ITV Tanzania:Kibanda awaambia Polisi waseme ukweli

kibanda tueleze ukweli ulimboka walimwamisha na nchi kabisa
 
Natumaini naye atatafutiwa fungu la kutosha ili atulie, nchi hii inaweza kukufanyia unyama na kukutajirisha at the same time. Hiyo bahati wengine haituangukii. Tusubiri hayo mabomu hata ikiwa kwa karne nyingi, tutaendelea kusubiri mpaka tuwajue watesaji.
Ndugu hela haina thamani zaidi ya macho yako, usiombe hilo mshukuru mungu.
 
Atasema tu maana mwenzake Uli amekula kitu cha kuziba mdomo yeye hawezi kukubali maana amepata ulemavu!inasikitishaa sana!jipange na kulipua bomu!hata ikibidi akiwa uhamishoni ubalozi usa au uk akaombe hifadhi!maana wale wanajua kila kitu hata waliohusika wanawajua!wanajua fitna zaidi ya tiss wetu !wanajua ukweli woote
unawaaminia USA na UK to the extent wakikuposa unawakubalia. ni wakoloni tuu wale
 
Peleka ushahidi polisi kwa mujibu wa sheria ya mwenendo wa jinai [the criminal procedure act]... sio unapayuka tu. una uhakika JK anahusika??? are you sure? Leta ushahidi wako hapa jamvini au peleka polisi hq.

Vipi mkuu JK mzazi wako? Pole kwa kuwa na mzazi dhaifu.
 
pole kibanda
pole dr ulimboka
pole daudi mwangosi
pole dr mwakyembe
pole prof mwandosya
poleni wanyakyusa
poleni wana mbeya
poleni waTANGANYIKA

pole juan mwakyusa
pole dan mwakiteleko
poleni wanyakyusa
poleni wana mbeya
poleni waTANGANYIKA
 
Peleka ushahidi polisi kwa mujibu wa sheria ya mwenendo wa jinai [the criminal procedure act]... sio unapayuka tu. una uhakika JK anahusika??? are you sure? Leta ushahidi wako hapa jamvini au peleka polisi hq.

Watu wengine hua najiulizaga kama mpo Tanzania hi hi au nje ya nchi? Lakini kama mpo Tanzania hi hi, may be mnayo macho lakini hayaoni na au mnayo masikio lakini nayo hayasikii au labda yanasikia lakini may be ule Ubongo unaotafsiri kile unacho kisikia na kukiona hautaki kuushughulisha, vinginevyo labda na wewe ni mtu wa system! Hi comment yako imekuonesha hivyo. Sheria na Tanzania wapi na wapi bwn.
 
peleka ushahidi polisi kwa mujibu wa sheria ya mwenendo wa jinai [the criminal procedure act]... Sio unapayuka tu. Una uhakika jk anahusika??? Are you sure? Leta ushahidi wako hapa jamvini au peleka polisi hq.

tulia mliberaliiiiiiiiiiiiiiiiiiii..............punguza mapovu, usiwe na papara hata kama unawashwa au umeshika ukuta.

1. Unaikumbuka ya mwakyembe??.... Ushahidi haukufika kwa dci manumba?? Haukuandikwa magazetini hata kabla ya yeye kudhurika?? Nini kilitokea??kuna mtu amefungwa hata kufunguliwa mashtaka??

2. Kwa akili zako unazani yule chizi wa kova ndiye anaweza kumteka na kupiga ulimboka pekeyake kwenye gari huku akiliendesha hilo gari...labda kama yule chizi anamikono 10 kama jini, lakini unafahamu watu aliokuwa anawasiliano kumbukumbuku zipo katika mitandao ya simu na line zao zimesajiliwa umesikia aliyekamatwa.... Nini kinaendelea???
3. Unakumbuka story ya kolimba?? Ni nani amewahi kukamatwa mpaka leo?? Umesahau ya marehemu imrani kombe???
4. Unafahamu muendelezo wa kesi wa yule prof mwaikusa wa ud, wa kuvamiwa na kuuwa jirani na nyumbani kwake?? Unajua nini kinaendelea....

Kwa kuwa wewe ni mliberali na adui yako ni chadema.... Basi sema yooote hayo niliyoyataja kwa uchache ni chadema ndio wanahusika tena dr. Slaa ndio kafanya hivyo......

Pole sana mzee wa haki sawa kwa wote kachukue buku 7 lumumba.
 
Watu wengine hua najiulizaga kama mpo Tanzania hi hi au nje ya nchi? Lakini kama mpo Tanzania hi hi, may be mnayo macho lakini hayaoni na au mnayo masikio lakini nayo hayasikii au labda yanasikia lakini may be ule Ubongo unaotafsiri kile unacho kisikia na kukiona hautaki kuushughulisha, vinginevyo labda na wewe ni mtu wa system! Hi comment yako imekuonesha hivyo. Sheria na Tanzania wapi na wapi bwn.

asikupotezee muda huyo mkuu, huyo METSADA NI MLIBERALI na anafaidka na huu mfumo mbovu.
 
Kama yeye hawezi kujisemea anadhan polis watamsemea? Naona mbwembwe tu za kutafuta mlango wa kunegotiate na watesi wake!. Angekuwa muwazi tu kwa kutangaza bei yake aitakayo wampatie ili awasitiri au kinyume chake!
hata mi naona anataka kutuchezea akili tu,kama alikua anajua setup yote kwanini asiepuke?au kaupata ufunuo wa watesi wake akiwa hospitalini sozafrika?
 
Mwenyektii wa jukwaa la wahariri Absalom Kibanda amerejea nchini baada ya matibabu ya muda mrefu nchini Afrikakusini huku akiomba polisi kueleza ukweli wa yaliyotokea na kuchukua hatua kwa yeyote aliyehusika kwenye unyama aliotendewa.

Source:ITV Tanzania Facebook Page
.
Swali:Kuna ukweli Gani Polisi wameuficha kuhusu kutekwa na kuteswa kwa Kibanda??

kama Kibanda ana maneno yeyote anayotaka kuwaambia watanzania ni bora angeyasema mara tu alipofika au ayaseme mapema, vinginevyo itakuwa kama Ulimboka
 
polisi hawaezi eleza chochote kuhusu uteswaji wa kibanda, yaani walivyomkamata lwakatale na kumtuhumu ndio wamemaliza kazi, style yao mbona ndio hiyo? mkenya kichaa aliyemtesa ulimboka mlishasikia tene neno?
 
tatizo nalo liona kwa waandishi wa habari! hawana umoja,wangeacha kuchua habari za kipolisi zote...
 
nilimsikia anasema kwanini ktk hii miaka nane ambayo jk amekaa madarakani kumekuwa na matukio mengi ya ukatili kwa waandishi wa habari? anasema hawezi kusubiri asemewe kama wengine hivyo atalipua bomu soon. sisi yetu macho na masikio

Labda ni namna ya kufungua uwanja wa mazungumzo ili waliomfanyia ule umafia waingie kiwewe na kumpoza kiaina! Kama vipi sioni kwa nini hakusema kabisa? Au anangoja nini?
 
Mwenyekiti wa jukwaa la wahariri na mhariri mtendaji wa new habari absalom kibanda amerejea leo nchini na kulakiwa na watanzania wapenda amani na maendeleo. Wanachi wengi sana walijitokeza huku wengine wakitokwa na machozi ya huruma huku wakiwa hawaamini kumuona tena kibanda akiwa na siha njema namna ile.

Kibanda amewashukuru watanzania kwa dua zao wakati wote tangu apatwe na masibu yale na ameahidi kuelezea mkasa mzima jinsi ulivyokuwa na kutoa leads ya ni nani hasa wahusika wa utesaji dhidi yake...

pole sana kibanda na karibu nyumbani...mungu azidi kukujaala afya njema uendelee kulijenga taifa lako...damu yako haijamwagika bure.

Kama mchawi vile.
 
Sina uhakika kama kweli M/kiti Kibanda atakuja front kutueleza kama anavyodai,naungana na mchangiaji mmoja kuwa unateswa kisha unatajirishwa huku ukitishwa zaidi halafu na maswali mfululizo kuwa shida yako nini,binafsi bado sijaona mwandishi anayesimama kwa miguu yake naona wengi wanatumika na wanasiasa na hili nina uhakika kibanda analijua vizuri.
 
Watu wengine hua najiulizaga kama mpo Tanzania hi hi au nje ya nchi? Lakini kama mpo Tanzania hi hi, may be mnayo macho lakini hayaoni na au mnayo masikio lakini nayo hayasikii au labda yanasikia lakini may be ule Ubongo unaotafsiri kile unacho kisikia na kukiona hautaki kuushughulisha, vinginevyo labda na wewe ni mtu wa system! Hi comment yako imekuonesha hivyo. Sheria na Tanzania wapi na wapi bwn.

Rubbish! Nadhani wewe huna unalolijua... to say the least.
 
Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda amerejea chini jana kutoka Afrika Kusini alikokuwa akitibiwa na kusisitiza kwamba hatanyamaza kuzungumzia janga la kushambuliwa kwake.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, Kibanda alisema asingependa kuona jambo hilo linamtokea mwandishi mwingine wa habari.

Kibanda, ambaye pia ni Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, alikuwa akitibiwa huko baada ya kushambuliwa na kuumizwa vibaya na watu wasiofahamika usiku wa Machi 5, mwaka huu.

Alisema kutokana na hali hiyo, waandishi wanapaswa kuwa na mshikamano ili kuhakikisha matukio ya aina hiyo hayajirudii.

“Waandishi wana nafasi kubwa ya kuliondoa taifa katika hali hii. Waendelee kuandika na kuelimisha wananchi ili nao wasaidie kuzuia ukatili wa aina hii. Hatuwezi kuishi katika nchi ambayo watu wanafanyiwa ukatili mkubwa kiasi hiki halafu wanaachwa hivihivi,” alisema Kibanda.

Kibanda alisema jambo lililomtokea lilikuwa baya kwani alikuwa akipoteza fahamu kila wakati kutokana na maumivu makali.

“Lakini sasa namshukuru Mungu, nimepona, sina maumuvu tena kama yale,” alisema Kibanda na kuelezea kufurahishwa kwake na ushirikiano mkubwa alioupata kutoka kwa wadau wa habari na wananchi kwa jumla.

Ameiomba Serikali kuharakisha ripoti ya uchunguzi wa tukio lake kwa sababu ni muda mrefu umepita na kwamba mpaka sasa hakuna taarifa zozote zilizotolewa.

“Nilipolazwa Muhimbili Kitengo cha Moi, alikuja kuniangalia Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova na Mkuu wa Jeshi la Polisi, Said Mwema waliniahidi kushughulikia suala langu ili waliohusika na tukio hili wafikishwe mahakamani,” alisema.

Alisema si hao tu, bali pia Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi, ambaye alikwenda Afrika Kusini kumjulia hali, alimwahidi kuwashughulikia watu waliohusika.

“Sisi sote ni mashahidi wa ukimya ambao upo kwani mpaka sasa watu hao hawajakamatwa, wala hakuna taarifa zozote zinazohusu kufikishwa mahakamani,” alisema.

Kibanda alisema katika miaka ya karibuni, kumekuwa na matukio mbalimbali yanayohusisha kupigwa, kuuawa au kutishiwa maisha kwa waandishi, jambo ambalo linaonyesha wazi kuwa matukio hayo hayaji bure, kuna chanzo chake.
 
tulia mliberaliiiiiiiiiiiiiiiiiiii..............punguza mapovu, usiwe na papara hata kama unawashwa au umeshika ukuta.

1. Unaikumbuka ya mwakyembe??.... Ushahidi haukufika kwa dci manumba?? Haukuandikwa magazetini hata kabla ya yeye kudhurika?? Nini kilitokea??kuna mtu amefungwa hata kufunguliwa mashtaka??

2. Kwa akili zako unazani yule chizi wa kova ndiye anaweza kumteka na kupiga ulimboka pekeyake kwenye gari huku akiliendesha hilo gari...labda kama yule chizi anamikono 10 kama jini, lakini unafahamu watu aliokuwa anawasiliano kumbukumbuku zipo katika mitandao ya simu na line zao zimesajiliwa umesikia aliyekamatwa.... Nini kinaendelea???
3. Unakumbuka story ya kolimba?? Ni nani amewahi kukamatwa mpaka leo?? Umesahau ya marehemu imrani kombe???
4. Unafahamu muendelezo wa kesi wa yule prof mwaikusa wa ud, wa kuvamiwa na kuuwa jirani na nyumbani kwake?? Unajua nini kinaendelea....

Kwa kuwa wewe ni mliberali na adui yako ni chadema.... Basi sema yooote hayo niliyoyataja kwa uchache ni chadema ndio wanahusika tena dr. Slaa ndio kafanya hivyo......

Pole sana mzee wa haki sawa kwa wote kachukue buku 7 lumumba.

Hahahahahaaaaaaaaaaaaaaaaa! Huna unalolijua wewe... endelea tu kukesha humu JF na kukalia propaganda za bosi wako slaa na magazeti ya udaku. Kama una ushahidi wa watu kuhusika na hivyo vitendo peleka polisi au kafungue mashitaka mahakamani kama private prosecutor - sheria inakuruhusu!
 
Nilimsikia akiahidi kuanika ukweli wote wa watesi wake bila kumuonea mtu, inashangaza tena kulitaka jeshi la polisi liwataje!

Hata hivyo, kwa mtazamo wangu Kibanda alishawataja watesi wake kupitia msemaji wake, jamaa wa mtandao hatari!!!
 
Bado wana tafuta mwendawazimu wa kumbambikia kesi, Hii ni nchi iliyo laaniwa! mwanzoni serikali ilipiga san kelele kuhusu hii ishu lakini sasa kuna ukikya wa ghafla, na ksheshe kubwa ni kushindwa kuunganisha tukio la kibanda na Lwakatare.
Mungu ibariki Tanzania!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom