ITV yagawa madawati 250 katika kutimiza miaka 20

ITV yagawa madawati 250 katika kutimiza miaka 20

Umeanza vizuri umemaliza vibaya,sasa Chadema inakusanya kodi? au ni NGO ile p.u.bu lako
 
wadau nawasalimu tena.
Kituo cha Radio one na ITV wametoa mchango Wa madawati mia mbili na hamsini kwa shule ya msingi Tandale kwa wanafunzi karibu elf Moja waliokuwa wanakaa chini, akizungumza na wanafunzi hao Mkurugenzi Wa redio one na ITV.

Bi. Mhavile amesema wameona sio busara kusherekea miaka 20 pasi kutafuta jambo jema kwa jamii yao ,mosi wanafunzi hao wakiojesha nyuso za Furaha wamemshukuru bwana Mengi kwa msaada huo.

my take: vyama vya siasa kama chadema wajifunze jambo kupitia hili kuwa wananchi wanataka maendeleo na sio maandamano.
nawasilisha

Mada na observation yako ni nzuri lakini YOUR TAKE ni ya kipuuzi. Ningekuona una maana kama ungezipeleka lawama hizi kwa CCM na serikali yake. Haya yote yanasababishwa na ubadhirifu wa viongozi na watendaji wa serikali, wananchi wanalipa kodi, miundombinu ya elimu ni jukumu la serikali vyote hivi hawafanyi lakini wewe unawaruka unaenda kuwarushia lawama Chadema. Kwa lipi hasa? Japo kuna maandamano siyaungi mkono, lakini mengine ni ya kuwaamasha watu kama nyie ili muone udhaifu wa serikali na huyo anayewaamsha ndo mnamuona anakosea. Tanzania tuna safari ndefu sana bado, na kwa hali hii tutegemee ongezeka kubwa la tabaka la walio nacho na wasio nacho. Vilevile tuwe tayari kwa mapambano kati ya haya makundi mawili ikiwemo wizi, uhalifu, ujambazi na ukosefu wa amani kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom