ITV VIPI TENA?

b191

JF-Expert Member
Jul 24, 2016
742
1,031
Habari wanajamvi!

Naomba niseme ukweli wangu kuwa Mimi ni mmoja kati ya watazamaji wazuri wa vipindi vya ITV - Tanzania hususani Maigizo.

Baada ya KAOLE kuacha kuonyesha vipindi vyao sikuwa na hamu ya kuangalia kile kipindi cha kila Jumamosi SAA 3 USIKU.

Lakini kuna IGIZO lilianza kuonyeshwa likiitwa DHAMIRA lilinivutia sana na kunifanya niwe karibu na TV kila Jumamosi. IGIZO hili lilikuwa na Waigizaji Wachanga lakini wenye taaluma ya hali juu ya uigizaji. Mfano Mwalimu Msham, Gumbo nk.

Season ya 1 na 2 vilienda vizuri kabisa. Wakati namsubiri Season ya 3 kwa hamu kubwa naona kuna IGIZO jipya limeanza.

Binafsi nikilinganisha ubora wa IGIZO hili la sasa na lile la zamani la DHAMIRA naona ITV wametukoseha sana RAHA sisi watazamaji wake kwa kutuondolea IGIZO LA DHAMIRA.

Naamini kuna watu wa ITV TANZANIA humu jamvini na watausoma ujumbe huu.

TAFADHALI RUDISHENI WAIGIZAJI WA DHAMIRA NA MUONGOZAJI WAO ILI MITIMA YA WATAZAMAJI WENU IZIDI KUFURAHIA UWEPO WENU.

Nawasilisha...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom