sana mwanamke atakaemzalia mtoto wa kike atamnunulia gari
nikamuuliza gari tu kwa exchange ya mtoto akasema ndio,nikamwambia basi kamnunulie mamayako maana alikuzaa nikahama na seat maana dar express huwa hayajazi saa zote...nikajua tu huyu anitaka baadae nikarudi kwenye seat nikalala zangu.akawa anahaha tu mara utakula kuku au mbuzi ...wanaume wapuuuzi wewe hasa waume za watu kaa mbali
 
Wanaume mashetani sana, akimtamani mwanamke hutumia trick za aina mbali mbali ili aonewe huruma atimiziwe lengo lake.

anaweza akajiliza ukaona unaliliwa kumbe anakung'ong'a moyoni. chezea banaume hawa. anaweza akamtukana mkewe kuwa ni shetani ukajiona wewe malaika wakati ana madhumuni mengine. shwain
 
Yani hapo huyo kaka atakua lazima alimtenda mke wake,mke akachoka,akaamua amlie jiwe afanye mambo yake mpaka achoke,sasa amechoka kufanya mambo yake amerudisha mapenzi kwa mke wajanja watakua wamemuwahi,sasa yy anataka ushauri wa nn,watu wa mawe tunawajua sana % ni wachafu wa tabia!
 
anaweza akajiliza ukaona unaliliwa kumbe anakung'ong'a moyoni. chezea banaume hawa. anaweza akamtukana mkewe kuwa ni shetani ukajiona wewe malaika wakati ana madhumuni mengine. shwain
mamburulah kabisa mimi mume wa mtu kabisa kabisa akiingia kwenye anga zangu huwa nmpa za uso hadi mwenyewe anajiona choo cha jiji
 
Kuna jamaa analalamika forward yake butu thread ya pili hapo,,, huku kuna mdada amezidiwa akili kwenye fast jet anakaribia kuvuliwa pichu kwa huruma..

Haya wewe uliyesema forward yako butu njoo ujifunze style ya counter attack hapa saa li moja tu on board mdada ameshaona huruma

Jamii forum ni zaidi ya social network
 
Back
Top Bottom