ITV Tanzania:Kibanda awaambia Polisi waseme ukweli

Mwenyekiti wa jukwaa la wahariri na mhariri mtendaji wa new habari absalom kibanda amerejea leo nchini na kulakiwa na watanzania wapenda amani na maendeleo. Wanachi wengi sana walijitokeza huku wengine wakitokwa na machozi ya huruma huku wakiwa hawaamini kumuona tena kibanda akiwa na siha njema namna ile.

Kibanda amewashukuru watanzania kwa dua zao wakati wote tangu apatwe na masibu yale na ameahidi kuelezea mkasa mzima jinsi ulivyokuwa na kutoa leads ya ni nani hasa wahusika wa utesaji dhidi yake...

pole sana kibanda na karibu nyumbani...mungu azidi kukujaala afya njema uendelee kulijenga taifa lako...damu yako haijamwagika bure.
 
Habari hizi nikizisikia napatwa sana na ghadhabu!
Mungu akupe uzima Ndugu Kibanda,
nasepa hapa nikiendelea ntaishia "jela"
 
hahhahah amesema pia matukio yameanza toka awamu ya nne iingie madarakani eight years back ! sijui alimaanisha nini, na kasema hataki kuwapoint wasiohusika, hapo nikamfikiria yule jamaa wa chadema aliyeko lupango.
 
pole kibanda
pole dr ulimboka
pole daudi mwangosi
pole dr mwakyembe
pole prof mwandosya
poleni wanyakyusa
poleni wana mbeya
poleni waTANGANYIKA
 
Mwenyekiti wa jukwaa la wahariri na mhariri mtendaji wa new habari absalom kibanda amerejea leo nchini na kulakiwa na watanzania wapenda amani na maendeleo. Wanachi wengi sana walijitokeza huku wengine wakitokwa na machozi ya huruma huku wakiwa hawaamini kumuona tena kibanda akiwa na siha njema namna ile.

Kibanda amewashukuru watanzania kwa dua zao wakati wote tangu apatwe na masibu yale na ameahidi kuelezea mkasa mzima jinsi ulivyokuwa na kutoa leads ya ni nani hasa wahusika wa utesaji dhidi yake...

pole sana kibanda na karibu nyumbani...mungu azidi kukujaala afya njema uendelee kulijenga taifa lako...damu yako haijamwagika bure.

Kuna mwenzake alisema kauli kama hiyo lakini ametuweka kwenye mataa, labda watesaji wake ni wa upande mwengine sio ule wa mwenzake!
 
KIBANDA AMEUDI NYUMBANI LEO MCHANA
Tuesday, 04 June 2013

Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri Tanzania na Mhariri Mtendaji wa New Habari, Ndugu yetu Absalom Kibanda amerejea LEO saa 7:00 mchana na ndege ya SAA kutoka Afrika Kusini alikokuwa amekenda kwa ajili ya Matibabu.

Watanzania wote wenye nia njema ya kumpokea na kumfariji, walijumuika pamoja uwanjani JK Nyerere International.
 
Angoje kwanza kaka ulimboka atuelezee kilichompata ndo nae ataelezea. Take your your bro, its not like we are going anywhere.
 
Kibanda hana sababu ya msingi ya kuwalaumu polisi! Polisi ni kama mbwa tu!! Mwenye mbwa ndiye anafahamu fika kwa nini mbwa wake aling'ata!! Ukweli wote Kikwete anaufahamu!! Ya nini kutafuna maneno?
 
Kibanda hana sababu ya kutafuta mchawi! Mchawi wake ni Kikwete!!! Huyu anajua siri zote za mauaji na utesaji unaoendelea nchini kwa sasa!!!
 
Anategemea polisicm watasema nini wakati uharamia umefanywa na serikali ya dhaifu kwa kuwatumia usalama wa taifa? Labda kama hao pilisi nao wameyachoka macho, meno na kucha zao!
 
Kibanda umekuja kwa mbwembwe sana ukisema hautanyamanza sasa ss usitufanya tuweke masikio juu kusubili kijacho kutoka kwako harafu baadaye kimyaaaaaa au huwa mnajinunua wenyewe maana mbwembwe huwa na wandishi wa habari baada ya hapo kimyaaaaaaaaaaaaaaa lakini pole sana
 
nilimsikia anasema kwanini ktk hii miaka nane ambayo jk amekaa madarakani kumekuwa na matukio mengi ya ukatili kwa waandishi wa habari? anasema hawezi kusubiri asemewe kama wengine hivyo atalipua bomu soon. sisi yetu macho na masikio

Awe makini kabla hajalipua Bomu anaweza akawa ameshalipuliwa yeye.
 
Kama yeye hawezi kujisemea anadhan polis watamsemea? Naona mbwembwe tu za kutafuta mlango wa kunegotiate na watesi wake!. Angekuwa muwazi tu kwa kutangaza bei yake aitakayo wampatie ili awasitiri au kinyume chake!
 
Tatizo la hawa watu wakirudi kutoka huko SA wanakuja na story nyingi za "nitataja"..."nitataja"mwisho wa siku hakuna kitu kwani yule Doctor si alikuja na ngonjera hizi hizi?!
 
nilimsikia anasema kwanini ktk hii miaka nane ambayo jk amekaa madarakani kumekuwa na matukio mengi ya ukatili kwa waandishi wa habari? anasema hawezi kusubiri asemewe kama wengine hivyo atalipua bomu soon. sisi yetu macho na masikio

Kama ni msemaji na anataka kusema ukweli hana sababu ya kusubiri Polisi imsemee.
Asilete zile za Dr. Ulimboka; "Muda ukifika,baada ya mapumziko, nitasema ukweli".
Dr. Ulimboka bado yuko mapumzikoni tu?

Kama Kibanda au Gorofa ana la ukweli aliseme, asilete ya:
Njenje we njenje
Njenje leo njenje
Njenje we njenje
Na kipara moto njenjeee

Ni bora aseme huo ukweli mapema kuliko kutoa vitisho, watu wa vitu vya ncha kali wanaweza kumalizia na hilo jicho la pili au hata kumrudisha kwa udongo.
 
Kibanda umekuja kwa mbwembwe sana ukisema hautanyamanza sasa ss usitufanya tuweke masikio juu kusubili kijacho kutoka kwako harafu baadaye kimyaaaaaa au huwa mnajinunua wenyewe maana mbwembwe huwa na wandishi wa habari baada ya hapo kimyaaaaaaaaaaaaaaa lakini pole sana

Ikiwezekane kufikia jumamosi atoe yale yaliyo moyoni mwake..ajue wazi kwamba wakati anajiandaa kutupa ukweli upande wa pili nao wanajipanga kumzima,tusubiri tuone mkuu.
 
Una maana wale watoa kucha na meno bila ganzi watamrudia tena,ili waje wamnyofoe hilo jicho la pili lililobaki?!

Na pamoja na mzee wa movie ya kichaa wa Kenya,kuwa hadi leo,baada ya miezi mitatu hajamkamata hata mtuhumiwa mmoja,wa tukio la kutekwa kwa Kibanda,bado hata hivyo,JK,amemtunukia utumishi uliotukuka na amempandisha na cheo!!

watamuwahi kumkata ulimi asiweze kuongea na jicho lililobaki asiweze kuandika then game the end.
 
pole kibanda
pole dr ulimboka
pole daudi mwangosi
pole dr mwakyembe
pole prof mwandosya
poleni wanyakyusa
poleni wana mbeya
poleni waTANGANYIKA

CCM wanafanya makusudi kutesa wana Mbeya!! Wazee wa Mbeya wangetoa tamko la sivyo, Sugu is next
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom