utaifakwanza
JF-Expert Member
- Feb 1, 2013
- 14,193
- 2,812
Mwenyekiti wa jukwaa la wahariri na mhariri mtendaji wa new habari absalom kibanda amerejea leo nchini na kulakiwa na watanzania wapenda amani na maendeleo. Wanachi wengi sana walijitokeza huku wengine wakitokwa na machozi ya huruma huku wakiwa hawaamini kumuona tena kibanda akiwa na siha njema namna ile.
Kibanda amewashukuru watanzania kwa dua zao wakati wote tangu apatwe na masibu yale na ameahidi kuelezea mkasa mzima jinsi ulivyokuwa na kutoa leads ya ni nani hasa wahusika wa utesaji dhidi yake...
pole sana kibanda na karibu nyumbani...mungu azidi kukujaala afya njema uendelee kulijenga taifa lako...damu yako haijamwagika bure.
nilimsikia anasema kwanini ktk hii miaka nane ambayo jk amekaa madarakani kumekuwa na matukio mengi ya ukatili kwa waandishi wa habari? anasema hawezi kusubiri asemewe kama wengine hivyo atalipua bomu soon. sisi yetu macho na masikio
nilimsikia anasema kwanini ktk hii miaka nane ambayo jk amekaa madarakani kumekuwa na matukio mengi ya ukatili kwa waandishi wa habari? anasema hawezi kusubiri asemewe kama wengine hivyo atalipua bomu soon. sisi yetu macho na masikio
Kibanda umekuja kwa mbwembwe sana ukisema hautanyamanza sasa ss usitufanya tuweke masikio juu kusubili kijacho kutoka kwako harafu baadaye kimyaaaaaa au huwa mnajinunua wenyewe maana mbwembwe huwa na wandishi wa habari baada ya hapo kimyaaaaaaaaaaaaaaa lakini pole sana
Una maana wale watoa kucha na meno bila ganzi watamrudia tena,ili waje wamnyofoe hilo jicho la pili lililobaki?!
Na pamoja na mzee wa movie ya kichaa wa Kenya,kuwa hadi leo,baada ya miezi mitatu hajamkamata hata mtuhumiwa mmoja,wa tukio la kutekwa kwa Kibanda,bado hata hivyo,JK,amemtunukia utumishi uliotukuka na amempandisha na cheo!!
pole kibanda
pole dr ulimboka
pole daudi mwangosi
pole dr mwakyembe
pole prof mwandosya
poleni wanyakyusa
poleni wana mbeya
poleni waTANGANYIKA